Mkwawe
JF-Expert Member
- Jun 10, 2016
- 3,132
- 5,508
Niwapongeze watanzania (hususani watanganyika) kipekee zaidi watumishi wa umma kwa kufanikisha nchi yetu kuwa na moja ya miundombinu na usafiri wa kisasa nchini hakika pongezi ziende kwenu na naamini mtamsamehe magufuli kwa kutiwapandisha madaraja ili tunufaike tunu njema kama hii.
Lakini siku zote mbongo ni mbongo, Mimi siyo nabii ila ninaongea hili jambo kwa ujasiri na uhakika mkubwa mkubwa kuwa ndani ya miaka 6 chini ya serikali ya CCM hii reli inaenda KUFA kifo kibaya sana siyo cha mende ila cha vunjajungu dume. Vunjajungu dume akishampanda jike tu yeye anageuka chakula cha vunjajungu jike na hapo ndo umauti wake hufikia. Sasa hii SGR unaenda kuwa ni mradi wa hasara sana kw taifa hili sio kwa kuwa umetekelezwa kwa gharama! La! ila kwa kuwa utatalekezwa kwa gharama
Nawajua watanzania, hawajawahi kuwa dhahiri (serious) kila kitu kwao ni 10%
Naahidi kutoa sh 700k kwa yeyote atakayekuwa wa kwanza kuufufua huu uzi baada ya miaka 6 na kunionesha SGR ikifanya kazi
Nieleweke namaanisha ndani ya miaka 6 hii SGR haitakiwi kusitisha huduma zake ikitokea imesitisha huduma zake hata kwa wiki kadhaa au mwezi mmoja au miezi miwili au kadhaa tafsiri take utabiri wangu utakuwa umetimia, kwa maana ile integrity na durability iliyotegemewa si yenyewe
Nawasilisha