#COVID19 Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, Tunapoteza watu kwa kiwango kikubwa kutokana na Corona

Inawezekana umepuuzwa kwa kuuliza mambo yaliyo wazi mno.
Sawa, naomba unitoe upuuzi huo kwaku kunionyesha chanzo cha takwimu za Zitto kilicho wazi. Natanguliza shukrani.
 
Guys Corona ipo na ina ua challenge tuliyonayo ni aina ya maisha tuliyo nayo mungu atatuvusha tu japo Tanzania haijatuathiri sana viongozi wasitumie mwanya wa kuongeza hofu sana
 

Kwamba?

"Hiyo ni death toll ya siku moja kwenye baadhi ya nchi zenye population kama yetu!"

Nchi gani hizo?

Nchi zingine kama sisi:





Bado unadhani ni sawa kwa sababu hujaguswa?

Kwani upumbavu utakuwa ni nini basi?
 
Sawa, naomba unitoe upuuzi huo kwaku kunionyesha chanzo cha takwimu za Zitto kilicho wazi. Natanguliza shukrani.

Kwenye mada (a) na (b) imeelezwa au unataka hadi mtu akusomee kwa sauti?

Ndiyo maana unapuuzwa.
 
Ukiwa na tb, cancer, kisukari, pressure etc ukipata corona huchomoki. Na wengi wanokufa ni kwa sababu ya matatizo uliyoyataja ila chanzo cha kifo ni corona kuingia mwilini. Nina ndugu wawili wamekufa kwa design hii wiki nya jana tu!. Huu ugonjwa upo tusiupuuze. Tatizo ninaliliona ni jinsi serikali ilivyo downplay huu ugonjwa mwaka jana na ikaacha kutoa takwimu hivyo watanzania hatujui idadi halisi ya ndugu zetu waliokufa kwa ugonjwa huu. Iliaminisha watu kuwa chanjo ni fake na ni njama za mabeberu kutumaliza. Sasa hivi hiyo hiyo serikali inakuja na msimamo mwingine kuwa chanjo ni salama na kuwa tusikilize wana sayansi wakati mwaka jana iliwadownplay sana wanasayansi. Ndugulile peke yake alisimama na sayansi na akaishia kutumbuliwa. Sasa hivi hili suala ni la mtu binafsi kuamua anataka kuishi au lah! Afanye nini, ni juu yake. Ila ugonjwa upo na unatisha. Actually haujawahi kuondoka ulikuwepo tu ila takwimu zilikuwa hazitolewi!!!
 
Corona anasingiziwa sana!
 

Ila unasimama vipi peke yako:

"Sasa hivi hili suala ni la mtu binafsi kuamua anataka kuishi au lah! Afanye nini, ni juu yake."

Wakati serikali haina habari:

1. Ikiendelea kuwakamua wananchi kwa kuwaongezea kodi na tozo mbalimbali ndani ya gonjwa hili.
2. Ikiendelea kuwakamua wananchi kwa kuwatelekezea mzigo wa matibabu wa gonjwa hili kila linapowasibu.
3. Ikiendelea kuufanyia siasa ugonjwa huu kwa kuendelea kuficha takwimu zake.
4. Ikiendelea kutokufanya jitihada za kutosha kuwanusuru watu na ugonjwa huu.


Yako mengi ambavyo kwa hakika pamoja na kila kitu, kwa mwenendo wa serikali hii kwa hakika hatutoboi.
 
Upo sahihi sana. Hali ni mbaya sana. Kila unakopita unaambiwa habari za misiba. Jana jirani yangu amefiwa na mlinzi wake ghafla kwa tatizo la upumuaji. Nimeenda kwa mtu ambaye nimeelekezwa ndiye ana bidhaa ninayoihitaji. Nafika, anafunga duka, anasema ndugu yake amefariki ghafla.
 
Corona anasingiziwa sana!

Ukitaka kujua kuwa hasingiziwi zingatia:

1. Tofauti ya takwimu za vifo 2019 na 2020.
2. Tambua jitihada za serikali kuficha takwimu za Corona Apr 2020.
3. Zingatia idadi ya misiba uliyoisikia wewe kuhusiana na Corona ndani ya mwezi mmoja.
4. Jiulize "nane nane" inafanyika lini?
5. Mbio za mwenge zimefika wapi?
6. Kumbuka tuko ushetu kwa mazishi bila kusahau:



Ukimaliza tafuta wa kwako wa kusingizia.
 
Uko sahihi
 
Mkuu mwenge umekimbizwa Mpwapwa wiki iliyopita
 

Hawana jina zaidi ya kuwaita kuwa ni wapumbavu waliojificha hawa:



kama ni watu na kama wanadhani inawasaidia kutokuonekana.
 
Hameni Huko wanakokufa kila siku !! Ila mimi nakokaa na home nilikozaliwa kila siku naongea nao hakuna hiyo misiba!!
Mtu analeta reference et angalia taarifa za vifo Facebook WTF
 
Kwenye mada (a) na (b) imeelezwa au unataka hadi mtu akusomee kwa sauti?

Ndiyo maana unapuuzwa.
Sawa: Nimerudia mara mbili kusoma hivyo vipengele kisha kufuatilia vyanzo vya habari anavyodai kutumia Zitto kupata takwimu hizo kabla ya kuuliza.

(a) unasema alitumia E-huduma. Nimeenda kwenye ukurasa wa E-huduma ambao upo kwenye mtandao wa RITA, sijapata takwimu hizo. Link hii hapa.

E-Huduma

(b) unasema serikali ni chanzo. Nimeenda kwenye mtandao wa serikali pia huko sikupata takwimu hizo. Link hii hapa


Sasa nielekeze vizuri hizo data zipo wapi ? Ni rahisi tu hivyo, Mkuu, ili ufanikiwe kunitoa upuuzi wangu.
 
Hawana jina zaidi ya kuwaita kuwa ni wapumbavu waliojificha hawa:

View attachment 1885942

kama ni watu na kama wanadhani inawasaidia kutokuonekana.

Hiyo misiba inatokea wapi? Kwahiyo waziri akifa na baba ake akafa ndio ina-justify kwamba watu wanakufa sana ?

Na vipi hapo kabla tz ilikuwa peponi watu walikuwa hawafi?
Acheni upumbavu .
 
Hameni Huko wanakokufa kila siku !! Ila mimi nakokaa na home nilikozaliwa kila siku naongea nao hakuna hiyo misiba!!
Mtu analeta reference et angalia taarifa za vifo Facebook WTF

Hata ushetu wanakoishi kuna Kuandikwa misiba hii 2 imeletwa tokea Dar.



Tofautisha mijini na kwenu Nguruka.
 
Guys Corona ipo na ina ua challenge tuliyonayo ni aina ya maisha tuliyo nayo mungu atatuvusha tu japo Tanzania haijatuathiri sana viongozi wasitumie mwanya wa kuongeza hofu sana

Kwa hakika hata huyu Mungu atamvusha:



na chui ajaye wala hatamwona.
 
Unaposema kuipata una maana gani ni kuumwa corona au kuwa na virusi tu vya corona? nauliza hivyo kwa sababu kuna tofauti kati ya kufa kwa corona na kufa ukiwa na corona hivyo kuwa corona postive haina maana ukifa ni covid tu. Na kuna utata sana kwenye kujua chanzo kilichosababisha kifo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…