Uchaguzi 2020 Kwa mtazamo wenu, mnadhani hizi hoja zitawabeba kwenye Sanduku la Kura?

Uchaguzi 2020 Kwa mtazamo wenu, mnadhani hizi hoja zitawabeba kwenye Sanduku la Kura?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Nasikitika na kushangaa sana ninaposikiliza hoja za wanasiasa wa upinzani. Nafikiri wanaona aibu kunyoosha mikono na kukubali tu kuwa CCM inafanya mazuri na kuwa wanalazimika kupinga tu ili kuondoa aibu ya kuonekana kuwa hawana mashiko mbele ya umma wa watanzania.

Wanasema Tanzania kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za bindamu na wanatamka wazi kuwa hakuna uhuru wa kufanya kazi na kujieleza. Hivi hili linaweza kuthibishwa vipi? Unaposema hakuna uhuru na haki za wananchi zimeminywa wananchi wangekuwa huru kufanya shughuli zao za kila siku? Au ni uhuru gani mnaoutaka. Kama ni uhuru wa kujieleza mbona tunaona wanasiasa wengi tu wanafanya mahojiano na vyombo vya habari! Tunaona wananchi wapo vijiweni wakijadili masuala mbalimbali.

Mnataka uhuru wa kukosoa serikali kwani mmezuiwa? Mnaambiwa kosoeni ila kwa lugha staha.Hili lipo wazi hata ibara ya 30(1) ya katiba ya JMT imetamka wazi, tusitumie uhuru na haki tulizopewa vibaya kiasi cha kuingilia haki na uhuru wa watu wengine. Kwa hiyo kusema mmezuia kukusoa ni hoja ambayo haina mashiko.

Mnasema wananchi walibomolewa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara. Na hili mnataka kulichukulia kuwa litawapa kura. Je waliobomolewa walikuwa kwenye hifadhi ya barabara au walikuwa nje? Tunaomba mtufafanulie juu ya hili, Sheria za nchi juu ya mwananchi anayekuwa amejenga ndani ya hifadhi ya barabara zinasemaje? Anatakiwa alipwe fidia au asilipwe? Kama kuna upanuzi wa barabara. Maana kila nchi inatawaliwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

Pia, mnazunguka na kuleta hoja eti CCM imejikita kwenye kuwekeza kwenye maendeleo ya vitu kuliko ya watu. Hii hoja haina mashiko kabisa,maana nini dhana nzima ya inclusive development? Hospital, vituo vya afya,barabara, na miradi yote mikubwa ni kwa ajili ya watu. Ni kwa manufa ya watanzania wote. Hii hoja ndio inawafanya wanachi wawadharau kabisa.

Maana kupinga ujenzi wa mradi kama JNHPP au SGR ni dhahiri kuwa hamna nia njema na wanachi. Kupinga kufufuliwa kwa meli kama Mv Victoria na Mv Butiama ni kujitia matope mbele ya wananchi. Maana sio maendeleo ya vitu bali ya watu. Na kwa mantiki hii wananchi mpaka sasa hawana mbadala wa chama cha kuiondoa CCM. Maana wapinzani hawana nia thabiti ya kuwatumikia wananchi.
 
Post za namna hii tukizisusia maoni zitakufilia mbali na hao waletaji wake watajiona hadhira imewapuuza..hawatarudia tena kuandika upuuzi
Sio upuuzi huu ndugu. Kama ni upuuzi Oktoba 28 utapata jibu.
 
Aibu sana naona kwako mleta mada.
Kuitetea ccm inahitaji roho ya paka.
Mgekuwa mnajiamini na hayo mnayojisifia kwayo,chaguzi ziwe huru na haki.Asubuhi saa nne mnaachia madaraka.
Mlioyafanya hata Rungwe angeweza fanya,kawazidi tu pale anapojiongeza kwa Ubwabwa.
#NI YEYE
 
Mlijua na agenda ya kuua upinzani sasa mmeamua kucheza kwaito kwenye majukwaa mkiomba kura.
 
Aibu sana naona kwako mleta mada.
Kuitetea ccm inahitaji roho ya paka.
Mgekuwa mnajiamini na hayo mnayojisifia kwayo,chaguzi ziwe huru na haki.Asubuhi saa nne mnaachia madaraka.
Mlioyafanya hata Rungwe angeweza fanya,kawazidi tu pale anapojiongeza kwa Ubwabwa.
#NI YEYE
Kuna maswali nimeuliza. Nafikili ungeli yajibu ingekuwa ni sawa. Mfano nipe jibu moja tu. Waliobomolewa kimara walikuwa kwenye hifadhi? Sheria inasemaje? Tanzania hakuna uhuru wa kufanya kazi? Uhuru wa kujieleza? Jikite kwenye mada.
 
Back
Top Bottom