TATHMINI YANGU KATIKA UFUNGUZI WA KAMPENI WA VYAMA VIKUU VITATU,CCM,CHADEMA NA ACT WAZALENDO.
Leo 10:15am 30/08/2020
Vyama vya siasa nchini Tanzania vimeanza safari ya kampeni kutangaza sera kwa Watanzania kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na madiwani, Watanzania watakwenda kusikiliza sera za wagombea, Watanzania watakwenda kuchagua Chama chao kilicho bora, Watanzania watakwenda kumchagua Rais mwenye kuongelea hatma ya kizazi cha Watanzania leo,kesho na kesho kutwa.
Kwa lugha nyingine tunasema kwamba sasa kumekucha wakati ambapo vyama vyote vimejiweka mguu sawa kuanza kushambulia majukwa kwa hoja na vijembe vya hapa na pale vikijaribu kuwavutia wapiga kura kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa mwezi wa Oktoba,Chama Cha Mapinduzi CCM kilizindua kampeni zake Jana tarehe 29 jijini Dodoma,wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kilizindua kampeni zake tarehe 28 Mbagala,jijini Dar es Salaam huku Chama Cha ACT Wazalendo kikizindua tarehe 30 Mjini Mtwara,
Kinadharia,iko hivi,Katika Uchaguzi huu Mkuu,Mwajiri ni Watanzania wenye nchi yao,kila baada ya Miaka mitano, Watanzania wanaiboresha nchi yao kwa kufanya marekebisho kupitia Uchaguzi,Miaka mitano ya uchaguzi ilirekebisha ruksa,Miaka mitano ya uchaguzi ilirekebisha ubinafsishaji,Miaka mitano ilirekebisha na kukemea rushwa na ufisadi,hivyo basi kila Uchaguzi Watanzania wanaifanyia tathmini nchi yao,
Katika mpangilio, Watanzania ni waajiri,Mwajiriwa aliyepo sasa ni Chama Cha Mapinduzi CCM,watafuta ajira ni Chadema,Act Wazalendo,Chauma,Cuf,Nccr Mageuzi,Tlp na vyama vingine vya Upinzani,hivyo basi Uchaguzi unalenga kumfanyia tathmini Mwajiriwa aliyepo,kwa hiyo CCM inafanyiwa tathmini na Watanzania yaani "performance appraisal" lakini Chadema,Act Wazalendo,Cuf wao watakwenda kufanya interview kama muomba kazi mpya kabisa, wapinzani wanafanyiwa "job interview" na Watanzania.
Kwa maana nyingine CCM haipo sawa na wapinzani kwa namna nilivyoeleza hapo juu,CCM inafanyiwa tathmini ya kuwepo kwake kazini na kama tuonavyo wamejitahidi kuonyesha Utendaji na wanaweza kuendelea na ajira yao,wakati wapinzani wanafanyiwa job interview yenye full recruitment process hata ikiwezekana wapitie midahalo ya kuwahoji kitu itakuwa si kumtendea haki Chadema au Act Wazalendo kufanya mdahalo na CCM yaani job seeker afanye mdahalo na employee lazima employee atashinda tu,
Mdahalo utakaohusu utendakazi kwenye performance review and appraisal kwa CCM itakuwa kati ya CCM na mwajiri ambae ni Watanzania,CCM imefanya kazi kwa kiwango gani na kwa nini CCM ipewe nafasi tena ya kuwatumikia Watanzania,Huu ndio upekee wa CCM kama Mwajiriwa akienda kuchuana na waomba ajira Chadema,Act Wazalendo,Cuf,Chauma,Nccr Mageuzi na vyama vingine,
-Tathmini yangu kwa wagombea wa vyama vikuu vitatu,
Kwa mtazamo wangu naona Ndugu Tundu Lissu amejawa Chuki na visasi,
Ndugu John Pombe Magufuli yuko na moyo mweupe wenye furaha bila vinyongo, chuki, visasi,
Ndugu Bernard Membe yeye ni kazi na bata,ukimya wake umeanza kuchukuliwa na Hashimu Rungwe Mgombea wa Chauma anayegawa ubwabwa na nyama,
Ndugu John Magufuli anapangilia sana maneno kuepuka kuropoka ovyo,hotuba yake ya Jana mwanzo hadi mwisho alikuwa akitaja Mambo Makuu aliyoyafanya kwa Miaka mitano aliyokuwa Madarakani,
Ndugu Tundu Lissu uongea tu kile kinachomjia kichwani kwa wakati huo,anaweza kuacha kuhutubia kutuliza wahuni waliojaa mbele yake,kuwatuliza na kujiambukiza kwao,
Ndugu John Pombe Magufuli anapenda sana utani unao tokana na utamaduni wa kitanzania,
Ndugu Tundu Lissu yeye kwake kila kitu ni nongwa kwa kifupi hana jema kwake kila kitu ni kibaya,atasema Ujenzi wa reli ya Umeme ni kupoteza hela,atasema yeye ana damu ya Kenya na Ubelgiji,
Ndugu John Magufuli yeye ni mtulivu,anapenda kumtanguliza Mungu mbele,
Ndugu Tundu Lissu yeye ana siasa za asili ya kiuhuni uhuni yaani haziko ki presidential,mfano akihutubia na kusema yeye hatomwachia Mungu,sasa sijui atamwachia nani?
Ndugu John Pombe Magufuli anaweka sana utaifa mbele,anawaza watoto na wajukuu waje kupata ajira,anaanzisha Ujenzi wa bwawa la Umeme,ambalo litatoa Umeme mwingi na kuchochea Ujenzi wa Viwanda ambao utatoa ajira kwa Watanzania Milioni 60,
Ndugu Tundu Lissu yeye ni mwanaharakati zaidi yupo tayari kwa chochote ikiwa tu kinamletea political popularity.
Nimalizie kwa kusema tathmini ya Uzinduzi wa kampeni inatupa picha ya nani amejiandaa na nani hajajiandaa,Nani atakwenda kushinda na nani atakwenda kushindwa,CCM imejipanga,CCM inajibeba kwa Utendaji wake uliotukuka,Chadema inapiga jalamba lakini haina maajabu yoyote,Act Wazalendo wao eti wanawaandaa wafuasi wao kama vile Maalif Sefu au Membe ndio Jemedari Mkuu wa Majeshi,
kwa hiki kipindi kifupi ambacho viongozi wa vyama mbalimbali wamekuwa wakitoa hotuba zao majukwaani,utaweza kunyambua yafuatayo;
1.Kuna wagombea waliojiandaa kushinda Uchaguzi.
2.Kuna wagombea waliojiandaa kushindwa Uchaguzi.
Wagombea waliojiandaa kushinda Uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 wanaeleza sera zao kwa ustaarabu na unyenyekevu mkubwa sana,Kwa kufanya hivyo tu,wameshashinda tayari kwani Watanzania wanapenda zaidi amani.
Kwa wagombea waliojiandaa kushindwa Uchaguzi huu wa 2020, wao hawana mpango kutoa sera zao, bali hutumia muda mwingi(95%) kukejeli,kubeza,kulaumu,kulalamika,kutukana na kulia lia kuhimiza Maandamano kwa wafuasi wao badala ya kueleza sera zao,
Hayo yote hutolewa kwa lugha kali za kutisha na kuwaogofya Watanzania.
Maoni yangu ni kwamba, Watanzania wa leo si wajinga kiasi hicho,wanasikiliza na kupima sera na hoja kwa kina,kama kweli wagombea wanataka kuchaguliwa katika Uchaguzi huu,hawanabudi kubadili staili ya Kampeni zao majukwaani, yaani kupiga kampeni za kistaarabu.
Amini, Amini nawaambia, hakuna mtanzania hata mmoja atakayekubali kuacha shughuli zake zinazomwingizia kipato na kwenda kushiriki Maandamano yasiyo na kichwa wala miguu,na ningeshauri anayehitisha Maandamano yeye akae mbele,maana uwa wanakimbilia Ulaya ndio wanatangaza andamaneni,si hivyo tena,Sisi Watanzania si wa kututumia hovyo hovyo kwa maslahi yenu binafsi.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business,
-Master's in Leadership and Management.
-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.