Kwa mtazamo wangu naona Treni ya SGR haitachukua miaka 6 itakufa

Kwa mtazamo wangu naona Treni ya SGR haitachukua miaka 6 itakufa

Maneno yanaumba ila kusema kweli bora ingejengwa barabara ya njia 5 mpaka huko ilipoishia hiyo reli kuliko hiyo White elephant project ya Snake slide iron way.....
Anyway naunga mkono hoja!
#ilawabongokwauchawi!!!
😁😁
Huu mradi mzuri sana shida Sasa anayeusimamia ihiiiiiiii

ila nashukuru kwa kuniunga mkono mchawi mwenzangu
 
Roho za kichawi hizi na watu wachawi ni watu wasiopenda maendeleo ndio wana tabia hizi, treni itakuwepo sana tu hata miaka 60 ijayo
Kama mtanzania nitafurahi ikifika miaka 60 unayosemea ila kama mtu mkweli nitafurahi kuona nilichosema kilikuwa sahihi
 
Naelewa wasiwasi wako juu ya watanzania kuhusu matumizi mabaya ya miundombinu na kutokujali. Utabiri wako unaangukia kwenye hii reli iliyojengwa mpaka Makutupola au unaongelea pia reli ambayo inajengwa hivi sasa ya kwenda Mwanza na Kigoma?? ... kwamba nazo zitakufa hata kabla ya kuanza baada ya miaka sita?
 
Mkuu, nchi zote zilizoendelea all means of transportation zinafanya kazi kwa ufanisi. Study shows ufanisi wa njia moja unavyoongezeka na njia zingine zinakua as well.

Kudhani reli itaua biashara ya malori is being short-sighted, realistically biashara ya malori itaongezeka zaidi. Wateja watakua na option na watu wengi wataitumia TZ maana usafiri utakua wa uhakika na ushindani wa nguvu.

Nchi kuendelea inahitaji reli bora, kilimo chenye tija na umeme wa kutosha na uhakika; the human capital goes without saying. That's it.
Trc baada ya kutangaza viwango vya nauli wamiliki wa mabasi wameanza kulalamika yaani Tanzania bogus wapo kila mahali, wote hufikiria msosi wa leo tu hawana hata future

These people are pathetic pthooo!
 
Naelewa wasiwasi wako juu ya watanzania kuhusu matumizi mabaya ya miundombinu na kutokujali. Utabiri wako unaangukia kwenye hii reli iliyojengwa mpaka Makutupola au unaongelea pia reli ambayo inajengwa hivi sasa ya kwenda Mwanza na Kigoma?? ... kwamba nazo zitakufa hata kabla ya kuanza baada ya miaka sita?
Hiyo ya mwanza haitaanza kazi leo, naongelea hiki kipande cha Dodoma kwanza
 
Haihitaji rocket science kujua kuwa huo mradi utakufa au kuchakaaa mpaka efficiency yake kupungua below 50 percent. Angalieni mradi wa mabasi ya mwendokasi. Trend ya uendeshaji wake inatosha kutoa utabiri juu ya SGR.
Sababu kubwa ya mbili zitaiangusha SGR
MOJA:KUKOSEKANA UTAMADUNI WA UKARABATI. _Yaaani tunasubiri vitu viharibike hadi vinashindwa kurekebishika au gharama inakuwa kubwa na tuna opt kwenye shortcuts.
MBILI_Wizi ,ten percent masilahi binafsi nauongozi /usimamizi mbovu. Haya ni magonjwa sugu kila sector. Mnayafahamu haya. Wanaosema mtoa mada ni mchawi hawajatumia ubongo wao vizuri kudadavua mwenendo wa miradi yetu.
Eti mkuu Kuna haja kuagua kujua haya yote?
Hizi si ndo kero za tangu uhuru!!!?
 
Reli ya Kaskazini iliyofufuliwa na Magufuli inafanya kazi?
Sasa shirika lishindwe reli na treni za maintenance ndogo waje wafanye SGR kwa ufanisi?

Serikali isindwe kuendesha mabasi ya mwendokasi, izidiwe na hata Benjamin Makundi wa BM ije iweze SGR. Serikali hii hii inayoshindwa Air Tanzania inakula hasara wakati FastJet kwa nauli ya laki Dar to Mwanza bado walikuwa wanapata faida mpaka wakafukuzwa.
Ukiwaambia haya uvccm watakuita we mchawi na sio mzalendo
 
Vitu vingi vilivyo anzishwa kwa mbwembwe na vilivyo tumia gharama kubwa kuvifanya viwe mara nyingi havina mwendo mrefu.

Inakuwa hivyo kwa vile kuanza vinaanzishwa kwa propaganda za kisiasa na kuviendesha vinaenda kisaasa na maslahi ya wana siasa kwa ujumla wake, hivyo hatuna matarajio marefu na huu mradi wa treni hata hio miaka sita ya mleta mada huwenda ikawa ni mingi mno!

Hata hivyo jana sio leo na kesho hailingani na leo, huwenda ikawa kinyume chake.
Waambie ukweli Hawa machawa hawaelewi chochote! Ni siasa za kipumbavu TU!
 
Binafsi naona kilichoandikwa sio chuki wala uchawi
Ni kama motisha kwa wahusika wa hiyo project kuhakikisha wana-prove wrong kilichoandikwa...kwasababu najua wapo humu,na uzi wata/wameshauona
Na Nina uhakika 99% hawawezi kuni prove wrong hili Nina ujasiri nalo
 
Kwa sababu uzoefu unaonyesha kwamba serikali haijawahi kuanzisha na kusimamia mradi wo wote ule na ukaendelea kwa mafanikio na tija. Na uzoefu, wanasema, ndiye mwalimu mzuri!

Mradi hata uwe mzuri namna gani serikali ikitia mguu tu na mradi ukaitwa mradi wa umma basi hesabu maumivu. Tazama mwendokasi. Mamilioni ya pesa yanayokusanywa pale kwa siku na mradi ulivyo. Itazame Air Tanzania. TANESCO...Na maviwanda mengi tu.

Kwanza wananzengo wataanza kuharibu vifaa kwa makusudi. Na hakuna mtengenezaji. Miezi 6 tu mabehewa yatakuwa choka mbaya mkangafu. Vyoo havitamaniki...Na hasara zitaanza kurundikana haijalishi kama ina mamilioni ya abiria...na mizigo!

Hata mimi sina matumaini nayo. Let them prove me wrong! Niko nimekaa paleeee!
Tuko paleee tunawasubiri watuite mbwa 🐕🐕 baada ya miaka 6

😂😂😂
 
unasema thabiti au kufa? ebu badilisha juu huko , miradi inaweza kusua sua haina maana imekufa, kilichokufa HAKIPO kabisaaaa
Kwanini isuesue??? Huko ndo kufa, kama kitu hakuna muendeleza uleule hakuwezi kuzingatia kama Kuna manufaa ni kama nguo chakavu unapoitumia kulimia unaitumia sawa lakini huwezi kusema Nina nguo ya kulimia
 
Mkuu, nchi zote zilizoendelea all means of transportation zinafanya kazi kwa ufanisi. Study shows ufanisi wa njia moja unavyoongezeka na njia zingine zinakua as well.

Kudhani reli itaua biashara ya malori is being short-sighted, realistically biashara ya malori itaongezeka zaidi. Wateja watakua na option na watu wengi wataitumia TZ maana usafiri utakua wa uhakika na ushindani wa nguvu.

Nchi kuendelea inahitaji reli bora, kilimo chenye tija na umeme wa kutosha na uhakika; the human capital goes without saying. That's it.
So, in regard to our context, our history and experience what you think it will happen? Mana hii nchi iko kwenye mikono ya watu wachache sana... kun muda italeta shida tu na huu mradi utabinfsishwa.

Hatari na kasoro/damage ya uendeshaj wa mrad huu unaitazamaje? Unajua hii nchi sio developed, asilimia kubwa ya watu ni wachov wa kufikiri. SGR kuna namna tu itaingia kwenye trap ili iwanufaishe wachache
 
Back
Top Bottom