Kwa mtazamo wangu naona Treni ya SGR haitachukua miaka 6 itakufa

Kwa mtazamo wangu naona Treni ya SGR haitachukua miaka 6 itakufa

Nimechoka kusikia kuwa mwenyekiti wa bodi TRC naye alisafiri bure kwenda Moro na kurudi Dar! Na huenda na sekretari wake na waandishi walikuwemo.
Usikute hata walinzi wa terminus nao walisafiri
 
Ila kote mimi nakubali ila hako kamsemo nakachukia sana
Unajua mwanahiphop JCB?

Ndo mwanzilishi wa huu msemo
"Ukisikia paaah ujue imekukosa
Alolenga Hana shabaha amefanya makosa"


Labda uwe umezaliwa 2006 ndo usiujue
 
Unajua mwanahiphop JCB?

Ndo mwanzilishi wa huu msemo
"Ukisikia paaah ujue imekukosa
Alolenga Hana shabaha amefanya makosa"


Labda uwe umezaliwa 2006 ndo usiujue
Bravo unamakadilio mazuri 💯
 
YAANI HAPA BAADO
😂😂😂

Shirika la Reli Tanzania (TRC), limeomba radhi kufuatia hitilafu ya umeme iliyojitokeza kati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete na kusababisha treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili usiku wa jana July 30, 2024 ambapo limesema taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system).

Taarifa iliyotolewa leo July 31,2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano - TRC, Jamila Mbarouck imesema
“Hitilafu ilisababisha umeme kukatika kituo cha kupoozea umeme namba 7 (Godegode) ambayo kitaalamu hujulikana kama (Instanteneous Overcurrent Protection Trip) majira ya saa 4:20 usiku”

“Mafundi wa TRC walifanikiwa kutatua changamoto na kurejesha umeme saa 6:30 usiku na treni kuendelea na safari kuelekea Dodoma na kuwasili Dodoma majira ya saa 7:57 usiku, Shirika la Reli Tanzania linaomba radhi kwa usumbufu” #MillardAyoUPDATES
 
Itahujuliwa si muda mrefu, kuna mi fisi maji ina malori semi kibao - ikale wapi? Takukuru.
 
Niwapongeze watanzania (hususani watanganyika) kipekee zaidi watumishi wa umma kwa kufanikisha nchi yetu kuwa na moja ya miundombinu na usafiri wa kisasa nchini hakika pongezi ziende kwenu na naamini mtamsamehe magufuli kwa kutiwapandisha madaraja ili tunufaike tunu njema kama hii.

Lakini siku zote mbongo ni mbongo, Mimi siyo nabii ila ninaongea hili jambo kwa ujasiri na uhakika mkubwa mkubwa kuwa ndani ya miaka 6 chini ya serikali ya CCM hii reli inaenda KUFA kifo kibaya sana siyo cha mende ila cha vunjajungu dume. Vunjajungu dume akishampanda jike tu yeye anageuka chakula cha vunjajungu jike na hapo ndo umauti wake hufikia. Sasa hii SGR unaenda kuwa ni mradi wa hasara sana kw taifa hili sio kwa kuwa umetekelezwa kwa gharama! La! ila kwa kuwa utatalekezwa kwa gharama

Nawajua watanzania, hawajawahi kuwa dhahiri (serious) kila kitu kwao ni 10%

Naahidi kutoa sh 700k kwa yeyote atakayekuwa wa kwanza kuufufua huu uzi baada ya miaka 6 na kunionesha SGR ikifanya kazi

Nieleweke namaanisha ndani ya miaka 6 hii SGR haitakiwi kusitisha huduma zake ikitokea imesitisha huduma zake hata kwa wiki kadhaa au mwezi mmoja au miezi miwili au kadhaa tafsiri take utabiri wangu utakuwa umetimia, kwa maana ile integrity na durability iliyotegemewa si yenyewe

Nawasilisha
Uchawi upo,kwahiyo ushaanza kuroga tunguli kama zote,maendeleo haya yana faida
 
Huu mradi ukifa na hao viongozi wafe.....

Ova
 
Back
Top Bottom