Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bima ni mkombozi mkubwa, inatufanya tutafute huduma sahihi wakati wa uhitaji pasipo kujari gharama. Wekeza kwenye BIMA kuponguza gharama na kuwa na uhakika wa matibabu sahihi wakati wa uhitajiBima ya afya Tanzania haiwezekani.
Watu hawana pesa za kulipa kiasi halisi cha bima inabidi bei ipunguzwe na hapo huduma inapungua.
Magonjwa mengi na watu karibu wote ni wagonjwa.
Ufisadi wa kuongeza gharama zinazofanywa na mahospitali wakishirikiana na watumishi wa bima.
Mzee umeongea jamb jema!!!Bima ya Afya haitakagi Siasa!
Hiyo bima ilikwama Kwa wanaojielewa huko. Sembuse huku ambako mtu anajemga Petrol station kwenye Makazi ya watu na vibali anavyo? Ghafla anatokea mtoa vibali anasimamisha ujenziHabari wana Bodi,
Ninachokishuhudia katika mwenendo wa watendaji pamoja na hali ya sasa ya mfuko wa Bima yà Afya, inakatishà tamaa yà kwanini mfuko huu unawafanyia hivi wateja wake?
Kabla sijaendelea naomba niweke jambo moja sawa.. watumishi wa umma Tanzania tambueni kuwa ninyi sio Miungu watu ni watumishi wao mmpo hapo na hali mliyonayo inatokana na sisi kuwagharamikia ninyi. Hivyo basi haiingii akilini kuwaona waajiri wako" hamnazo".
Malengo ya kupitishwa kwa sheria ya Bima ya Afya kwa wote kwa hakika yanaweza yasifikiwe kutokana na taratibu na au watumishi wasiofaa wa Mfuko wa Bima ya Afya.
Mifano yangu itajikita katika Hospitali ya Bugando. Hapa kwenye jengo la Bima wahudumu wake nafikiri wasiokuwa na taaluma ya Afya, waliwataka ndugu warudi nyumbani kumleta mgonjwa ambaye yuko kwenye hali isiyoridhisha na kuhitaji usafiri wa tax ili wamuone kabla ya kumuona daktari ambaye kwa siku hiyo alikuwa anakwenda kuwasomea ndugu majibu ya vipimo alivyochukua.
Mfano mwingine unanihusu mimi. Mgonjwa wangu mwenye bima inayoitwa ya vifurushi alifanyiwa upasuaji hospitalini hapo. Kurudi kwa ajili ya klinik, kwa daktari aliyemfanyia upasuaji na kumpangia siku ya kurudi, tunaambiwa na wàsimamizi wa mfuko kuwa, haiwezekani mpaka muanzie hospitali ya chini iwapatie rufaa ya kwenda Bugando.
Mimi sio tabibu lakini jambo hili haliingii akilini. Siamini kwamba mgonjwa aliyepata matibabu hospitali kubwa anastahili kurudi nyuma ili apewe rufaa na hospitali ya chini kurudi hospitali kubwa.
Kimbembe ni kupata hiyo rufaa, haina tofauti na kuingia na kukutwa ukiwa na mnyama pori! Hospitali ya chini kwa hapa karibu ni Sekou Toure, hawa wako radhi wakuandikie uende Muhimbili lakini sio Bugando.
Mbilinge hizi na nyingine nyingi za watumishi na taratibu zisizofaa za bima ya Afya, zimenipelekea Juzi 23/11 kulipia gharama za matibabu licha ya kuwa mwanachama wa Timiza Afya.
Kwa msingi huu, uliojengwa na taratibu zisizofaa za mfuko wa Bima ya Afya, nina pata mashaka kama haiwezi kuwa kikwazo kwa Bima mpya.
Kwa sasa kuna mambo machache ya kufanya ili kuhakikisha taratibu hizi zina koma.
1. Katiba ya JMT inapiga marufuku vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote. Tunakusudia kuiomba mahakama kutoa tafsiri ya kitendo cha watumishi wa umma kuruhusiwa kutibiwa popote ilhali watanzania wengine ambao kimsingi wanachangia zaidi kuliko hao wa umma, wakizuiliwa.
2. Kuishauri hospitali ya Bugando kuwa Bima ya Afya ni muwezeshaji wa huduma hivyo hawezi na hana mamlaka ya kuqapangia taratibu za kutoa huduma.
3. Mashirika na taasisi zisizokuwa za kiserikali, msiangalie tu kuhamashisha watu wajiunge na mifuko hii, angalieni pia utendaji wake.
Ninyi Wananchi ni wajinga sana tena mnoo tangu lini ccm ikaanzisha jambo kwa ajili yenu !!? Ninyi maskini ??Habari wana Bodi,

Asilimia 90 ya wanaolipa Bima Binafsi ni wagonjwa,(rejea utaratibu wa Toto Afya ambapo watoto walikuwa wanaandikishwa wakiwa wagonjwa na ikafutwa) ndiyo maana imewekewa ukomo wa huduma,Sitaki kuwasagia kunguni. Wana haki ya kupata wanachopewa. Nalalamika ubaguzi kwenye huduma.
Nimesoma humu basic salary ya daktari anayeanza ni 1,480,000. Malipo yake kwa mwaka ni 888,000. Anaweza kubeba wazazi wake. Tujaaliye hana watoto. Yeye binafsi na wazazi wake mchango wao ni 296,000 kila mmoja.
Nalipa 984,000 kwa ajili yangu peke yangu.
Bado sijapata jibu lenye mantiki kwa ubaguzi huu. Hata hiyo asilimia 90 hakuna ushahidi.Asilimia 90 ya wanaolipa Bima Binafsi ni wagonjwa,(rejea utaratibu wa Toto Afya ambapo watoto walikuwa wanaandikishwa wakiwa wagonjwa na ikafutwa) ndiyo maana imewekewa ukomo wa huduma,
Lakini leo serikali ikiajiri watu elfu 8, wanaingia kwa lazima bima ya Afya.
Mkuu.Ninyi Wananchi ni wajinga sana tena mnoo tangu lini ccm ikaanzisha jambo kwa ajili yenu !!? Ninyi maskini ??
Bima ya Afya kwa wote imeanzishwa ili kuokoa mfuko wa NHIF sio ninyi maskini wa kutupwa msio na akili.
Bima ya Afya kwa wote ni kama KIKOKOTOO tu vipo ili kuokoa vifuko isife waendelee kupiga pesa zenu ninyi maskini mnaokera.
Watu hawakurupuki data zinaongea na facts, Utilization ya huduma inaonyesha.Bado sijapata jibu lenye mantiki kwa ubaguzi huu. Hata hiyo asilimia 90 hakuna ushahidi.
Nalipa 984,000 kwa mwaka kwa ajili yangu peke yangu. Sioni sababu ya kupata huduma pungufu nikilinganishwa na anaelipa 150,000. Nakwenda hospitali mara mbili au tatu kwa mwaka. Sifanyiwi dialysis.Watu hawakurupuki data zinaongea na facts, Utilization ya huduma inaonyesha.
Ongea kwa takwimu,
Haya Tanzania ina watoto wangapi? Walioandikishwa NHIF walikuwa wangapi, walichangia kiasi gani na kutumia kiasi gani? Come on, hauko informed na huna taarifa halafu unataka jibu lenye mantiki,
Analysis zinafanyika na zinatoa taarifa, unafikiri waziri anaweza kutoka mbele ya vyombo akalitangazia taifa anafuta kitu bila kuwa na taarifa kamili?
Kwa hiyo kusema kwamba nyie mnachangia kuliko watumishi wa umma siyo kweli
Mimi nakatwa 120,000/- kila mwezi na ni mimi na mke wangu, hapo vipi?Nililipia 900,000 kwa watu wawili tu(mama na mtoto) kuna mtumishi wa umma wa 2m analipia laki 9 bima kwa watu wawili?
Siyo kweli hata mm nilienda kutibiwa hospitali fulani hizi kwa kweli maswali niliyoulizwa mapokezi yalikuwa ya kijinga sana.naulizwa wewe ni mchangiaji au benefitiary wakati mfumo unaoonyesha kila kituBima ya Afya haitakagi Siasa!
Hayo maswali uliyoulizwa Ndio Siasa zenyeweSiyo kweli hata mm nilienda kutibiwa hospitali fulani hizi kwa kweli maswali niliyoulizwa mapokezi yalikuwa ya kijinga sana.naulizwa wewe ni mchangiaji au benefitiary wakati mfumo unaoonyesha kila kitu
Hiyo ni 1,440,000 kwa mwaka. Na utakuwa na basic salary ya 2,000,000. Si waajiriwa wengi wenye mishahara kama wako. Na ukiwa na wategemezi wanne pesa ni hiyo hiyo. Wewe una haki ya kupata huduma kamili kama upatavyo. Utata upo kwa anayelipa kama wewe au zaidi lakini anapewa huduma pungufu.Mimi nakatwa 120,000/- kila mwezi na ni mimi na mke wangu, hapo vipi?