Yapo ambayo Mama anaongozwa kweli kabisa, ila sio hili la nyongeza ya mshahara.
Nyongeza ya mshahara haijawahi kuwa zaidi ya elfu 50+, hata enzi ya JK.
Shida ni kwamba mtangulizi wa huyu Rais wa sasa hakuwa akiongeza kila mwaka. Sasa watu walifikiri wakisema nyongeza itakuwa laki 1, 2, 3. Si kweli.
Kwa Uchumi wetu ulivyo ktk nchi, kiwango anachoweza kuongeza, net kabisa kwenye akaunti za benki ikasoma ni hizo hela kuanzia shilingi elfu 7 (7,000/- Tsh) hadi kufikia elfu 30 huko.
Kuhusu nyongeza ya 23% aliyotamka wkt wa Mei mosi, ile ni kweli na kasomeni tena ile barua, inasema, nanukuu kwa ufupi....., "Rais ameridhia nyongeza ya mshahara serikalini/kwa watumishi wa Umma, ikiwemo ongezeko la 23% kwa kima cha chini cha mshahara....."
Sasa waTz either ni wavivu wa kusoma katikati ya mstari "read between the lines" ,au hesabu inawachenga sana.
Haya maneno yana maana,
.... ikiwemo ongezeko la kima cha chini cha mshahara kwa 23% ....
Sasa kima cha chini hadi JK anatoka ni sh 300,000/-. JPM hakuwahi kuongeza.
Sasa mh Samia kawaongeza sh 69,900/- hao wa laki 3 kushuka chini.
Barua haikutaja kuwa waliokuwa wanapokea mshahara wa zaidi ya laki 3, wameongezwa sh ngapi!!
Kwa hiyo acheni kupamba pamba, eti mama anapotoshwa sijui ooh wanataka achukiwe.
Katika hili la nyongeza ya mshahara huo ni uongo au maneno ya kuunga unga.
Huo ndio ufafanuzi sahihi.