Kwa namna ya uchezaji na midundo inayovutia, hizi ni ngoma za kikabila zilizonivutia zaidi

Kwa namna ya uchezaji na midundo inayovutia, hizi ni ngoma za kikabila zilizonivutia zaidi

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
1. WAHAYA - Ngoma zao nazielewa sana vile wanavyo tumia miguu kusigina na kutumia viuno na mikono, ni ngoma inayochezesha mwili mzima.

2. WAZARAMO - Napenda zaidi vyombo vya wapiga ngoma, ni vibe la hatari ila kucheza ngoma hakuna mpangilio.

3. WASAFWA - Hawa ni kabila lipo Mbeya, Ngoma zao nazipenda wanavyovaa vikengele miguuni , kama sikosei ngoma inaitwa mbeta

Ngoma ambazo sijawahi kuzielewa

Wakurya - hawa wanatikisa vichwa mwanzo mwisho, kama sio mzoefu unapata kizunguzungu, wananivutia mchezo wa mieleka ila sio ngoma.

Wamasai - Ni kuruka mwanzo mwisho

Wahehe - Ni wanadua kwa miguu pekee, kukanyaga sakafu hadi inatikisika
 
Back
Top Bottom