Utajiri namba moja ninaomiliki ni kutambua kua dini ni kwa ajili ya matajiri ndio maana ukienda kanisani unakutana na masanduku ya Sadaka, masikini asie na kitu akienda kanisani anaonekana hajatoa kitu anaonekana hajafanya ibada yoyote na kaenda kanisani kujaza wingi tu, kwa hio maarifa niliyonayo ya kuyatambua hayo ni moja ya utajiri tosha, maana utajiri uanzia kwenye akili sio kwenye utashi sio kwenye hisia hapa nazungumzia Maarifa ambavyo vyote kwa pamoja vipo ndani ya mfumo wa Nafsi, mfumo wa Roho unajihusisha na Imani ili uwe tajiri lenga mfumo wa Nafsi yako ambao umegawanyika katika sehemu kuu 3 yaan akili, utashi na hisia ambavyo kwa pamoja vinahusisha Maarifa na ili uwe tajiri inabidi uwe na Maarifa ya kutosha ambayo yanahiusisha akili yako
Nimekujibu kwa kadri inavyowezekana ili uelewe angalau, Vita zote ambazo binadamu hupambana huanzia kwenye mfumo wa Roho unapigwa Roho kwanza baada ya kuishinda Roho adui anahamia kwenye mfumo wa Nafsi na akiushinda mfumo wa Nafsi ndipo adui uhamia kwenye mfumo wa Mwili, mkumbuke yule mchungaji wa Mchongo wa Kenya Paulo Mackienz yeye alicheza kwanza na mfumo wa Roho wa waumini wake kisha akahamia kwenye mfumo wa Nafsi (Maarifa) akilenga Maarifa ya uongo ya kwneye Biblia kwamba ukifunga hadi kufa utaonana na Mungu na kwa kua alishawashinda wale waumini kwenye Vita ya mfumo wa Roho akawashinda kwenye mfumo wa Nafsi mwisho akawamaliza mfumo wa Mwili wakafa vibudu
Una swali jingine uliza uwanja ni wako,