Kwa mwendo huu, Bima ya Afya kwa wote itakwama

Bima ni mkombozi mkubwa, inatufanya tutafute huduma sahihi wakati wa uhitaji pasipo kujari gharama. Wekeza kwenye BIMA kuponguza gharama na kuwa na uhakika wa matibabu sahihi wakati wa uhitaji
 
Hiyo bima ilikwama Kwa wanaojielewa huko. Sembuse huku ambako mtu anajemga Petrol station kwenye Makazi ya watu na vibali anavyo? Ghafla anatokea mtoa vibali anasimamisha ujenzi
 
Ninyi Wananchi ni wajinga sana tena mnoo tangu lini ccm ikaanzisha jambo kwa ajili yenu !!? Ninyi maskini ??

Bima ya Afya kwa wote imeanzishwa ili kuokoa mfuko wa NHIF sio ninyi maskini wa kutupwa msio na akili.

Bima ya Afya kwa wote ni kama KIKOKOTOO tu vipo ili kuokoa vifuko isife waendelee kupiga pesa zenu ninyi maskini mnaokera.
 
Asilimia 90 ya wanaolipa Bima Binafsi ni wagonjwa,(rejea utaratibu wa Toto Afya ambapo watoto walikuwa wanaandikishwa wakiwa wagonjwa na ikafutwa) ndiyo maana imewekewa ukomo wa huduma,
Lakini leo serikali ikiajiri watu elfu 8, wanaingia kwa lazima bima ya Afya.
 
Bado sijapata jibu lenye mantiki kwa ubaguzi huu. Hata hiyo asilimia 90 hakuna ushahidi.
 
Mkuu.
Inawezekana una hoja. Lakini sina uhakika kama kulikuwa na ulazima wa kutumia lugha kama hiyo.
 
Bado sijapata jibu lenye mantiki kwa ubaguzi huu. Hata hiyo asilimia 90 hakuna ushahidi.
Watu hawakurupuki data zinaongea na facts, Utilization ya huduma inaonyesha.
Ongea kwa takwimu,
Haya Tanzania ina watoto wangapi? Walioandikishwa NHIF walikuwa wangapi, walichangia kiasi gani na kutumia kiasi gani? Come on, hauko informed na huna taarifa halafu unataka jibu lenye mantiki,
Analysis zinafanyika na zinatoa taarifa, unafikiri waziri anaweza kutoka mbele ya vyombo akalitangazia taifa anafuta kitu bila kuwa na taarifa kamili?
 
Nalipa 984,000 kwa mwaka kwa ajili yangu peke yangu. Sioni sababu ya kupata huduma pungufu nikilinganishwa na anaelipa 150,000. Nakwenda hospitali mara mbili au tatu kwa mwaka. Sifanyiwi dialysis.
 
Bima ya Afya haitakagi Siasa!
Siyo kweli hata mm nilienda kutibiwa hospitali fulani hizi kwa kweli maswali niliyoulizwa mapokezi yalikuwa ya kijinga sana.naulizwa wewe ni mchangiaji au benefitiary wakati mfumo unaoonyesha kila kitu
 
Siyo kweli hata mm nilienda kutibiwa hospitali fulani hizi kwa kweli maswali niliyoulizwa mapokezi yalikuwa ya kijinga sana.naulizwa wewe ni mchangiaji au benefitiary wakati mfumo unaoonyesha kila kitu
Hayo maswali uliyoulizwa Ndio Siasa zenyewe

Sasa unakataa nini?
 
Mimi nakatwa 120,000/- kila mwezi na ni mimi na mke wangu, hapo vipi?
Hiyo ni 1,440,000 kwa mwaka. Na utakuwa na basic salary ya 2,000,000. Si waajiriwa wengi wenye mishahara kama wako. Na ukiwa na wategemezi wanne pesa ni hiyo hiyo. Wewe una haki ya kupata huduma kamili kama upatavyo. Utata upo kwa anayelipa kama wewe au zaidi lakini anapewa huduma pungufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…