Kwa mtazamo wangu naona Treni ya SGR haitachukua miaka 6 itakufa

Kwa mtazamo wangu naona Treni ya SGR haitachukua miaka 6 itakufa

Niwapongeze watanzania (hususani watanganyika) kipekee zaidi watumishi wa umma kwa kufanikisha nchi yetu kuwa na moja ya miundombinu na usafiri wa kisasa nchini hakika pongezi ziende kwenu na naamini mtamsamehe magufuli kwa kutiwapandisha madaraja ili tunufaike tunu njema kama hii.

Lakini siku zote mbongo ni mbongo, Mimi siyo nabii ila ninaongea hili jambo kwa ujasiri na uhakika mkubwa mkubwa kuwa ndani ya miaka 6 chini ya serikali ya CCM hii reli inaenda KUFA kifo kibaya sana siyo cha mende ila cha vunjajungu dume. Vunjajungu dume akishampanda jike tu yeye anageuka chakula cha vunjajungu jike na hapo ndo umauti wake hufikia. Sasa hii SGR unaenda kuwa ni mradi wa hasara sana kw taifa hili sio kwa kuwa umetekelezwa kwa gharama! La! ila kwa kuwa utatalekezwa kwa gharama

Nawajua watanzania, hawajawahi kuwa dhahiri ( serious) kila kitu kwao ni 10%

Naahidi kutoa sh 700k kwa yeyote atakayekuwa wa kwanza kuufufua huu uzi baada ya miaka 6 na kunionesha SGR ikifanya kazi

Nieleweke namaanisha ndani ya miaka 6 hii SGR haitakiwi kusitisha huduma zake ikitokea imesitisha huduma zake hata kwa wiki kadhaa au mwezi mmoja au miezi miwili au kadhaa tafsiri take utabiri wangu utakuwa umetimia, kwa maana ile integrity na durability iliyotegemewa si yenyewe

Nawasilisha
Huyu ndio pure Tanzanian

Hapendi kabisa kuona nchi inafanikiwa
 
Vitu vingi vilivyo anzishwa kwa mbwembwe na vilivyo tumia gharama kubwa kuvifanya viwe mara nyingi havina mwendo mrefu.

Inakuwa hivyo kwa vile kuanza vinaanzishwa kwa propaganda za kisiasa na kuviendesha vinaenda kisaasa na maslahi ya wana siasa kwa ujumla wake, hivyo hatuna matarajio marefu na huu mradi wa treni hata hio miaka sita ya mleta mada huwenda ikawa ni mingi mno!

Hata hivyo jana sio leo na kesho hailingani na leo, huwenda ikawa kinyume chake.
 
Haihitaji rocket science kujua kuwa huo mradi utakufa au kuchakaaa mpaka efficiency yake kupungua below 50 percent. Angalieni mradi wa mabasi ya mwendokasi. Trend ya uendeshaji wake inatosha kutoa utabiri juu ya SGR.
Sababu kubwa ya mbili zitaiangusha SGR
MOJA:KUKOSEKANA UTAMADUNI WA UKARABATI. _Yaaani tunasubiri vitu viharibike hadi vinashindwa kurekebishika au gharama inakuwa kubwa na tuna opt kwenye shortcuts.
MBILI_Wizi ,ten percent masilahi binafsi nauongozi /usimamizi mbovu. Haya ni magonjwa sugu kila sector. Mnayafahamu haya. Wanaosema mtoa mada ni mchawi hawajatumia ubongo wao vizuri kudadavua mwenendo wa miradi yetu.
 
Mkuu, nchi zote zilizoendelea all means of transportation zinafanya kazi kwa ufanisi. Study shows ufanisi wa njia moja unavyoongezeka na njia zingine zinakua as well.

Kudhani reli itaua biashara ya malori is being short-sighted, realistically biashara ya malori itaongezeka zaidi. Wateja watakua na option na watu wengi wataitumia TZ maana usafiri utakua wa uhakika na ushindani wa nguvu.

Nchi kuendelea inahitaji reli bora, kilimo chenye tija na umeme wa kutosha na uhakika; the human capital goes without saying. That's it.
Reli ya Kaskazini iliyofufuliwa na Magufuli inafanya kazi?
Sasa shirika lishindwe reli na treni za maintenance ndogo waje wafanye SGR kwa ufanisi?

Serikali isindwe kuendesha mabasi ya mwendokasi, izidiwe na hata Benjamin Makundi wa BM ije iweze SGR. Serikali hii hii inayoshindwa Air Tanzania inakula hasara wakati FastJet kwa nauli ya laki Dar to Mwanza bado walikuwa wanapata faida mpaka wakafukuzwa.
 
Toa solution SGR isife. Unapta faida gani kutabiria mradi kama huu mabaya, kijana mdogo mchawi kama Kalaga baho
Wachawi ni VIONGOZI wa CCM wasiokuwa na Akili. It is obvious SGR itakata pumzi mapema Kama unavoona mwendokasi

Ilianza kwa mbwembwe now ni kusukuma siku

Shida ni CCM
 
Toa solution SGR isife. Unapta faida gani kutabiria mradi kama huu mabaya, kijana mdogo mchawi kama Kalaga baho
Kwa sababu uzoefu unaonyesha kwamba serikali haijawahi kuanzisha na kusimamia mradi wo wote ule na ukaendelea kwa mafanikio na tija. Na uzoefu, wanasema, ndiye mwalimu mzuri!

Mradi hata uwe mzuri namna gani serikali ikitia mguu tu na mradi ukaitwa mradi wa umma basi hesabu maumivu. Tazama mwendokasi. Mamilioni ya pesa yanayokusanywa pale kwa siku na mradi ulivyo. Itazame Air Tanzania. TANESCO...Na maviwanda mengi tu.

Kwanza wananzengo wataanza kuharibu vifaa kwa makusudi. Na hakuna mtengenezaji. Miezi 6 tu mabehewa yatakuwa choka mbaya mkangafu. Vyoo havitamaniki...Na hasara zitaanza kurundikana haijalishi kama ina mamilioni ya abiria...na mizigo!

Hata mimi sina matumaini nayo. Let them prove me wrong! Niko nimekaa paleeee!
 
Binafsi naona kilichoandikwa sio chuki wala uchawi
Ni kama motisha kwa wahusika wa hiyo project kuhakikisha wana-prove wrong kilichoandikwa...kwasababu najua wapo humu,na uzi wata/wawameshauona
Jojo!

GT! ❤️
 
Reli ya Kaskazini iliyofufuliwa na Magufuli inafanya kazi?
Sasa shirika lishindwe reli na treni za maintenance ndogo waje wafanye SGR kwa ufanisi?

Serikali isindwe kuendesha mabasi ya mwendokasi, izidiwe na hata Benjamin Makundi wa BM ije iweze SGR. Serikali hii hii inayoshindwa Air Tanzania inakula hasara wakati FastJet kwa nauli ya laki Dar to Mwanza bado walikuwa wanapata faida mpaka wakafukuzwa.

Toa solution au hili nalo linahitaji katiba mpya?
 
Kwa sababu uzoefu unaonyesha kwamba serikali haijawahi kuanzisha na kusimamia mradi wo wote ule na ukaendelea kwa mafanikio na tija. Na uzoefu, wanasema, ndiye mwalimu mzuri!

Mradi hata uwe mzuri namna gani serikali ikitia mguu tu na mradi ukaitwa mradi wa umma basi hesabu maumivu. Tazama mwendokasi. Mamilioni ya pesa yanayokusanywa pale kwa siku na mradi ulivyo. Itazame Air Tanzania. TANESCO...Na maviwanda mengi tu.

Kwanza wananzengo wataanza kuharibu vifaa kwa makusudi. Na hakuna mtengenezaji. Miezi 6 tu mabehewa yatakuwa choka mbaya mkangafu. Vyoo havitamaniki...Na hasara zitaanza kurundikana haijalishi kama ina mamilioni ya abiria...na mizigo!

Hata mimi sina matumaini nayo. Let them prove me wrong! Niko nimekaa paleeee!

Toeni solution au mnapata faraja kusema "tulisema itakufa tu"? Madeni ya ujeni wa hii SGR yatalipwa either inatumika au haitumiki na wote mtakamuliwa.
 
Kabla SGR haijafa tayari mtoa mada atakuwa amejifungua mapacha
 
Toeni solution au mnapata faraja kusema "tulisema itakufa tu"? Madeni ya ujeni wa hii SGR yatalipwa either inatumika au haitumiki na wote mtamtakamuliwa
Solution? Mwigulu au Kadogosa utampa solution gani?

Wewe huko ndiyo una exposure labda utusaidie huko. Wanafanyeje wazungu huko mpaka treni zao zinadumu miaka na miaka tena kwa faida? Ibeni maarifa huko mtuletee. Huku ni kama vile tulishakwama! Huku tunawaza upigaji tu!
 
Hiyo Laki 7 utaitoaje wakat tunakuzika mwezi November mwaka huu mchawi mkubwa wewe?

Mnachoweza ni kutabir mabaya Tu na mnaona ufahar kabisa.
Hatutabiri mabaya, tumeyazoea kuyaona ndo maana hata kwa hili tunajua linaweza kufuata mkumbo uleule tu
 
Niwapongeze watanzania (hususani watanganyika) kipekee zaidi watumishi wa umma kwa kufanikisha nchi yetu kuwa na moja ya miundombinu na usafiri wa kisasa nchini hakika pongezi ziende kwenu na naamini mtamsamehe magufuli kwa kutiwapandisha madaraja ili tunufaike tunu njema kama hii.

Lakini siku zote mbongo ni mbongo, Mimi siyo nabii ila ninaongea hili jambo kwa ujasiri na uhakika mkubwa mkubwa kuwa ndani ya miaka 6 chini ya serikali ya CCM hii reli inaenda KUFA kifo kibaya sana siyo cha mende ila cha vunjajungu dume. Vunjajungu dume akishampanda jike tu yeye anageuka chakula cha vunjajungu jike na hapo ndo umauti wake hufikia. Sasa hii SGR unaenda kuwa ni mradi wa hasara sana kw taifa hili sio kwa kuwa umetekelezwa kwa gharama! La! ila kwa kuwa utatalekezwa kwa gharama

Nawajua watanzania, hawajawahi kuwa dhahiri (serious) kila kitu kwao ni 10%

Naahidi kutoa sh 700k kwa yeyote atakayekuwa wa kwanza kuufufua huu uzi baada ya miaka 6 na kunionesha SGR ikifanya kazi

Nieleweke namaanisha ndani ya miaka 6 hii SGR haitakiwi kusitisha huduma zake ikitokea imesitisha huduma zake hata kwa wiki kadhaa au mwezi mmoja au miezi miwili au kadhaa tafsiri take utabiri wangu utakuwa umetimia, kwa maana ile integrity na durability iliyotegemewa si yenyewe

Nawasilisha
mtabiri tambi tambi kutoka Manyoni yuko kazini
 
Back
Top Bottom