Naam nimeshachoka kuona gari zinakufa injini Kila siku gereji vijna mnapenda magari ila hamyajui mwisho yanawapa hasara
Sasa jirani yangu hapa ana Toyota Ist ina engine ya 1nz Bado mbichi tu no EG Gari ilikuwa inaenda kufa kizembe, juzi asubuhi Ile naamka niende kwenye mishe zangu nikaskia kawasha gari Yake ila Kuna kelele sio za kawaida nikawa naziskia yaani kama vyuma kwenye engine vinang`atana mean Kuna mahali kwenye engine oil ilikuwa haifiki
Nikamwambia zima hiyo gari haraka huo mlio sio sahihi, nikamuuliza umepima oil ipo kiwango Gani jibu hapana yaani kawasha tu anataka kuondoka
Kupima oil nikakuta ipo ila nyepesi mean inaonekana ilikuwa ni feki ikabidi nimuulize alibadili lini na wapi
Akasema alimpepekea fundi kariakoo fundi ndio akamuelekeza kwenye kiduka akanunue 5w 30 sh 50,000 na filter sh 10,000 nikasema kashehe hili umeona wapi oil og 50000 na hapo usikute inauzwa. 35000 fundi kala ganji 15000
Nikamwambia oil uliyowekewa ni feki filter nayo ni feki maana yake Kuna sehem injini haipati kilainishi ndio hivyo vyuma ndani Humo vinalia krrrrrrrriii nikamuelekeza sehem 3 zenye oil og na Lita 5 ni 170,000 Hadi 135,000 kwa Lita 4 nikamwambia nenda sheli iwe puma,Total,Branch za Atlantic au Liqui moil mikocheni chukua moja kati ya hzo na iwe 5w 30 na oil filter akanunue Toyota genuine parts wenyewe na filter SI chini ya 35000 beba njoo na fundi akuwekee
Baada ya kufuata hayo maelekezo injini ule mlio ukapotea Moja Kwa Moja maana yake kama sio kumshtua alikuwa anaenda kulia na ndio vilio vingi sasa hivi mtu ana gari Bado mbichi anatafuta mswaki au anabadili injini mzima
Kwa sasa oil feki ni nyingi Kwa usalama wa gari yako acha kabisa kumwambia fundi niwekee oil wewe mafundi wamekuwa ni vibaka na hawajali gari ya mtu
Oil nenda kanunue mwenyewe Kwa wahusika wanaoaminika nadhani mnaona watu wa Mazda kila siku wanavyolia kilio kimehamia mpaka Subaru Forester na gari za ulaalya hazitaki vitu feki ukiweka kimiminika cha kuchovya tu umeisha