Kwa niliyoyashuhudia ibadani Kenya ni sahihi kabisa alichofanya Rais Magufuli kuzuia mikutano holela ya kisiasa hadi wakati wa kampeni

wananchi wa kawaida tunayajadili haya kwasababu sisi ndiyo walipa kodi,

KUB atatimiza wajibu wake kama KUB.

Hivi mnadhani watanzani wote ni mburula kama watoto wenu mnaowasomesha kwa malipo mnayopata hapo Lumumba??
Anza kwanza kuhoji matumizi ya kodi yako inayotafunwa kama ruzuku hapo Ufipa.

Anza kufagia chumbani bwashee kama kweli una nguvu ya kushika " mfagio"

Sumu haionjwi by Frederick Sumaye
 
Reactions: Oii
Sidhani kama unaelewa dhana ya siasa, siasa inafanyika katika maisha ya kila siku siyo wakati wa kampeni pekee. Hata viongozi wanapokuwa wanaongea hutoa statement za kisiasa na hii hufanyika on a daily basis, acha kutuingiza chaka mkuu....
 
Huna akili, siasa ya Kenya inahusishaje na ya TZ?
 


Ibada ni yao,wazungumze wanachotaka ni wao...

Rais watakao mchagua ni wao,wakimzungumzia wewe inakuhusu nini?

Usijifanye mawe alipiga marufuku siasa nchini sababu anaipenda sana nchi

Kila mtu anajua alipiga marufuku sababu anajua kabisa upinzani ukiachiwa huru wanachukua nchi maana yeye hajui siasa na hapendwi,thats clear!

Eti mawe anapenda sana utaifa eti ndio maana alipiga marufuku siasa,wewe una smoke kitu gani?

Na hoja yako ni hovyo zaidi maana mbona kipindi cha marais waliopita Mkapa,Kikwete,Mwinyi,Watanzania walikua huru na demokrasia,mbona hawakuongelea makanisani?

Iweje wewe leo uone eti wangezungumzia kama walivyo Wakenya?

Majitu yanamtetea mawe hua hayana akili hata kidogo.

Hii ndio quality ya mawazo ya majitu yanayotetea dictatorial tendencies za mawe?

Tuna hatari sana!
 
Hahahaaaa......... Bwashee umekasirika sana!

Upinzani gani utakaochukua nchi?........huu unaosubiri Tume huru ya uchaguzi kwenye sahani?

Mtasubiri sana.
 
Anza kwanza kuhoji matumizi ya kodi yako inayotafunwa kama ruzuku hapo Ufipa.

Anza kufagia chumbani bwashee kama kweli una nguvu ya kushika " mfagio"

Sumu haionjwi by Frederick Sumaye
CCM ruzuku ni sh ngapi na CDM ni sh ngapi?Maana huwa siwaelewi kanisa mnaoleta hii hoja wakati CCM anapokea zaidi ya mara 6 ya anachopkea CDM!

Kwanini manunuzi ya JPM na fungu lake la ikulu hataki yakaguliwe?Tuanzie hapo!
 
Hahahaaaa......... Bwashee umekasirika sana!

Upinzani gani utakaochukua nchi?........huu unaosubiri Tume huru ya uchaguzi kwenye sahani?

Mtasubiri sana.
Furahia tu,siku watu wakichoka kudhulumiwa na wewe hutakuwa salama!Sehemu ambapo haki haipo kisiasa na kiuchumi,ni rahisi sana kupenyeza ugaidi au uasi!Ukute yule extrimist aliyechoka kunyanyaswa,ukampa tu silaha basi umemaliza!Tusijifanye tumesahau ya Kibiti,sasa imagine hiyo sumu ingekuwa imeenea nchi nzima ingekuwaje?
Endeleeni kufurahi kuwa na Tume mliyoiweka mfukoni,ila siku mambo yakiharibika tunaharibikiwa wote!
 
Hahahaaaa......... Bwashee umekasirika sana!

Upinzani gani utakaochukua nchi?........huu unaosubiri Tume huru ya uchaguzi kwenye sahani?

Mtasubiri sana.

Upinzani mbovu

Kwanini utumie dola na kuvunja katiba kuwazuia wasifanye siasa?

Come again?

Ain’t no fool here!
 
Magufuli ametamka tu maneno ya kuzuia mikutano ya kisiasa, ila katika uhalisia wa swala lenyewe, waliozuia mikutano hiyo ni wanasiasa kutoka upinzani, siyo Magufuli!
 
Wakenya hawa hawa nilio nao hapa ndio wanajadili hayo unayoyasema? Kwamba kila kitu kimesimama, uchumi umeharibika kisa tunamjadili nani awe rais? MaCCM mumeishiwa kweli, hehehe yaani poleni.
 
Lugha ya kifasihi hiyo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata bunge kutokuwa live mnaogopa nini mkuu? Kazi za gizani huwa ni shetani na watenda maovu ili wasidhihirike!

Ni assume nakubaliana na wewe kwenye swala la siasa, je, vp kuhusu katiba mpya? na tume huru ya uchaguzi nako ina issue gani?
 
Katazo lipo kwa vyama vya siasa tu, ila mwenyewe, Bashiru na Pole Pole kila siku wanafanya mikutano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katazo lipo kwa vyama vya siasa tu, ila mwenyewe, Bashiru na Pole Pole kila siku wanafanya mikutano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…