Hili tatizo ni kubwa kuliko linavyo jidhihirisha sasa.
Tatizo hili lianza tangu utawala wa mwalimu.
Mwl alijitahidi kushughulikia lakini lilijichipua. Kutumbuliwa kwa Jumbe ni mfano halisi. Lakini enzi hizo wakati ni mshiriki humu JF wa kusoma nyuzi za wengine na si member nilisoma mahali Sokoine eti alichapishaga kadi zake. Lakini Mwl yasemekana alinusurika kupinduliwa Mara kadhaa. Mimi naijua ya 1984, angalau ilikuwa wazi kiasi.
Tatizo lenyewe ni hili mtu/kikundi cha watu kinakuwa na masilahi yake, yaliyo jazwa na tamaa za kujinufaisha binafsi, wao, marafiki na jamaa zao si wananchi wote/taifa. Mbinu inayofanywa ni kuandaa mtandao ambao si rasimi hauko ndani ya chama kiundeshaji wake, lakini nje ya chama. Mtandao huu unawahusisha watu mbalimbali, kama kwa baadhi ya wafanyabiashara na watumishi wa serikali na mashirika wasio waaminifu. Kwenye chama ndio wanatumia wakati wa uchaguzi kama sasa kuweka mamluki wao kwa ajili ya kuandaa kuunda serikali ijayo ie awamu ya sita. Wafanyabiashara wanaahidiwa mambo yakifanikiwa mtandao ukishika serikali basi watapendelewa kwenye shughuli zao za kibiashara, hivyo wanatakiwa wawe wafadhili wa fedha wa kutekeleza mipango ya wanamtandao, kumbuka baadhi ya wanaotakiwa na mtandao hununuliwa kwa vipande vya fedha wakionekana ni wagumu kutoa ushirikiano.
Mwl alijaribu sana kupambana na hili tatizo, mfano halisi ni uchaguzi 1995. Mwl aliamua kama kawaida yake kuvaa uso usio na soni ila wakijasiri kwa maana halisi ya ujasiri. Mkapa akapata Urais na Mwl akaamini kuwa jamaa hata muangusha mengine ni historia jiongeze.... Ndio hii kauli mbiu ya kura hazikutosha. Lakini Mwl aliependa nchi kwa dhati na uzuri wenyewe wawili hawa walikuwa Marais. Kama ukweli huna hiyana ndani yako utajuwa who was the best president kati yao.
Watumishi wa umma wasio waaminifu wanaahidiwa kupandisha vyeo, si vyeo tu ila vyeo kwenye nafasi nyeti. Mfano Mkurugezi nssf au tass. Wako walio ahidiwa hivyo na wanajulikana. Wengine wakaambulia patu, yuko nguli mmoja wa kalamu na aliitumua vizuri kalamu yake kuwa uzia Watanzania mbuzi kwenye gunia yeye amebakia kumnunuia kila ajaye. Mtumishi akisha ahidiwa hivyo yeye kazi yake ni kuhujumu, kwa kuchelewesha mambo ofisni, kukatisha tamaa wenzake,kutafuta siri zitakazo saidia mtandao na kumhujumu kiongozi mkuu na wale wanaonekana ni wazuri na mahiri katika kumsaidia kazi. Ni rahisishe kwa kusema hivi wanamtandao wanaunda mfumo nje ya mfumo rasmi. Kazi ya huu mfumo ni kuhujumu mfumo rasmi kwanza usiwe na nguvu na lakini usiimarike. Kazi nyingine ni kumuandalia mazingira mtu wao kuwa Rais.
Wanamtandao hawa wakishafanya hivyo ndani ya nchi kama haitoshi hutafuta washirika nje ya nchi. Wanawapataje hawa? Nje ya nchi wako wenye masilahi ndani ya Tanzania. Masilahi haya mengi ni wingi wa raslimali lakini yako ya kisiasa na ya kijamii, mfano hai na halisi ni ushoga na yule mfalme aliyepinduliwa Zanzibar ana tamani arudi kwa mlango wa nyuma. Hawa nao wanapewa abadi zao stahiki kutokana na matamanio yao.
Pia kwa hili la nje ya nchi wanatumia propaganda zinazoichafua serikali iliopo madarakani kwa kutumia walewale wafanyakazi wasio waaminifu ambao wamewarecruit katika mtandao. Hili liko wazi mwenye akili atakuwa na mfano ya hivi karibu na inayo endelea.
Nitoe ushauri kwa matokeo haya ya kura za maoni CCM bado wana muda hawajachelewa, watume watu waaminifu kwenye majimbo yeye ukakasi wafanye kautafiti kwa random sampling ya maoni ya wapiga kura wananchi wa kawaida wakashangazwe na ukweli halisi. Na amini Mkt taifa na team yake ya uongozi wa juu ni watu makini na very serious hawatalipuuza hili.
Niishie hapo tusubiririe wachangiaji wengine.