Japo mengi ya aliyosema mtoa Uzi yana ukweli 90%, napenda kuongeza mazuri ya Burundi
[emoji117] Warundi ni watu wakarimu sana kwa jamaa, ndugu na marafiki zao.
Ukifika, watakuja kukutembelea wakiambatana na sukari, mkate au pesa taslimu (ya sukari na mkate)..
Swali la kwanza kwa mgeni: "utakunywa fanta au bia..?" [emoji28]
[emoji117] Burundi kuna fursa za wazi kabisa kibiashara. Na hapa mimi niliona uhaba wa gesi ya kupikia. Familia nyingi zinatumia mkaa, chache zinatumia gas
Hivyo km mtu anaweza kuchangamkia fursa hii, bas atatoboa
[emoji117] Biashara ya kubadilisha fedha inalipa sana hapa. Forex zipo nyingi, lakini mahitaji ni mengi zaidi.
Warundi Wana ndugu wengi Canada, USA, Belgium, France, na nchi nying za uarabuni, hivyo usishangae kumuona bibi kizee tu anajua kupanda na kushuka kwa dollar, uero, n.k
[emoji117] Buja ni mlango mpana wa kwenda ng'ambo. Watu wengi wa mikoa jirani (mfn kigoma, kagera, musoma) wanatumia sana mlango wa buja kwenda ughaibuni. Kwa bongo hata kupata tu passport ni jasho
[emoji117] Ukitaka kuona jinsi watu wanafurahi, basi njoo Bujumbura. Pamoja na shida za kisiasa walizonazo lakini hawa viumbe ni watu wa kufurahi muda wote. Wanapenda pombe kuliko kitu kingine chochote km sijakosea. Bia maarufu ni primus na Amstel
[emoji117] Bei ya bidhaa muhimu km sukari, sabuni, mafuta, dawa n.k viko chini sana ukilinganisha na Tz.
Kwa sasa sukari imeadimika sana hapa buja, lakini pamoja na kuadimika huko, bei ya kilo moja ni 2500fbu, petrol ni 2700fbu
Isipokuwa kwa bidhaa zinazotoka nje, hizo bei zake zinategemea stability ya dollar
[emoji117] Hotels za buja zinajaa kila siku. Unaweza tembelea hotel 3-5 ukaambiwa zimejaa, si ajabu hii
Hii inaonesha bado kuna fursa za uwekezaji wa biashara ya nyumba za wageni (hotels) na ukapata faida
[emoji117] Hakuna asiyejua km watusi wanamuonekano mzuri. Hivyo hili libaki hapo[emoji28]
[emoji117] Bujumbura (ville/mjini) hakuna bajaji, bodaboda wala baiskeli (Kinga). Usafiri wa tax ni WA gharama nafuu kuliko Tz. Japo tax za hapa nyingi ni probox na hazina hali nzuri sana ukilinganisha na Tz.
Mjini hauno msongamano wa magari km bongo
[emoji117] Azam ameteka soko la juice na biskuti hapa buja. Hii inakupa picha kuwa fursa za uwekezaji zipo na uhitaji ni mkubwa sana.
Wazawa wanahifia kuwekeza nchini kwao, kwa sababu ya kiusalama, lakini wageni wanalindwa vya kutosha
Mambo ni mengi, lakini Burundi ndio nchi ya kwanza kwa umasikini duniani. Na kwa sababu hii, wenye akili nyingi wanaweza kuitumia kujitajirisha