JEJUTz
Member
- Aug 22, 2024
- 75
- 197
Hey wanajamvi heri ya msimu huu wa sikukuu na tukiwa tunaelekea kumaliza mwaka, naamini pilika zinawaendea vizuri kabisa.
Kwa sisi tunaopata nafasi ya kuzunguka sehemu tofauti tofauti ndani ya nchi hii,naweza kusema Watanzani angalau sasa tumekuwa wastaarabu.
Zamani ulikuwa ukiingia maeneo ya stand,sokoni na huko kwenye mikusanyiko ya watu utakutana na mizozo,fujo, matusi hali iliyopelekea watu kupigana na kuumizana vibaya.
Siku hizi ni nadra kuona watu wakipigana ingawa purukushani za hapa na pale zipo ingawa si kama zaman.Zamani watu walikuwa wababe na walipenda fujo hasa!
Tangu mwaka huu uanze takriban mikoa kumi na tatu ambayo nimezunguka sijashuhudia kadhia, mtafuruku wala fujo ya aina yoyote .
Kwa hili linatosha kuthibitisha kuwa jamii ya Kitanzani kwa kiasi fulani imestaarabika.
Ms.JJ.....Tchao