Kwa namna hii kuna haja ya kuwa na marafiki kweli?

Kwa namna hii kuna haja ya kuwa na marafiki kweli?

ni kweli ving'ang'anizi wapo ila kama hupendi mabishano na ugomvi we mpe tena kiasi tu kidogo kwa kumsaidia na si kumkopesha zaidi ya hapo labda kama upo tayari kwa shari kipindi atakapoanza chenga.
No!! wee! mkopeshe akukimbie vizuri!!...ukimpa atakuwa anakuja mara kwa mara kukutembelea na vistory viiingi visivyoisha!
 
Bro unatoa pesa kirahisi mno,pesa ya biashara unaichezea mno
 
Soon atakushika makalio, endelea kumuendekeza hivyo hivyo.
Sio hata kumuendekeza, ila najiuliza anapataje ujasiri wa kurudi kwangu kuniomba pesa ilhali kuna nyingine namdai...
Nimesoma msg yake nikacheka tu na kumpotezea maana hata kumjibu sijajua namjibu nini yaani
 
Mm wale watu ambao najua ni watu wa vizinga akipiga/akitext me naanza kujilalamisha tu hali mbaya yaan huwa hawawezi kunipiga vizinga tena,na sasa hv nmekuwa mkali sana mtu akisema ana shida ya pesa namwambia sina ila bank wanakopesha kwa mashart mafuu sana[emoji39] naanza kumpa maelezo jinsi ya kukopa hzo pesa [emoji1787] maelezo mareefu mpaka anagwaya mwenyewe!
 
Sio hata kumuendekeza, ila najiuliza anapataje ujasiri wa kurudi kwangu kuniomba pesa ilhali kuna nyingine namdai...
Nimesoma msg yake nikacheka tu na kumpotezea maana hata kumjibu sijajua namjibu nini yaani
Mbwa ukimuendekeza atakufuata Hadi msikitini.
 
Hahaaaaa, mkuu kwa sababu ya jina la JF MTU ndo anifanyie makusudi yaani
Mkuu mimi ni.mtu na nusu, nikikukopesha pesa yangu, na ukazingua kuileta hata kwa siku 1, hizo kelele zake hutokaa unisahau

kwa kifupi, nafanya biashara ya kukopesha pesa, napata faida ya laki moja kwa wiki.

kama sio kuwa na roho ya Hitler, ningekuwa natapeliwa kama wewe.

Nilianza na 50,000 tu na sasa pesa imefika 750,000.

Nakopesha kwa wiki 1 moja, ukizidisha lazima mwenyekiti, balozi, majirani wajue labda utoe riba uendelee na mkopo😎
 
Bro usimkopeshe tena mtu hadi roho wa mungu akushukie akupe maelekezo,binafsi nimepoteza baadhi ya Ndugu na marafiki, watu wanakopa wanaingia mitini, wengine wanatengeneza mazingira ya kutaka waliwe... Shida tupu.
 
Mkuu mimi ni.mtu na nusu, nikikukopesha pesa yangu, na ukazingua kuileta hata kwa siku 1, hizo kelele zake hutokaa unisahau

kwa kifupi, nafanya biashara ya kukopesha pesa, napata faida ya laki moja kwa wiki.

kama sio kuwa na roho ya Hitler, ningekuwa natapeliwa kama wewe.

Nilianza na 50,000 tu na sasa pesa imefika 750,000.

Nakopesha kwa wiki 1 moja, ukizidisha lazima mwenyekiti, balozi, majirani wajue labda utoe riba uendelee na mkopo😎
Kwa kitaalamu inaitwa " kuwajazia nzi"
 
Mkuu biashara ya miamala ya kifedha si ya siri, anaona unavyobadilishana pesa na wateja, kwa hiyo kwenye mazingira ya dharura sana na kwa kudhani kuwa wataona umuhimu wa kutokuangusha biashara unavaa ubinadamu na kutoa pesa, lakini kumbe wao fikra zao zipo tofauti kabisa na tatizo linaanzia hapo
Wakija tena uwe unawaelekeza ofisi ya mikopo wanayotoa mikopo ya dharura, ninaweza kukupa no za kampuni mbili wanatoa mikopo ya dharura kama hizi riba ni 10% kwa mwezi, tuone kama hawatolipa.
 
Wakija tena uwe unawaelekeza ofisi ya mikopo wanayotoa mikopo ya dharura, ninaweza kukupa no za kampuni mbili wanatoa mikopo ya dharura kama hizi riba ni 10% kwa mwezi, tuone kama hawatolipa.
Very good idea, naomba nipe namba zao aisee, MTU akihitaji kukopa tu nampa namba na kumwambia mimi pia nimekopa hapo juzi tu...hahahaaa
 
Na nisipobeba TV, fridge na vitanda vya watu term hii sijui, maana sio kwa upuuzi huu, watu wanafanya maskhara sana na pesa
 
Back
Top Bottom