#COVID19 Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, Tunapoteza watu kwa kiwango kikubwa kutokana na Corona

#COVID19 Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, Tunapoteza watu kwa kiwango kikubwa kutokana na Corona

Yaani ndio akili za wana lumumba ,ukiwaambia watu wanapukutika kwa corona wao wanajibu mbona wewe hujafa?

Inajulikana kuwa ujinga ni mzigo kama wa kuni tu nao hubebwa kichwani.

Hatubabaishi wala nini:

IMG_20210711_205649_038.jpg
 
Sasa huu ni upuuzi kukuza jambo kuliko uhalisia.
Corona ipo na inaua hasa. Ukweli ni kwamba Corona inavyouwa Tanzania haijafikia au kuzidi kama iliyofanya India.

Palipokuzwa wapi? Umesoma kilichoandikwa? Graph umeisoma? Au zile za kukurupuka tu?

No wonder takwimu walikuwa hawatoi.
 
Palipokuzwa wapi? Umesoma kilichoandikwa? Graph umeisoma? Au zile za kukurupuka tu?

No wonder takwimu walikuwa hawatoi.
Wewe weka ushabiki, chuki na siasa pembeni kisha tafuta takwimu halisi utauona ukweli.
 
Wewe weka ushabiki, chuki na siasa pembeni kisha tafuta takwimu halisi utauona ukweli.

Hapana ushabiki hapo wala nini.

India wastani wa wiki ni 502 sisi tunagonga 507.

Labda kama una maana 502 > 507.
 
Mwaka huu kwa kweli nimezika sana ndugu zangu wa karibu, ndugu wa damu, na kesho naenda kunzika Mama yangu mdogo, rafiki yangu wa dhati Tumaini Kakuyu Mlewa
Iringa nini maana huko napajua huwa haipiti siku bila msiba.
 
Wewe kama siyo kipofu, utakuwa mnafiki; kama mnafiki, utakuwa na ulemavu wa akili. Ni wapi ambako misiba haijaongezeka zaidi ya ilivyozoeleka?

Kesho, huku anazikwa Waziri wa ulinzi, jioni hii kuna misiba mingine mitatu. Wewe unaona hii ni kawaida. Na mwenyeji hapa anasema kuwa leo ni afadhali maana siku hizi, karibia kila siku ni 6 kwenda juu.
Hao watu ni rika gani au ni rika zote?
 
Wengine mpaka afe yeye ama mtu wake wa karibu ndio anaelewa.
Kuna tofauti kati ya kuelewa na kutumia hisia, watu wengi humu baada ya kufiwa na watu wao wa karibu basi huja humu na hutumia hisia yani wanahusisha hizo hisia zao za kufiwa na watu wao na kuzihusisha na corona. Juzi kati tu nimetoka kufiwa na ndugu yangu kabisa na ningetaka kutumia hisia basi sasa hivi ningekuwa napiga kelele za corona maana nisingeeleza huyo ndugu yangu alikuwa anasumbuliwa na nini na ilikuaje bali ningehusisha tu na corona basi kama wengine humu wanavyofanya.
 
Nmekuja hapa chuoni kuchkua cheti na nmekua hapa kwa wiki moja, nmeshuhudia vifo vya maprofesa watatu ndani ya wiki moja, na mmoja kafariki leo asubui. Anasema data za kupika asubir siku wakidondoka ndugu zake ndo ataamini. Ofkoz hali sio nzuri.
Watu wanatamani kukimbia mikataba yao waache kufnya kaz za kuhudumia public,
Mimi nafikiri hadi aone hospitali kuzidiwa wagonjwa, unajua suala la vifo tu pengine ni ngumu kuona maana mwengine atakwambia sijui Kilimanjaro watu wanakufa sana na mwengine atakwambia mtaani kwake ndio watu wanakufa sana ila hospitali zikijaa wagonjwa hapo kila mtu ataona na kuelewa kuwa sasa maambukizi yamepamba moto kuna hali isiyo ya kawaida.
 
Jambo la kheri kuwa sherehe za nane nane zimefutwa kimya kimya.

Juzi kati Mwenge wa Uhuru ulikuwa Morogoro nao kimya kimya.

View attachment 1885518

Mambo ya mbuni yametufikisha hapa.

View attachment 1885424

---- extracts tokea kwake Zitto Kabwe.

Kwamba tunapoteza watu si chini ya 2,000/mwezi kwa Corona. Hali hii si ya kufumbiwa macho.

Wanaokufa katika hali hizi zinazoweza kuzuilika ni watu kama wewe na miye.

Kwamba hajawajibika mtu hadi leo kwa hali hii, kwa hakika haikubaliki.


Nadhani wewe (kama alivyo Zitto) huyajui mapigo ya COVID-19. Ungekuwa unayajua usingeshangaa vifo 2,000 kwa mwezi kwenye nchi yenye population ya watu takribani 60 million. Hiyo ni death toll ya siku moja kwenye baadhi ya nchi zenye population kama yetu!
 
Back
Top Bottom