Kwa mtazamo wangu imfikia wakati sasa hesabu lisiwe somo la lazima(compulsory)

Kwa mtazamo wangu imfikia wakati sasa hesabu lisiwe somo la lazima(compulsory)

ligendayika

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2012
Posts
1,183
Reaction score
198
Kwa sasa hesabu au math ni somo la lazima sasa kwa uhaba huu wa walimu shule nyimgi za kata hazina walimu si hesabu tuu hata masomo mengine ya sayansi. Kwa hali hii kwangu mimi sioni sababu ya serikari kuendelea na kusema hesabu ni compulsory ilihali somo hilo kwa shule nyingi halifundishwi ipasavyo hapa nchini. Nadhani serikari ingelifikilia jambo hili ni kama kuwaumiza wale ambao hawasomi kwa kukosa walimu.
 
solution ya tatizo la uhaba wa walimu si kufuta somo na hasa kama somo lenyewe ni hesabu. somo la hesabu ni la lazima ktk makuzi ya akili na ufahamu. karibu tutakuwa vilaza wa dunia tukiwaza kufuta hesabu ktk dunia ya leo ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. tunahitaji walimu zaidi na tunahitaji walimu weledi na bora wanaojua kuwaelekeza vijana.
 
kwani sasa hivi sio la lazima?au una somo lako la hesabu jingine,au unaongelea kwa advance wenye comb zisiso na hesabu
 
u must be a fellow with ill intentions for this country....do you realise what type of nonsense you have written?tena me nasema passmark ipandishwe na mtoto yoyote pasipo kuifikia asivuke darasa alilopo.... kama unafikra kama hizi katika challenge za maisha ulizonazo basi you are extra cheap...difficult challenges dont need cheap solutions like this...serious buddy think???!!!!
 
solution ya tatizo la uhaba wa walimu si kufuta somo na hasa kama somo lenyewe ni hesabu. somo la hesabu ni la lazima ktk makuzi ya akili na ufahamu. karibu tutakuwa vilaza wa dunia tukiwaza kufuta hesabu ktk dunia ya leo ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. tunahitaji walimu zaidi na tunahitaji walimu weledi na bora wanaojua kuwaelekeza vijana.

sio karibu tutakuwa tayari maana sa hivi hata logic hamna kwenye maneno na siasa zetu..simple logic which is maths should tell if this then what next but nobody is thinking lack of proper math.....kudekeza watoto hataki chakula unampa maziwa utampa hadi lini na miaka 60 upuuzi tunaibiwa kila mahali kwa kukosa basics tu na logics....
 
Kwa sasa hesabu au math ni somo la lazima sasa kwa uhaba huu wa walimu shule nyimgi za kata hazina walimu si hesabu tuu hata masomo mengine ya sayansi. Kwa hali hii kwangu mimi sioni sababu ya serikari kuendelea na kusema hesabu ni compulsory ilihali somo hilo kwa shule nyingi halifundishwi ipasavyo hapa nchini. Nadhani serikari ingelifikilia jambo hili ni kama kuwaumiza wale ambao hawasomi kwa kukosa walimu.

Wewe ni ngwini
 
Wewe ni ngwini

Labels kama hizi ni useless na zinaendana sana na mwanzilishi wa mada hii. For disclosure, I am a ngwini par excellence, actually a ngwini by choice. I am a ngwini who advocates for a well-rounded basic education. Elimu yetu TZ inajaribu ku-compartmentalize hata basic education na kufanya masomo fulani kuwa ya ziada. Isitoshe watu wanafundishwa kukariri tu mambo. Masomo hayafundishwi kwa namna ambayo watu wataelewa umuhimu wa kile wanachosoma. Huku ni kukoleza ujinga. Nitoe mifano michache. Watu wanapuuzia Kiingereza na kuwaachia "ngwini". Halafu baadae mtu amekuwa mhandisi anashindwa kuandika Kiingereza. Au mtu anaenda kusoma nje, kasheshe Kiingereza. Mtu unapuuzia hesabu, baadae anashindwa hata kufanya logical reasoning, anashindwa kutumia very basic data and statistics kueleza jambo hata rahisi sana. Utamsikia mtu anasema kama vile sifa kwamba: historia haikuwa somo langu. Atakapoambiwa kwamba yeye na watu wake hawana mchango ktk maendeleo ya binadamu anakasirika lkn hawezi kupinga. Hata kuona tu teknolojia inavyobadilika na nafasi yetu au uwezekano wetu wa kujiletea maendeleo, hawezi.... Tutakaa na kungoja wazungu watuletee MISAADA. nk. Ningeweza kusema mengi, lkn inachosha na inaudhi sana. Kwa nini watu wanafikiri ukisoma hisabati basi huhitaji kujua jiografia, au ukisoma historia basi huhitaji kujua bailojia? Hii ni kwa sababu elimu yetu inalenga kwenye mitihani tu na si kuelimika kwa ajili ya maisha yako. Majirani wanatuita "half-educated."
Kwa hivyo basi, mtu anapotoa wazo la kutisha kama hili la kufanya hisabati kuwa somo lisilo la lazima, kumpuuzia tu kwa kusema: ngwini wewe, inaonyesha upeo mdogo wa mtazamo juu ya elimu ya TZ. maoni ya mtu huyo kwa kweli ni dalili mbaya sana ya matatizo ya elimu yetu. ni lazima tufikiri kwa kina nini cha kufanya.
 
Back
Top Bottom