Kwa ndugu au wanaomfahamu Francis Johnpili, mwenyeji wa Mlandizi

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
1,598
Reaction score
2,905
WanaJF, salaam kwenu.

Mtajwa hapo juu kijana wa kiume mwenye umri (kwa kukadiria) wa miaka kati ya 19 hadi 24 ameonekana.

Kijana huyo ni kama ana upungufu wa akili lakini ukimchunguza vizuri ni kama aliyepoteza kumbukumbu tu.

Anadai kwamba yeye ni mwenyeji wa "Mlandizi bondeni" na baba yake anaitwa Johnpili na ni mwenyekiti wa Mlandizi bondeni. Dada yake anadai anaitwa "Vigi"

Amevaa suruali ya jeans iliyochanika mguu wa kulia kwanzia chini hadi juu karibu na kalio na t-shirt ya buluu bahari.

Anaulizia sehemu mbili;
1. DAWASA
2. JESHINI

Alionekana tangu jana na watu wanaonekana kutojali kabisa. Leo katika pita pita zangu nikamkuta akiwa amelala njiani ameishiwa nguvu nadhani ni njaa, nilipatwa na huruma kuu nimempatia chakula na maji.
Kwa wanaomfahamu wakuu tafadhali yupo huku.

Location:
Ni huku lilipo shamba la Mkulazi 1 (tarafa ya Ngerengere, kata Mkulazi, kijiji Usungura).

Asanteni.
 
Binafsi simfahamu lakini nitumie nafasi hii kukupongeza kwa moyo wa ukarimu mungu akuongoze kwakila jambo na mwisho muweze kuwapata ndugu zake pia ukiweka mawasiliano yako ingependeza zaidi ili wenye kumfahamu waweze kukupigia.
 
Shukran mkuu, ubarikiwe pia! Kuhusu mawasiliano si vema kuyaweka public.

PM kupo wazi kwa wanaomfahamu nawakaribisha.
 
mstahi kijana wa watu hata kwa kumpeleka kituo cha polisi kilicho karibu yako

ngerengere huko kuelekea Diguzi kuna uchawi sana.. fulu kuchunana ngozi..
Kutoka hapa nilipo hadi Ngerengere ni mbali mno na ukizingatia kuwa hiki ni kijiji cha mwisho kabisa katka tarafa hii hvyo ni porini mno.

Kuna kisa nakisikia pia hapa Kijijini kuwa kuna mtu mwenye hali hii alifika hapa kijijini alikuja akaranda randa bila kupata msaada mwishowe akafariki (ilikuwa mwaka jana..) pamoja na hayo nitampeleka kwenye uongozi wa Kijiji mkuu.
 
Kutoka hapa nilipo hadi Ngerengere ni mbali mno na ukizingatia kuwa hiki ni kijiji cha mwisho kabisa katka tarafa hii hvyo ni porini mno.

Kuna kisa nakisikia pia hapa Kijijini kuwa kuna mtu mwenye hali hii alifika hapa kijijini alikuja akaranda randa bila kupata msaada mwishowe akafariki.. pamoja na hayo nitampeleka kwenye uongozi wa Kijiji mkuu.
hao huwa wanafanyiwa michezo na ndugu zao ili wakafie mbele.

mtu kama huyo anapakizwa gari zinazoenda mbali sana maeneo ya vijijini huko kabisa. akifika anakosa msaada so anahangaika na kufia huko

Kuna mdada mmoja aliwahi kufanyiwa hivyo, kapandishiwa gari mbezi mwisho kwenda diguzi ndani ndani bila msaada, hakuweza kurudi dar huku ana mtoto

life is not fair
 
Inasikitisha sana mkuu!
 
Aisee,nimeumia sana walikufa yeye na mtoto mkuu

kwa kweli alifanikiwa kupanda gari bila kulipa nauli kimaficho, ila alipofika Ngerengere alishushwa kwa nguvu na kondakta.
Yule dada alikuwa kama ana upungufu flani katika mfumo wa akili.
Ifikie hatua sasa serikali iwe inawachukua kwa nguvu hawa watoto wanaolelewa na wamama vichaa
 
Kabisa,kuna kichaa mmoja yuko na watoto wake 2,huwa najiuliza serikali haioni kuwa hapa panahitajika msaaada??
kwa kweli alifanikiwa kupanda gari bila kulipa nauli kimaficho, ila alipofika Ngerengere alishushwa kwa nguvu na kondakta.
Yule dada alikuwa kama ana upungufu flani katika mfumo wa akili.
Ifikie hatua sasa serikali iwe inawachukua kwa nguvu hawa watoto wanaolelewa na wamama vichaa
 
WanaJF, salaam kwenu.

Mtajwa hapo juu kijana wa kiume mwenye umri (kwa kukadiria) wa miaka kati ya 19 hadi 24 ameonekana.

Kijana huyo ni kama ana upungufu wa akili lakini ukimchunguza vizuri ni kama aliyepoteza kumbukumbu tu.

Anadai kwamba yeye ni mwenyeji wa "Mlandizi bondeni" na baba yake anaitwa Johnpili na ni mwenyekiti wa Mlandizi bondeni. Dada yake anadai anaitwa "Vigi"

Amevaa suruali ya jeans iliyochanika mguu wa kulia kwanzia chini hadi juu karibu na kalio na t-shirt ya buluu bahari.

Anaulizia sehemu mbili;
1. DAWASA
2. JESHINI

Alionekana tangu jana na watu wanaonekana kutojali kabisa. Leo katika pita pita zangu nikamkuta akiwa amelala njiani ameishiwa nguvu nadhani ni njaa, nilipatwa na huruma kuu nimempatia chakula na maji.
Kwa wanaomfahamu wakuu tafadhali yupo huku.

Location:
Ni huku lilipo shamba la Mkulazi 1 (tarafa ya Ngerengere, kata Mkulazi, kijiji Usungura).

Asanteni.
Hello!
Mimi ninamfahamu nu kijana wa Babu yangu John Pilli...tafadhari tunamtafuta na jana tuliona tangazo na Babu yuko njiani kuja uko hii leo na jana nilijaribu kuwatafuta kupitia sicial media zenu tafadhari namba ya Babu yangu ni hii 0754779867 na Yangu ni 0713753469
 
Hello! nawashukuru sana kwa msaada wenu na upendo wa dhati,Mungu atawalipa pale mlipoonesha upendo na ushirikiano wa dhati kwetu,hivyo sisi kama Familia tumerudi kushukuru maana tumefanikiwa kumpata kijana wetu akiwa salama kabisa.Shukurani nyingi kwa mtoa habari hii na Mungu amfanikishe sana sana.
 
WanaJF, salaam kwenu.

Mtajwa hapo juu kijana wa kiume mwenye umri (kwa kukadiria) wa miaka kati ya 19 hadi 24 ameonekana.

Kijana huyo ni kama ana upungufu wa akili lakini ukimchunguza vizuri ni kama aliyepoteza kumbukumbu tu.

Anadai kwamba yeye ni mwenyeji wa "Mlandizi bondeni" na baba yake anaitwa Johnpili na ni mwenyekiti wa Mlandizi bondeni. Dada yake anadai anaitwa "Vigi"

Amevaa suruali ya jeans iliyochanika mguu wa kulia kwanzia chini hadi juu karibu na kalio na t-shirt ya buluu bahari.

Anaulizia sehemu mbili;
1. DAWASA
2. JESHINI

Alionekana tangu jana na watu wanaonekana kutojali kabisa. Leo katika pita pita zangu nikamkuta akiwa amelala njiani ameishiwa nguvu nadhani ni njaa, nilipatwa na huruma kuu nimempatia chakula na maji.
Kwa wanaomfahamu wakuu tafadhali yupo huku.

Location:
Ni huku lilipo shamba la Mkulazi 1 (tarafa ya Ngerengere, kata Mkulazi, kijiji Usungura).

Asanteni.
Hello! nawashukuru sana kwa msaada wenu na upendo wa dhati,Mungu atawalipa pale mlipoonesha upendo na ushirikiano wa dhati kwetu,hivyo sisi kama Familia tumerudi kushukuru maana tumefanikiwa kumpata kijana wetu akiwa salama kabisa.Shukurani nyingi kwa mtoa habari hii na Mungu amfanikishe sana sana
 
Kila la heri na MUNGU awabariki pia.
 
Back
Top Bottom