Kwa nini Ben Saanane asikamatwe?

Kwa nini Ben Saanane asikamatwe?

CosaNostra

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
382
Reaction score
139
Mambo ya uongo na uzushi huwa ni hatari sana, nchi nyingi zimeingia katika mapigano na mifarakano kwa ajili ya uongo wa watu wachache.

Ben - verified user hapa JF ameshiriki ku-publisize uongo kuwa eti mkuu wa majeshi (CDF) Gen . Davis Mwamunyange amedhuriwa na serikali inaficha taarifa zake.

Alifika mbali na kuipa serikali siku saba CDF aonekane hadharani. Bahati nzuri kutokana na kazi za kawaida, CDF akawepo katika media hii majuzi.

Sasa huyu Ben, anayefahamika na kutambulika anachukuliwa hatua gani? Sababu kesho atasema ooh, Kamishna wa TRA amedhurika, alikataa kupitisha mizigo fulani.... siku ingine Oooh, Mkuu wa uhamiaji amefanyiwa hiki au kile , na kadhalika.

Hawa ndio watu wanaotuletea tetesi zisizo na chembe ya ukweli na kisha kung'ang'ania kuwa ni kweli. Sometimes tetesi huwa zipo na huhojiwa zithibitishwe, lakini kung'ang'ania tetesi na kuzifanya ni ukweli inapasa tujue alikuwa na lengo gani? Nasema kwa nini Ben asihojiwe?
 
Mwacheni mwana Rombo na yeye anaroho, kukosea ni kwa kila mwanadamu.
 
Kama vipi mkamate tu! Usingoje polisi
 
Wewe jamaa ni kiazi sana na hujui sheria hata moja. Ben hajaziaha na aliuliza kwa mujibu wa sheria. Usidhani kuwa polisi wa Tanzania ni vihiyo. Ndio maana aliyesema kuwa CDF kalishwa sumu alikamatwa ila ben hajakamatwa kwa sababu yeye aliuliza kuhusu alipo Davis na wala hajazusha kitu.
Usiweke akili yako mfukoni.
I am sure wewe ni ccm 100% magufulika wazee wa kukurupuka.
 
Mi nakushauli hayo maoni yako uyapeleke polisi sio kutuuliza hapa JF
 
kukamatwa ni mpaka ushauri? sheria ziko wazi kama kuna jambo baya....
 
Mambo ya uongo na uzushi huwa ni hatari sana, nchi nyingi zimeingia katika mapigano na mifarakano kwa ajili ya uongo wa watu wachache.

Ben - verified user hapa JF ameshiriki ku-publisize uongo kuwa eti mkuu wa majeshi (CDF) Gen . Davis Mwamunyange amedhuriwa na serikali inaficha taarifa zake.

Alifika mbali na kuipa serikali siku saba CDF aonekane hadharani. Bahati nzuri kutokana na kazi za kawaida, CDF akawepo katika media hii majuzi.

Sasa huyu Ben, anayefahamika na kutambulika anachukuliwa hatua gani? Sababu kesho atasema ooh, Kamishna wa TRA amedhurika, alikataa kupitisha mizigo fulani.... siku ingine Oooh, Mkuu wa uhamiaji amefanyiwa hiki au kile , na kadhalika.

Hawa ndio watu wanaotuletea tetesi zisizo na chembe ya ukweli na kisha kung'ang'ania kuwa ni kweli. Sometimes tetesi huwa zipo na huhojiwa zithibitishwe, lakini kung'ang'ania tetesi na kuzifanya ni ukweli inapasa tujue alikuwa na lengo gani? Nasema kwa nini Ben asihojiwe?
CosaNostra wewe umejificha kwa ID yako kama mimi, halafu wataka verified user akamatwe kwa mawazo aliyoongea bila kujificha. Bahati mbaya sikuona Ben Saanane akiandika hayo unayodai. Aliomba Mwamunyange ajitokeze. Watu kama Ben Saanane wanastahili heshima, maana wamethubutu kuuliza vitu ambavyo mimi na wewe twaona uoga kuuliza.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, omba radhi kwa utumbo uliotundika hapa jamvini. Kama hukuelewa ungeuliza
 
Ben kijana mdogo wala sura haijaharibiwa na mabom mimi nadahan utoto pia unamsumbua maana hata ukitaka kukamaliza ni sec chache ajuwi wala rule zakujilinda
 
Mwacheni mwana Rombo na yeye anaroho, kukosea ni kwa kila mwanadamu.
Aje aombe msamaha jukwaani. Mi binafsi naichukia tabia ya uongo maana hata rwanda na burudi walianza kuwa na watu kama ben
 
CosaNostra wewe umejificha kwa ID yako kama mimi, halafu wataka verified user akamatwe kwa mawazo aliyoongea bila kujificha. Bahati mbaya sikuona Ben Saanane akiandika hayo unayodai. Aliomba Mwamunyange ajitokeze. Watu kama Ben Saanane wanastahili heshima, maana wamethubutu kuuliza vitu ambavyo mimi na wewe twaona uoga kuuliza.

Ozzie, tatizo linakuja pale mtu anapokurupuka na kutoa taarifa za uongo ambazo zinaweza kuhatarisha amani, Suppose vijana wangeingia mitaani kudai CDF amedhuriwa, wakafanya fujo na kuumiza watu, nani ni msababishaji?
 
Back
Top Bottom