Nakosoa mtindo uliotumika katika kura za maoni. Wagombea wote waliopitishwa ni wale waliotoa pesa ya kutosha kwa wajumbe wa majimbo. Bei za wajumbe zilianzia shilingi 30,000 hadi 100,000 kutegemea jimbo lenyewe. Wanaoshinda katika kura za maoni ndo wanategemewa kwa kiasi kikubwa kupitishwa kupeperusha bendera ya CCM lakini, naanza kuona ugumu wa kuungwa mkono hata na wanachama wa CCM.
Mimi ni mwanachama je, CCM inaniambia huyo aliyewahonga wajumbe wachache tumuunge mkono wakati mimi sikupata mgao huo wa pesa? Mtindo wa miaka iliyopita, wanachama wote tuliramba rushwa pale watia niya walipokuwa wakijipitisha kila kata na hatimaye kila mwana-CCM kupiga kura. Mtindo wa mwaka huu umewaruhusu wajumbe wa CCM ndani ya jimbo tu ndo waliogusana na watia niya.
Ni hakika kwamba sisi wana CCM hatutawaunga mkono wagombea ambao hatukufaidika na kupitishwa kwao. Chama kijiandae kulazimisha matokeo. Watu hawa hawauziki kwa wanachama, wanauzika kwa wajumbe wachache waliopewa chochote.