Ismoo
JF-Expert Member
- Apr 18, 2018
- 1,101
- 1,573
Au sio [emoji23]Ingekuwa vizuri Sana tungekuwa tunafanya student exchange na nchi hizo masikini kuliko Sisi ili vijana waache kulalamika waone fursa au kushukuru Tu wamezaliwa Tanzania
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Au sio [emoji23]Ingekuwa vizuri Sana tungekuwa tunafanya student exchange na nchi hizo masikini kuliko Sisi ili vijana waache kulalamika waone fursa au kushukuru Tu wamezaliwa Tanzania
Halafu hii hoja yako ni mfu dini ni mfumo wa maisha na sio jina( ndo maan ulikuwa unasoma peke ako darasani).kwahyo kwasababu zamani watu walikuwa wanaita siku ya kwanza mpaka ya 7 kwenye wiki na sio jumapili mpaka jumamosi wewe utasema kuwa siku hazikuepo sio?Hakukua na dini ya ukristo toka yesu anakuja mpaka anasurubiwa.
Ukristo umeanza baada ya yesu kupaa...
Hata mimi nimeshangaa!1 burundi franc = 1.13 Tsh.
Mbona pesa yetu ndio haina thamani mbele ya pesa yao.
Sawa pastor tumekusikia[emoji3]Watu masikini wanaenda makanisani kutafuta faraja mmekazana kusema dini ndo imeleta umasikini sasa waliendaje kanisani wakiwa masikini bado. Hao machokoraa nao wanashinda makanisani emu acheni chuki binafsi na dini. We unaechukia dini unanua bando la mb 300 sasa nd umekomboka na nini hapo wakati kuna watu wanatoa sadaka milion 100 kanisani na wana marange rover.
Mimi nachukizwa sana na swala la waafrica kutafuta mwavuli wa kufichia umasikini wetu wakati kila mtu anajua tatizo liko wapi. Sasa mtu anakuja anaropoka dini ukimuuliza ni kwa fact gani utasikia watu wanasali muda ote. Hii hii nchi watu wana michepuko ya kutosha kuna walevi wa kutosha ila mtu anakuambia dini. Masikini mwenyewa kanisani anatoa sadaka buku mbili kwa wiki ambayo kwa mwaka haifikia hata laki na 20 ila utasikia dini imenifirisi.Sawa pastor tumekusikia[emoji3]
Mh labda hao ni walugaluga tuUjatembea KE wewe nenda Eldoret au Nairobi alaf waambie ni MTZ uone maneno ya shombo tulienda kipindi flani pale Nakumat Garille Supermarket Nairobi tukasema sisi ni from TZ aisee jamaa wakaanza kutushambulia "How come waTZ wanabonga kinge vzuri hivi?Nyie sio wa TZ wa TZ hawajui kinge"
AhaaaaaaMbona laisi wa miamba lizard mwenyewe alisema "twende burundi"? Taarifa alikuwa hajui !!
Tubadilishane mademu pia [emoji17]Ingekuwa vizuri Sana tungekuwa tunafanya student exchange na nchi hizo masikini kuliko Sisi ili vijana waache kulalamika waone fursa au kushukuru Tu wamezaliwa Tanzania
Yesu alikua mkiristo mkuu,, 😂Huyo Yesu mbona hakua na dini au unajua alikua ni dini gani?
Yeah, tunashindia sandwich 🥪, mayai boilo na sausage 😁Nairobi hata mjini hali mbaya tu. Majority wamepanga kwenye majengo ya matajiri wachache... hali ni ngumu mno Nairobi. Watu wanashindia mikate. Mkenya ukimnunulia pilau anashangaa mno.
Nigeria itoe hapo weka Dakar pale ongeza Mauritius, Cape Verde na Sao Tome & Principe.Nafikiri Bongo inakimbiza nchi nyingi za Afrika ukiacha nchi kama South Africa, Kenya, Namibia, Botswana, Nigeria kwa huu ukanda wa kusini mwa Sahara. Kuna kipindi nilienda Accra Ghana, aisee nikajiuliza hawa watu wakija bongo wanaweza kupaona ulaya.
Kuna NGO ilikua inafanya. Sema za Afrika ilikua chache na ilikua Ghana, Mozambique na SA.Ingekuwa vizuri Sana tungekuwa tunafanya student exchange na nchi hizo masikini kuliko Sisi ili vijana waache kulalamika waone fursa au kushukuru Tu wamezaliwa Tanzania
aiseeKwenye "kusaka tonge" Nimejikuta mara kadhaa nadondokea kwenye nchi jirani ila hii nchi ya BURUNDI inanifanya kila siku nizidi kuthamini na kuipenda TZ..Burundi ni nchi ambayo imepitiwa na Bonde la UFA "Rift valley" sasa sijui ni geographical area ndo inasababisha umaskini huu au ni nini? Lakini mbona Rwanda Nao ni nchi ndogo tena walikua Level moja kiuchumi miaka kadhaa ila Leo Rwanda iko mbali sana.
MIUNDOMBINU:
Barabara ya TZ ni nyembamba ila ya Burundi ni nyembamba Pro max na inamabonde,Mashimo,Kona na miinuko ya kufa mtu.Ajali ni kila siku tena zinaua kuliko za bongo.Mbaya zaidi wanatumia protocol ya barabara(Left na Right) kinyume na hii yetu hali ya kuwa magari mengi ni (Right hand)Kwaio kuovertake mpama utokeze mzimamzima kuchungulia hapo ndo msala unaanzia.kifuatacho ni INNALILLAH..BWANA ALITWAA..RIP
USAFIRI:
Burundi inamikoa zaidi ya 7 ila Airport iko moja tu nchi nzima (BUJUMBURA tu)..Usafiri wao sanasana ni TAX(probox mchomoko) bodaboda na Baiskeli ndo za Kumwagaa....!!!
MAMBO YANAYONISHANGAZA:
~Sio waislamu wala christians Burundi watu ni wafia dini yani wanajua na wanapenda dini balaa makanisani panajaa miskitini panajaa.Naamini dini zetu zinachangia pakubwa sana kwenye umaskini hapa Mzungu na Mwarabu walituweza washenzi wale...!!!
~Elimu HONGERA kwa Sekta ya Elimu ya TZ japo mtaala ni mbovu ila kwenye uniform TZ ilipatia sana..Haiwezekani wanafunzi wa Burundi sketi hazijawekewa Marinda yani zinachora shepu na vitoto vya sikuizi miaka 14 tu shape hiyoo.Watu kama KENGE tunapata tabu sana Wakuu..pia hata KENYA vyanafunzi vinavaa sketi fupi mno sijajua kwa UG na Rwanda.
Burundi wanapata sana Scholarship za France kwakua ni Colon lao..Elimu ni kuanzia la kwanza mpaka 13-16...
~Burundi hakuna Vivutio vya Utalii wala Mbuga za wanyama.Cha zaidi ni (Game reserve) Kinachoniuma kwenye Geography tulisoma Maeneo yaliyopitiwa na Rift valley yanaasilimia kubwa kutoa milima mirefu kama Oldonyo Lengai,Everest n.k Lakini kwa Burundi Hakuna Mlima hata mmoja wa kivutia cha utalii licha ya kuwa na miinuko,Mabonde nchi nzima
Cha kusikitisha kuna Ziwa Tanganyika ila Hakuna Mamlaka ya maji kama DAWASCO kwa TZ yaani kifupi kuna mgao wa maji hasa kule RUMONGE mkoa mzima umepakana na Ziwa ila kuna shida kubwa sana ya Maji Umeme ndo usiulize.
Mziki wanasikiliza wa TZ na Maeneo kama Rumonge wanaongea kiswaili vzuri kabsa ila Bujumbura ndo kuna baadhi wanaelewa kiswahili licha ya kuwa lugha mama ni Kirundi lakini asilimia kama zote wanabonga Kiswahili
Burundi ni nchi pekee unayoweza kusema wewe ni Tanzanian na wakakushobokea..Yaani pamoja na kwamba Nina ngozi ngumu kama ya KENGE na Sura mbaya kama Lori la Mchele kule Mbeya...Lakini huku kwa warundi nikisema tu mimi M-TZ basi watoto wananishobokea balaa kiasi kwamba wanavuka mpaka na kuniita (Hensam boi) Hapa ndo nikashtuka..Nenda Kenya sasa Useme wwe ni m-bongo uone wanavyokudharau...!!
Pia,Nilichogundua Bongo machokoraa wa stendi ni wasafi kulinganisha na wa Burund...Choko wa Burundi wanajua kuomba aisee hawakuachi na ni vichafu kinoma ukijumlisha Udongo ni mwekundu maeneo mengi basi vinakua vichafuu,,vyeusii..Mungu atuepushe na Umaskini aisee lakini Awezi kutuepusha kama sisi wenyewe tumebweteka kusubiri wazungu watutengenezee kila kitu.
Vilevile Ukitembea jiji zima hakuna nyumba iliotengenezwa kwa Tofali za Block..ni mwendo wa (Tofali za Choma)
Nchi kama hizi Chakula sio shida kwasababu uti wa uchumi wetu ni Kilimo kwaiyo vilevile Burundi Wanakima kila kitu na Kufuga kwaio nyama na Maziwa ni kama zote..Wana Ugali wao wa Roi umetengenezwa kwa Mihogo bongo inabidi tuutumie ni mzuri kwa Afya japo ukiskia unavyotengenezwa unaweza kuhairisha/Kususa kula..
View attachment 2606757
~VYUO VIKUU vinapatikana Bujumbura tu
~AIRPORT ni moja tu nchi nzima
~FARANGA haina thamani kabsaa ukichange 100k Tsh kuwa Faranga wewe ni taita..
~Kama wabongo tu wanaamini South kwa Madiba ndo kuna Maisha yani ukifika umetoboa..
~Maeneo mengi vijijini gari likipita wanalishangaa wakubwa kwa watoto
Pamoja na yote BURUNDI wanazaliana balaa sio ajabu kukuta Mzee anawake wawili na kila Mke anawatoto 10+ nafkir ni kwasababuSTAREHE YA MASKINI NI KUDINYANA
Fursa za Ajira kwa wabongo ukija ukosi kabsaa yani kama unataka utoboe mapema ujenge mapema nenda Burundi kama unaakili ya pesa utapiga sana kwasababu bado wako nyuma ya muda
Narudi kuendelea,bado nipo bujumbura
View attachment 2606756
Pesa na Uchumi ni vitu 2 tofauti, kibiashara yetu hapo ndio inafaida sio hiyo ya Burundi.1 burundi franc = 1.13 Tsh.
Mbona pesa yetu ndio haina thamani mbele ya pesa yao.
Siwezi kuishi Nigeria ni hovyo tuu ,South Africa hakuna usalama hata Kwa bunduk hunipelekeki..Asante Kwa taarifa,sijafika Burundi Wala Sina mpango wa kwenda huko.
Nilikuwa naamini Burundi ni kuchafu Sasa umenikazia maarifa .
By the way Africa Kuna nchi masikini sana ukifika tashangaa
1) central Africa
2)Togo
3) Mozambique ( hasa northern party)
4) Burkina Faso Kwa kina Aziz ki
5)Chad
6) DRC
7) Madagascar
8) Mali
9) Niger
10) Eritrea
11)congo Brazzaville
12) sudani kusini
13)Ethiopia ( usione Wana midege,ni malofa haswa)
14) Benin
15)Liberia
...........
Nita kutafuta mkuu ,nimetamani kwenda huko.Japo mengi ya aliyosema mtoa Uzi yana ukweli 90%, napenda kuongeza mazuri ya Burundi
[emoji117] Warundi ni watu wakarimu sana kwa jamaa, ndugu na marafiki zao.
Ukifika, watakuja kukutembelea wakiambatana na sukari, mkate au pesa taslimu (ya sukari na mkate)..
Swali la kwanza kwa mgeni: "utakunywa fanta au bia..?" [emoji28]
[emoji117] Burundi kuna fursa za wazi kabisa kibiashara. Na hapa mimi niliona uhaba wa gesi ya kupikia. Familia nyingi zinatumia mkaa, chache zinatumia gas
Hivyo km mtu anaweza kuchangamkia fursa hii, bas atatoboa
[emoji117] Biashara ya kubadilisha fedha inalipa sana hapa. Forex zipo nyingi, lakini mahitaji ni mengi zaidi.
Warundi Wana ndugu wengi Canada, USA, Belgium, France, na nchi nying za uarabuni, hivyo usishangae kumuona bibi kizee tu anajua kupanda na kushuka kwa dollar, uero, n.k
[emoji117] Buja ni mlango mpana wa kwenda ng'ambo. Watu wengi wa mikoa jirani (mfn kigoma, kagera, musoma) wanatumia sana mlango wa buja kwenda ughaibuni. Kwa bongo hata kupata tu passport ni jasho
[emoji117] Ukitaka kuona jinsi watu wanafurahi, basi njoo Bujumbura. Pamoja na shida za kisiasa walizonazo lakini hawa viumbe ni watu wa kufurahi muda wote. Wanapenda pombe kuliko kitu kingine chochote km sijakosea. Bia maarufu ni primus na Amstel
[emoji117] Bei ya bidhaa muhimu km sukari, sabuni, mafuta, dawa n.k viko chini sana ukilinganisha na Tz.
Kwa sasa sukari imeadimika sana hapa buja, lakini pamoja na kuadimika huko, bei ya kilo moja ni 2500fbu, petrol ni 2700fbu
Isipokuwa kwa bidhaa zinazotoka nje, hizo bei zake zinategemea stability ya dollar
[emoji117] Hotels za buja zinajaa kila siku. Unaweza tembelea hotel 3-5 ukaambiwa zimejaa, si ajabu hii
Hii inaonesha bado kuna fursa za uwekezaji wa biashara ya nyumba za wageni (hotels) na ukapata faida
[emoji117] Hakuna asiyejua km watusi wanamuonekano mzuri. Hivyo hili libaki hapo[emoji28]
[emoji117] Bujumbura (ville/mjini) hakuna bajaji, bodaboda wala baiskeli (Kinga). Usafiri wa tax ni WA gharama nafuu kuliko Tz. Japo tax za hapa nyingi ni probox na hazina hali nzuri sana ukilinganisha na Tz.
Mjini hauno msongamano wa magari km bongo
[emoji117] Azam ameteka soko la juice na biskuti hapa buja. Hii inakupa picha kuwa fursa za uwekezaji zipo na uhitaji ni mkubwa sana.
Wazawa wanahifia kuwekeza nchini kwao, kwa sababu ya kiusalama, lakini wageni wanalindwa vya kutosha
Mambo ni mengi, lakini Burundi ndio nchi ya kwanza kwa umasikini duniani. Na kwa sababu hii, wenye akili nyingi wanaweza kuitumia kujitajirisha