Kwa namna viongozi wa CCM walivyonuna baada ya hotuba tusubiri mkwamo

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Jana hakuna kiongozi yeyote wa CCM aliyempongeza Mhe. Rais kwa Hotuba nzuri, hata akina Kigwangala wanaokesha mitandaoni walikaa kimya. Watu waliopongeza ni wapinzani na wanaharakati pamoja na wananchi wa kawaida.

Siku zote ccm si chama kilichopo kwa ajili ya wananchi ni chama kwa ajili yakuongoza. Kauli na hotuba ya Mhe. Rais ya jana ililenga kutengeneza misingi ya Taifa lakini ikimomonyoa misingi ya chama. Matokeo yake tutayaona, watashauriana na soon watakuja na mkakati ambao maumivu ya wananchi yatakuwa makubwa zaidi .

Tanzania tunaporomoka kwa kasi, tukitaka kusimama tunayumbishwa na madreva waliovaa nafsi mbili. Tutatokaje hapa?
 
Chadema wamepora kazi ya MATAGA acha wapambane kumsifia mwana ccm Samia.
 
Safari hii watakwama wao sisi wanyonge tutasonga mbele lasivyo wamfuate mwenda zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…