Haaaahaaaa, hapana kaka mimi siko ESCROW ni Mtanzania mwema sana, yes huo ni urembo tu siunajua kupenda hakuna mtu muhimu kwenye maisha kama mke na anafaa apendeze kila wakati. Amini au usiamini mimi ni mkulima tu wa mananasi, kilimo kinanipatia zaidi ya 100,000,000 kwa mwaka. Kama kwa mwaka naweza kuuza mananasi 350,000 piga hesabu kwa bei ya jumla ya chini kabisa ya nanasi moja likiwa shambani ni kiasi gani. Fanya utafiti nanasi moja shilingi ngapi kisha piga hesabu. Nchi hili ni kubwa mno ninyi mnang'angana na kutaka kuwa watumwa wa Wahindi na kuuza chupi barabari mpaka lini, mtaendelea tu kuona wenzenu matajiri kumbe uzembe wenu. Nakupa home work pale Kiwangwa Bagamoyo **** mtu anaitwa Mzee Mitigo hakwenda shule lakini analima tu, angalia pato lake la mwaka na vitegauchumi anavyowekeza kutokana na kilimo. Tunafanya kilimo full time job, karibu uje nikufundishe kilimo kwakuwa mali iko shambani bana.