Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Mimi nachukizwa sana na swala la waafrica kutafuta mwavuli wa kufichia umasikini wetu wakati kila mtu anajua tatizo liko wapi. Sasa mtu anakuja anaropoka dini ukimuuliza ni kwa fact gani utasikia watu wanasali muda ote. Hii hii nchi watu wana michepuko ya kutosha kuna walevi wa kutosha ila mtu anakuambia dini. Masikini mwenyewa kanisani anatoa sadaka buku mbili kwa wiki ambayo kwa mwaka haifikia hata laki na 20 ila utasikia dini imenifirisi.
Dini inasingiziwa tu sababu za umaskini nchi hii zinajulikana
 
Maandiko yanasema siku sita fanya kazi siku ya saba pumzika muabudu Mungu we unazungumzia dini ipi. Sababu watu katikati ya wiku huwa wanakutana kwa nusu saa tu(30 minutes) elezea wewe hizo dakika zinamzuru vipi mtu kuwa masikini. Hutaki kuzungumzia mtu anaeshinda kwenye michepuko masaa hata 8 club masaa 8 kuangalia mpira masaa mawili ( mpka 8 sababu mechi ni nyingi) ila umekazana na dini tu.
Nawaamuru acheni kuharibu uzi kwa mambo ya dini.
 
Thibitisha madai yako kwa mifano na onesha sehem ambazo hazina dini zina maendeleo. Riverside kuna uzinzi wa wazi onesha kama kuna maendeleo makubwa zaidi kwa watu wake. Zile range zinazopaki makanisani na sadaka za milion 100 zinatoka wapi?
Kuna wezi kibao, wauaji kibao, watoa kafara kibao, wako pale kuzuga tuu, fuatilia ipo siku utagundua ninachosema.
 
Mombasa wana interchanges kadhaa, vivuko vikubwa pale Likoni. Mji wa kihistoria kiasi fulani, tabia kiasi kama za Tanga. Kuna Wasomali, Wahindi na Waarabu, mida ya jioni kuna kahawa/chai, kachori na vipochopocho hasa kwa wale wafanyakazi mjini mabachela. Sijui kama bodaboda wao wanakula half cake na energy drinks kama wetu.
Watu wa bara huwadhiaki wa Pwani kuwa ni wazembe, wa Pwani huwaona wa bara sio wastaarabu. Ni kama sisi

Polisi wa Kenya bora wa Tanzania, ila ukiwa na hela Kenya unauza chochote tena rushwa unaelekezwa. Unamgusa kidogo mpenzi wako wanawake wa Kenya ni empowered zaidi ya wetu, anakuitia polisi anawaonga unakaa lock up usipotaka kutoa rushwa wanakushangaa. Mahabusu uko polisi wanapita kuuliza umefanya kosa gani, ukisema kosa la kijinga wanakulaumu kwa nini uko ndani wanakwambia lipa let's say 10,000 hapo 5,000 ya polisi na boss wake na 5,000 ya hakimu. Unaelekezwa useme nini kesho na kesi yako inaitwa, unafanya vilevile na unatoka.

Kenya daladala nyingi ni SACCO, niliuliza hizi zinaubdwaje sikuelezwa vizuri anayejua anambie. Kuna chakula wanaita smokie sijui ni nini, sausage kama vile kuna neno lake. Pikipiki sijaona Boxer na TVS kwa wingi.

Mengine waseme wengine.
Kweli polisi wa Kenya ni wapenda rushwa balaa na makatili. Ila nachowapendea hawana konakona kwenye kutaka rushwa. Kwa mfano kwenye checkpoint ya kwenda Nairobi kutokea Namanga walikuwa na kiwango chao cha rushwa kama huna passport
 
Mkumbushe Mjerumani kaondoka Namibia 1990!!! In short Jiji lao ni Windwook ( sp) sio mchezo Dar ikaoge ,TREN za umeme wao ni ujinga tuu sisi ndio tunaanza!!
Windhoek gani ambayo inaiacha mbali Dar?

Hivi humu vichaa ni wengi kiasi hiki eeh.

Umewahi kufika au unaongea tu?
 
Uchumi unazungumzwa kwa vipimo. Namibia iko juu kiuchumi kwa kipimo gani ni GDP, PPP, GDP per capita au nini.
Wako kama milioni tatu nchi nzima, wanatuzidi GDP per capita, standard of living, mishahara na huduma bora za jamii. Tunawazidi GDP, tuna population kubwa, maji mengi, ardhi ya rutuba na hali ya hewa nzuri.
Ukitoka bongo ni vigumu kufanya biashara Namibia hawana konakona na hawataki mitaji midogo, huwezi kwepa kodi wala kuuza bidhaa feki. Namibia hakuna madawa ya Kihindi kwenye pharmacy unakutana na vitu vya Pfizer, Merck, Bayer yani kule ni rahisi kukutana na dawa ya original/patented producer ila bongo dawa karibia zote tunanunua kwa walionunua rights za kutengeneza.

Gari unaweza nunua kwa mkopo ukakatwa kwenye mshahara, nyumba unaweza chukua mortgage bongo sijawahi ona labda ipo, gari used ni kama hakuna mara nyingi wanatoa South Africa mpya na hakuna mafundi wa chini ya muembe mara nyingi ni dealers wana service na warranty zinazingatiwa.

Sina uhakika sana ila hakuna Tecno, Infinix wala Itel ila Wachina wapo ingawa sio wengi. Samsung, iPhone na brands kubwa. Simu used sio rahisi kama bongo hapa na "used from Dubai". Mitumba hamna hukuti mtu anamiliki magunia ya nguo, hakuna replicas na fakes sijui iPods za buku tano soko la Manzese.

Hakuna mamantilie na kuuza maandazi kwenye madumu ya plastiki. Hakuna maduka ya mangi, wana supermarkets zaidi ambazo bongo zimetushinda. Kupumzika mwezi December ni kawaida shughuli kibao zinafungwa na kama mahoteli yanafunga baadhi ya vyumba.

Hakuna bajaj na bodaboda, kupewa risiti ni kitu cha kawaida. Uchumi wao unategemea sana South Africa na makaburu wana ulinzi wa biashara zao, huwezi enda na Azam utaambiwa zina water content kubwa, sukari nyingi na some additives hazitakiwi. Wana figisu hivyo ni ngumu kuingilia biashara zao. Wabongo wako wanauza drugs uko, madaktari, pharmacists na wengine.

Wazungu wanafuga kisasa, wana uvuvi mkubwa baharini. Mfumo wao wa kodi TRA haiingii hata nusu, kwanza haukomoi na hauibiwi yani kurudishiwa kodi ni kawaida.

Hawana vitu vya misifa sijui kujenga jengo kubwa kupendezesha mji, wako 3 million na nchi ina ardhi kuliko Tz. Uchumi unaendeshwa na models za kizungu hawakurupukii miradi ya kunyonya damu.

Kwa hayo machache nimezungumzia maisha ya ushuani, vijijini sijui najua wanakula sana nyama na wanene kuliko sisi. Hawathamini sana wanawake kama sisi.

Kidogo niwasahau vijana wa hovyo. Kuna pisi mixer ya Wajerumani na makabila ya kule, kukuta mtu anaitwa Marina Krapf, Joachim Steinmann, Erwin Goering alafu mweusi tii ni kawaida.
NAMIBIA kwa namna yoyote haiwezi ingia kwa TANZANIA. NAMIBIA imeachwa mbali tuache kudanganyana humu ndani.
 
Nchi nyingine nasikia ni masikini wa kutupwa ni central Africa. Hapo Bangui makao makuu ya nchi nasikia pako Kama chalinze. Unaambiwa huko watu wanakula kila mdudu Hadi vyura watu wanapita nao[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ila sijawahi fika mie nmesimuliwa tu.
Umesema kweli. Uwanja wao wa ndege hata wa Arusha ni mzuri.

Uwanja unamipasuko kama yote yani.

Bangui ni kama Mji wa Namanga.

Usalama sio mzuri sana.
 
Kweli polisi wa Kenya ni wapenda rushwa balaa na makatili. Ila nachowapendea hawana konakona kwenye kutaka rushwa. Kwa mfano kwenye checkpoint ya kwenda Nairobi kutokea Namanga walikuwa na kiwango chao cha rushwa kama huna passport
Hata maofisa mipaka wa Kenya wanakuelekeza namna ya kutoa rushwa na namna ya kuwahonga upande wa Watanzania, nani umpe kiasi gani na nani umpe kiasi gani. Tena ukikosewa na Tz unarudi kwa Wakenya wanakupa mpango.
Trafiki Mbongo atatafuta kosa akilipata ajifanye mkali umpe, Mkenya unafika akihisi huna kosa anaomba hela direct. Wana kiwango chao sometimes daladala inapita inamdondoshea 50, hiyo ni bima next time ukiwa na kosa ufikiriwe. Uko ni Mombasa lakini, Nairobi wabishi hawatoi hela kizembe. Kukutana na polisi Kenya anazurula asubuhi mpaka jioni akitafuta quota aliyopangiwa na kamanda ni kawaida, ukikosa kufikisha unapewa kulinda sehemu hamna hela.
 
Msamehe bure huyo kwani hajatembea. Dar majiji mengi ya Afrika yakasome namba.
Humu kuna wajinga wanagoogle vipande vya mji basi, Yaani Windhoek iwe nzuri kuliko Dar? Au Namibia iwe bora kuliko Tanzania? Yaan nchi Jangwa tupy then iwe juu ya Tz?

Kwa SADC ni SOUTH AFRICA tu ndio imeiacha mbali Tanzania yetu hii, nimefika nchi karibu zote za SADC, Tanzania ni Nchi bora sana kwa kila Nyanja yaan hizo nchi kuna maeneo hayafikiki si kwa gari wala Bajaj, Tz pamoja na ukubwa karibu kila sehemu inafikika.

Unatembea Tz kwa amani, uwe ugenini au mkoani kwako, Tz unaishi kwa amani bila maswali wala nini. Narudi HAKUNA nchi inaizidi TANZANIA kwa SADC na EAST AFRICAN COMMUNITY isipokuwa KENYA na SOUTH AFRICA. Hao Wakenya wenyewe wana miaka michache tu wataachwa.
 
Japo mengi ya aliyosema mtoa Uzi yana ukweli 90%, napenda kuongeza mazuri ya Burundi

[emoji117] Warundi ni watu wakarimu sana kwa jamaa, ndugu na marafiki zao.
Ukifika, watakuja kukutembelea wakiambatana na sukari, mkate au pesa taslimu (ya sukari na mkate)..
Swali la kwanza kwa mgeni: "utakunywa fanta au bia..?" [emoji28]

[emoji117] Burundi kuna fursa za wazi kabisa kibiashara. Na hapa mimi niliona uhaba wa gesi ya kupikia. Familia nyingi zinatumia mkaa, chache zinatumia gas
Hivyo km mtu anaweza kuchangamkia fursa hii, bas atatoboa

[emoji117] Biashara ya kubadilisha fedha inalipa sana hapa. Forex zipo nyingi, lakini mahitaji ni mengi zaidi.
Warundi Wana ndugu wengi Canada, USA, Belgium, France, na nchi nying za uarabuni, hivyo usishangae kumuona bibi kizee tu anajua kupanda na kushuka kwa dollar, uero, n.k

[emoji117] Buja ni mlango mpana wa kwenda ng'ambo. Watu wengi wa mikoa jirani (mfn kigoma, kagera, musoma) wanatumia sana mlango wa buja kwenda ughaibuni. Kwa bongo hata kupata tu passport ni jasho

[emoji117] Ukitaka kuona jinsi watu wanafurahi, basi njoo Bujumbura. Pamoja na shida za kisiasa walizonazo lakini hawa viumbe ni watu wa kufurahi muda wote. Wanapenda pombe kuliko kitu kingine chochote km sijakosea. Bia maarufu ni primus na Amstel

[emoji117] Bei ya bidhaa muhimu km sukari, sabuni, mafuta, dawa n.k viko chini sana ukilinganisha na Tz.
Kwa sasa sukari imeadimika sana hapa buja, lakini pamoja na kuadimika huko, bei ya kilo moja ni 2500fbu, petrol ni 2700fbu
Isipokuwa kwa bidhaa zinazotoka nje, hizo bei zake zinategemea stability ya dollar

[emoji117] Hotels za buja zinajaa kila siku. Unaweza tembelea hotel 3-5 ukaambiwa zimejaa, si ajabu hii
Hii inaonesha bado kuna fursa za uwekezaji wa biashara ya nyumba za wageni (hotels) na ukapata faida

[emoji117] Hakuna asiyejua km watusi wanamuonekano mzuri. Hivyo hili libaki hapo[emoji28]

[emoji117] Bujumbura (ville/mjini) hakuna bajaji, bodaboda wala baiskeli (Kinga). Usafiri wa tax ni WA gharama nafuu kuliko Tz. Japo tax za hapa nyingi ni probox na hazina hali nzuri sana ukilinganisha na Tz.
Mjini hauno msongamano wa magari km bongo

[emoji117] Azam ameteka soko la juice na biskuti hapa buja. Hii inakupa picha kuwa fursa za uwekezaji zipo na uhitaji ni mkubwa sana.
Wazawa wanahifia kuwekeza nchini kwao, kwa sababu ya kiusalama, lakini wageni wanalindwa vya kutosha

Mambo ni mengi, lakini Burundi ndio nchi ya kwanza kwa umasikini duniani. Na kwa sababu hii, wenye akili nyingi wanaweza kuitumia kujitajirisha
Wanawake wa burundi, Zambia na rwanda wanatupenda sana watanzania.
 
Waburundi wengi wanakidharau kifaransa na kusema ni lugha ya umaskini.. ndoto zao ni kujua kiingereza. Pia kiswahili chao kimenyooka karibu sawa na bongo. Kiukweli Tanzania kwa sasa ipo kasi sana kulinganisha na nchi nyingi zinazotuzunguka. Bongo naona shida kubwa sana ni umeme. Kwa ukubwa wa nchi na idadi ya watu kiukweli umeme tulio nao ni mdogo mno.
Burundi bana hakuna kiswahili kilichonyooka

Sent from my PRA-LA1 using JamiiForums mobile app
 
Asante Kwa taarifa,sijafika Burundi Wala Sina mpango wa kwenda huko.
Nilikuwa naamini Burundi ni kuchafu Sasa umenikazia maarifa .
By the way Africa Kuna nchi masikini sana ukifika tashangaa
1) central Africa
2)Togo
3) Mozambique ( hasa northern party)
4) Burkina Faso Kwa kina Aziz ki
5)Chad
6) DRC
7) Madagascar
8) Mali
9) Niger
10) Eritrea
11)congo Brazzaville
12) sudani kusini
13)Ethiopia ( usione Wana midege,ni malofa haswa)
14) Benin
15)Liberia
...........
Ethiopia sio maskini wameizid hta tz kwa miondombinu ila tatzo lao maisha ya wananchi ni magumu sana ni km vile tu ilivyo china

Sent from my PRA-LA1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom