Wadau poleni na majukumu. Nimekuwa nikisoma makala mbalimbali zinazoonesha maswali kwamba, ni nani hasa mjenzi wa majengo ya Piramidi ambayo yapo kwenye nchi ya Misri. Lakini pia baadhi ya nchi nyingine duniani. Nimesoma mahali hata Ethiopia, Uturuki na China (nilisoma mahali).
Kila mtu anaeleza kulingana na elimu yake na vyanzo vyake. Lakini mimi (huenda na wengine wapo), naamini Mapiramidi yalijengwa na watu waitwao WAANAKI ambao ni damu moja na WANEFILI.
Haya nimeyapata kutoka kwenye Kitabu cha Biblia. Ingawa Biblia haijasema kuhusu Piramidi lakini ishu ni Waanaki kujenga majengo marefu sana na wao wenyewe kuwa wengi, wakubwa na warefu sana.
Nimesoma Biblia kwa utulivu sana na kwa muda mrefu na kubaini mambo haya.
Nitaomba twende polepole tukiangalia neno kwa neno, mstari kwa mstari.
Kwanza kabisa, Biblia inaonesha kuwa, kabla ya kuwepo kwa Adamu na Eva walikuwepo hao watu wanaitwa WANEFILI waliotoka uzao wa WAANAKI. Hawa WAANAKI waliendelea kuishi duniani miaka na miaka wakaja kuangamizwa na Joshua.
Mwanzo: Mwanzo 6: 1-7.
4. Nao WANEFILI walikuwako duniani siku zile; tena baada ya hayo, wana wa Mungu (malaika) walipoingia kwa binti za binadamu, wakazaa nao wana; hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
HII PARAGRAFU INAPOANZA NA NENO 'nao' INAONESHA MBALI NA BINADAMU KUWEPO 'PIA'.
5. Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.
6. Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
7. Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.
BIBLIA INASEMA NI KWELI MUNGU AKAUA KILA KILICHO NA MWILI KWA UZAO WA BINADAMU KWA MAJI YA GHARIKA. KASORO NUHU TU NA FAMILIA YAKE.
USHAHIDI HUU HAPA;
Mwanzo 8: 15-19.
15. Mungu akamwambia Nuhu, akisema, 16. Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. 17. Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi. 18. Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye;
19. kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina.
LAKINI KWA MUJIBU WA BIBLIA, MBELE GHAFLA TU WANAONEKANA WALE WANEFILI TENA. USHAHIDI HUU HAPA;
Hesabu 13: 30-33.
30. Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.
31. Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.
32. Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33. Kisha, huko tuliwaona WANEFILI, wana wa ANAKI, waliotoka kwa hao WANAFELI; tukajiona nafsi zetu kuwa kama MAPANZI; nao ndivyo walivyotuona sisi.
HOJA: PANZI WOTE TUNAWAJUA WALIVYO. KWA JINSI TULIVYO BINADAMU, NI KIUMBE GANI KINAWEZA KUTUONA SISI KAMA PANZI? NDIVYO WALIVYOKUWA HAWA WANEFILI KIZAZI CHA WAANAKI.
JINSI WANEFILI WALIVYOUMBWA NA UZAO WAO WAANAKI. USHAHIDI HUU HAPA;
Kumbukumbu la torati 1: 25-30.
25. Wakatwaa baadhi ya matunda ya nchi ile mikononi mwao, wakatuletea huku chini, wakatuletea habari tena, wakasema, Nchi hii anayotupa Bwana, Mungu wetu, ni nchi njema.
26. Lakini hamkukubali kukwea huko, mlihalifu neno la Bwana, Mungu wenu;
27. mkanung'unika hemani mwenu, mkasema, Ni kwa sababu Bwana ametuchukia, ndipo akatutoa katika nchi ya Misri, apate kututia katika mikono ya Waamori, ili kutuangamiza.
28. Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni WENGI, ni WAREFU KULIKO SISI; MIJI YAO NI MIKUBWA, imejengewa KUTA HATA MBINGUNI; na zaidi ya hayo huko tumewaona WAANAKI.
29. Ndipo nikawaambieni, Msifanye hofu, wala msiwache.
30. Bwana, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu.
KUZIONA KUTA ZIMEFIKA MBINGUNI NI KAMA VILE LEO TUNAVYOYAANGALIA MAGOROPFA MAREFU KWA KWENDA JUU. TUNAYAONA YAMEPITA MAWINGU NDIVYO WANA WA ISRAELI WALIVYOONA MAJENGO NA KUTA ZA WAANAKI.
WALIVYOUMBIKA WAANAKI NA KIZAZI CHAO. USHAHIDI HUU HAPA;
Kumbukumbu la Torati 2: 9-11.
9. Bwana akaniambia, usiwasumbue Wamoabi, wala usishindane nao katika mapigano; kwa kuwa sitakupa katika nchi yake kuimiliki; kwa sababu Ari nimewapa wana wa Lutu kuimiliki.
10. Walioketi humo hapo kale ni Waemi, nao ni watu WAKUBWA, WENGI, WAREFU, mfano wa WAANAKI.
11. na hawa nao wadhaniwa kuwa MAJITU kama WAANAKI; lakini Wamoabi huwaita Waemi.
Kumbukumbu la Torati 9: 1-2
1. Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo MAKUBWA, na yenye NGUVU kukupita wewe, MIJI MIKUBWA iliyojengewa KUTA hata MBINGUNI.
2. WATU WAKUBWA, WAREFU, wana wa WAANAKI uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa ANAKI?
WAANAKI WALIVYOANGAMIZWA. USHAHIDI HUU HAPA;
Yoshua 11: 21-22.
21. Wakati huo Yoshua akaenda na kuwakatilia mbali hao WAANAKI watoke nchi ya vilima, kutoka Hebroni, na kutoka Debiri, na kutoka Anabu, na kutoka katika nchi yote ya vilima vilima ya Yuda, na kutoka katika nchi yote ya vilima vilima ya Israeli; Yoshua akawaangamiza kabisa na miji yao.
22. Hawakusalia WAANAKI hata mmoja katika nchi ya wana wa Israeli; isipokuwa katika Gaza, na katika Gathi, na katika Ashdodi walisalia.
Yoshua 14: 15.
15. Basi jina la Hebroni hapo kwanza uliitwa Kiriath-arba; huyo Arba alikuwa ni mtu mkubwa kupita wenziwe wote katika hao WAANAKI. Hiyo nchi nayo ikatulia, vita vikakoma.