CPU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 3,858
- 687
- Thread starter
- #101
Tatizo lilikuwa uvimbe tu kwenye kizazi,nilikuwa napata maumivu wakati wote wa kukua kwa mtoto,sema sikuwa nakwenda kliniki kwa kuogopa kupimwa,nilipozidiwa na kuanza kutoka damu ndipo nilipoenda,wakasema ujauzito ulikuwa umeharibika muda tu na maumivu ni kwasababu ya uvimbe.baada ya kukatoa katoto nikakaa kama wiki tatu,kuongeza damu,wiki ya nne wakatoa huo uvimbe na kunisafisha.hawakuniambia kuwa sitazaa tena nami nina imani nitaweza,kaka CPU amefikiri hivyo kwa kuwa baadhi ya waliokuwa na tatizo kama langu hushauriwa kutoa kizazi kabisa au kupoteza ule uwezo wa kuzaa.
Afadhali umekuja dada, na uendelee kuwa na imani hiyo kwa msaada wa roho mtakatifu. Bila shaka unajiandaa ukapime afya hospital