Uchaguzi 2020 Kwa nilichokiona Mbeya Town, Sugu nakuomba urudi kwenye muziki wa kufoka foka, Dr. Tulia atakulaza asubuhi sana

Uchaguzi 2020 Kwa nilichokiona Mbeya Town, Sugu nakuomba urudi kwenye muziki wa kufoka foka, Dr. Tulia atakulaza asubuhi sana

macho yako yatakuwa na makengeza na yanakudanganya….
 
Kila kona ya jiji wanaimba jina la Dr Tulia Ackson, wanasema huyu mama amejitolea kuwahudumia wana Mbeya

Amewezesha sacsos nyingi sana karibu kila kata ya Mbeya, hizo saccos kwa kiasi kikubwa zimewezesha wananchi kujikimu na mahitaji ya kila siku.

Mama moja katika soko la Mwanjelwa aliyejitambulisha kama Mama Tarumbeta anasema, Huyu binti Tulia ana miaka michache tu tena aingie kwenye siasa ila amekuwa ni chachu kubwa kwa maendeleo ya wananchi wa Mbeya.

Anaendelea kusema, anasaidia sio kwamba ni tajiri ila ana moyo wa kutoa tofauti na viongozi wengine wa kisiasa waliopo Mbeya.

Vijana wengi wamehamishia matumaini kwa huyu dada ambaye toka awe Naibu Spika amefanya maajabu makubwa Tanzania.

My take: Mh Sugu ili kuepusha aibu ya mwaka tunaomba ustaafu ubunge kwa heshima, wana Mbeya wanakufanyia mazoezi ya kukuchinja kwenye boksi la kura.

Huu muda ungerudia kwenye muziki wa kufokafoka tu, huku kwenye Siasa wana Mbeya wamepata mwanamama ngangari anayeenda kuleta mapinduzi katika mkoa wa Mbeya.

Tuipende Tanzania

Pesa hiyo kwa mtumishi wa umma ameipata wapi, nenda Fanya tathmini ya anachokitoa dhidi ya pato lake. Hatuhitaji rushwa tunahitaji watu wenye uwezo wa kuleta Sera mbadala, badala ya ndio mzee.

Ni aibu kwa mtz kupromote rushwa nani aibu zaidi kama mtz Huyo ni mwanamme.

#kampeni kabla ya muda ni haki kwa baadhi
#Anzakanoon
 
Huyo tulia sikuzote alikuwa wapi,mpaka autake ubunge ndio afanye mambo hayo.hana sifa ya kuwa mbunge,anatoa rushwa ili apate ubunge.kama anafanya kwa kuwapenda wana mbeya basi anaweza kuendela kuwahudumia bila kuwa mbunge..
 
Hizo ni hela anapewa ili zimpatie ubunge sasa subirini baada ya kupata anachokitafuta ndo mtaelewa kwamba kuna mahusiano gani kati ya chizi na makopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1587031990417.png

Wenye akili zao ambao hawawazi kila siku kuua wapinzani wao!!
 
Yeye hafanyi kampeni Wananchi wanamwomba agombee na pia Wananchi walimuomba asaidie yeye hakujipeleka

Back
Top Bottom