Kwa mwenye uelewa mzuri na mambo ya NECTA naomba mnisaidie nahisi nimepigwa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Jamani naombeni msaada wenu mimi nilipotelewa na cheti cha form four mwaka 2001, tangia hapo nimekuwa nikitumia results sleep na lose report Kila mahali panapotakiwa vyeti.

Ila mwezi huu kulifanyika uhakiki wamevikataa hivyo vielelezo na kunitaka necta au notangaze gazetini.

Nilienda necta wakanipatia form inayonitaka niwe na lose report index number tangazo gazetini picha jina na shule na mwaka wa kuhitimu alafu wameweka tovuti ya nacte pale ili niombe online.

Nimekamilisha Kila kitu hapo juu ila baada kuletewa hiyo form nikaijaza hadi kufikia kipengele cha control number nikaletewa baada ya kulipia ili niendelee system inaniambia haijapokea malipo yoyote.

Napiga huduma Kwa wateja hawapokei sasa naamini humu tuna watu wenye fani tofauti yaweza kuwa hata necta wenyewe wamo naombeni msaada wenu.

Sijui nichukue hatua gani maana naona ni kama hela yangu itapotea.
 
Mambo mengi ya selikali hizi zetu ni upumbavu mtupu!

Yani hawana data kamili hadi uanze kwenda kujitangaza gazetini?
 
Nadhani ni utaratibu wa kiserikali hayo yote mimi nimekubali lakini hii ya kunikata hela alafu naambiwa sijalipia ndio imenivuruga kama kuna mtu anajua natumia njia gani aniambie.
 
Nenda ofisi kwao direct utasaidiwa mkuu ukiwa umebeba vielelezo vyote.
 
Ukishalipa si unabakiwa na detail zinazoonesha umelipa? Kama ulilipa kwa njia ya simu kwa mpesa au airtel money. Nenda Vodashop au Airtel shop wakakuprintie kisha nenda Ofisi za Necta.
Nadhani ni utaratibu wa kiserikali hayo yote mimi nimekubali lakini hii ya kunikata hela alafu naambiwa sijalipia ndio imenivuruga kama kuna mtu anajua natumia njia gani aniambie.
 
Nadhani ni utaratibu wa kiserikali hayo yote mimi nimekubali lakini hii ya kunikata hela alafu naambiwa sijalipia ndio imenivuruga kama kuna mtu anajua natumia njia gani aniambie.
Uko sure kwamba umelipia kwa control number sahihi bila kukosea?
 
Ukishalipa si unabakiwa na detail zinazoonesha umelipa? Kama ulilipa kwa njia ya simu kwa mpesa au airtel money. Nenda Vodashop au Airtel shop wakakuprintie kisha nenda Ofisi za Necta.
Nili
Uko sure kwamba umelipia kwa control number sahihi bila kukosea?
Sahihi kabisa mkuu ni crdb na baada ya kulipia meseji ilikuja Kwa simu yangu ikiniambia hela imepokelewa necta
 
Inabidi uende CRDB wakatoe copy inayoonyesha umelipa na nenda kwenye mtandao husika wa hiyo simu watoe copy kisha nenda kwenye ofisi za Necta.

Back
Top Bottom