Kwa nilichokiona leo, Watumishi wa Umma wategemee nyongeza ndogo chini ya 10% na sio 23 kama wanavyotarajia

Sasa unaongezaje elfu 20 KWa watumishi ambao wamekaa miaka sita BILA nyongeza ,huo ni utani, tunasema nchi maskini wakati wao wanajilipa a lot of money,?
Yani wafanyakazi wa chini linapokuja swala la stahiki zao ndo tunaona nchi maskini, wakati wabunge n.k wanaongezewa mapesa, mav8 yanaunguluma mda wote, Sasa tafaaili ya nchi bado maskini ni ipi
Watumishi wakikutana na nyongeza ya ajabu, na wakaa kimya watakua hawajitambui,

Kama nchi ni maskini anzeni punguza maposho,mishahara yenu, uza mav8 Ili twende sawa
 
Huwezi fanikiwa maisha kwa kutegemea nyongeza ya mshahara,buni miradi mbalimbali midogomidogo ya kukuongezea kipato,pathetic!
 
Jeshi la Polisi ndiyo kichaka cha Sukuma Gang ambao wameapa kuhakikisha hadi kufika 2025 Hangaya hatamaniki,na kwa uteuzi wa DCI huyu lengo hilo litafikiwa kwa asilimia tisini na tano
Si mlisema sukuma gang imekomeshwa?
 
Ulaya wanapitia heat wave.. watumishi wa tz wanapitia salary increment wave.
 
Ndiyo maana wenye kuitakia mema nchi wanasema elimu yetu inawalakini, wasomi wetu walipigwa na akadabla ya hesabu za asilima, mama akaongeza kodi kwenye mishahara anapunguza mafao ya uzeeni, kisha akawawekea 23% majuha yakawa yanaimba mama anaupiga wingi 😂😂😂, nadhani elimu ya fikra ndiyo ilikuwà inahitajika kufundishwa kuliko elimu shahada. Maana wengi wao waliokuwa wakiimba mapambio ya mama kaupiga ni wasomi ambao walishindwa kung'amua algebra ya asilimia, kama mama kawapiga matofali mazito ya kichwa.🙊😷
 
Mkuu usiwe msahaulifu kihivyo Mhe Kikwete alikuwa akitamka inaenda kuongezeka kwa wote hasa walimu na afya rate Ile Ile
 
Mkuu usiwe msahaulifu kihivyo Mhe Kikwete alikuwa akitamka inaenda kuongezeka kwa wote hasa walimu na afya rate Ile Ile
Ni kweli Kikwete alikuwa anatamka kwa wote. Juzi Kenya waliongeza kwa wote asilimia ile ile, Ghana hivo hivo .
Tofauti Mama aliamua kuongeza asilimia ya kima cha chini tu.
Soma Kwa utulivu
 
Nchi hii ngumu. Nisiseme sana
 
Ulichoandika hakishabihiani na title,kiufupi unaropoka mambo usiyoyaelewa..

Ongezeko la salary ni Kati ya 40,000-55,000 kulingana na scale ya mtu..

Rais aliongeza 23.6% ya kima cha chini na sio 23.6% ya gloss salary so any increament hapo itakuwa subjected to statutory deductions and henceforth take home itaongezeka kwa kiasi nilichotaja sanjali na gross salary
 
Saiv ni mwendo wa kushindia vipande vya mihogo..kula ngano na wali ni luxury.
 
Huo ndo ukweli wenyewe na iko hv kwa wale Maafisa utumishi ambao wana access na mfumo wa mshahara mkeka walishauona ongezeko ni Tshs 20000 flat rate
Hiyo nyingi mno kwa huduma mbovu watumishi wanazotoa kwa wateja wao.
 
Hiyo ndio hali halisi.
Yani nimecheka kijinga Sana,maana
Nimechukua miaka 6 bila nyongeza ×12 month=72month
Then tsh20000÷72month=tsh 278 per month,
So kama kweli mtumishi wa tz kila mwezi alikua anaongezewa 278 tsh Katika kipindi Cha miaka 6
Dunia simama nishuke
 
Wanataka kumlaumu Raisi tu, ikiwa alishasema wazi kuwa ongezeko ni kwa kima Cha chini.
Watumishi wengi wa umma ni walimu, hivyo sishangai kuwa na misinterpretation
 
Yani nimecheka kijinga Sana,maana
Nimechukua miaka 6 bila nyongeza ×12 month=72month
Then tsh20000÷72month=tsh 278 per month,
So kama kweli mtumishi wa tz kila mwezi alikua anaongezewa 278 tsh Katika kipindi Cha miaka 6
Dunia simama nishuke
Kama unaona ndogo acha kazi. Acheni ujuha nyie walimu msiojielewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…