MBOKA NA BISO
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 766
- 792
Kuna sababu kadhaa kaka, na mtu anaweza kuandika makala nzima kueleza kwa nini DRC, licha ya kuwa na ukanda wake wa pwani ya Atlantiki, inategemea kwa kiasi kikubwa Bandari ya Dar kusafirisha bidhaa zake. Nitajitahidi kufupisha kadri ya uelewa wangu mdogo 😂.
Kwanza, DRC ni nchi kubwa mno, yenye eneo linalokaribia ukubwa wa Ulaya Magharibi. Kutoka Kongo Central Province, ambako nchi hiyo inakutana na Bahari ya Atlantiki, hadi eneo lenye utajiri mkubwa wa madini la kusini mashariki, linalojulikana kama Katanga na sehemu ya Copperbelt, ni umbali wa takribani kilomita 2,500. Kwa upande mwingine, umbali wa barabara kutoka Dar es Salaam hadi Lubumbashi, kitovu muhimu cha shughuli za uchimbaji madini katika eneo hilo, ni takribani kilomita 1,846.
Unaweza kujiuliza, kwani tofauti ya kilomita 700 ni kubwa kiasi hicho ukizingatia umuhimu wa bandari?Lakini hapa ndipo hoja ya msingi ilipo, kuwa na pwani na bandari ni jambo moja, kuwa na miundombinu inayowezesha kusafirisha mizigo kutoka ndani ya nchi hadi bandari hiyo kwa gharama nafuu ni jambo jingine kabisa.
Changamoto kubwa ni miundombinu na jiografia.
Kusafirisha madini kutoka eneo la Copperbelt hadi pwani ya Atlantiki kunakabiliwa na changamoto kubwa za miundombinu, ikiwemo misitu minene ya kitropiki, maeneo yenye barabara mbovu na ukosefu wa mtandao wa kutosha wa barabara kuu na reli unaounganisha mashariki na magharibi mwa nchi. Kwa hiyo, hata kama njia ya magharibi inaonekana kuwa na mantiki kwenye ramani, kiuhalisia inaweza kuwa ndefu zaidi, ghali zaidi na yenye changamoto nyingi za kiutendaji.
Mtu anaweza kuuliza tena, kwa nini wasitumie mfumo wa mito unaopita katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo?
Ni kweli kwamba DRC ina mtandao mkubwa wa mito, lakini si kila mto unaweza kutumika kusafirisha mizigo kutoka eneo moja hadi jingine. Kina cha maji, maporomoko, kasi ya mkondo na ukosefu wa miundombinu inayounganisha njia hizo na maeneo ya migodi ni miongoni mwa changamoto zinazopunguza matumizi yake.
Kwa mfano, Mto Kongo una maporomoko na mikondo yenye kasi kubwa katika eneo la Livingstone Falls, chini ya Kinshasa kuelekea baharini. Sehemu hizo hazipitiki kwa urahisi kwa meli za mizigo. Hivyo, huwezi kutegemea kusafirisha madini kutoka maeneo ya migodi ya kusini mashariki hadi Atlantiki kwa kutumia mto pekee; kutakuwa na haja ya kutumia njia nyingine za usafirishaji na miundombinu ya ziada. Hapo ni bila kuzingatia kuwa vina vya maji ya mito nchini Kongo ni ndogo hivyo haziwezi pitisha meli kubwa za kisasa za mizigo.
Umbali wa barabara kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Lubumbashi ni takribani kilomita 1,846 kupitia Zambia. Ingawa huu pia ni umbali mrefu, njia hii inanufaika na mtandao wa barabara na huduma za usafirishaji zilizopo katika ukanda huo.
Ndiyo maana, kwa sehemu ya biashara ya madini ya DRC, njia ya kuelekea mashariki kupitia Zambia na Tanzania imekuwa na umuhimu mkubwa kuliko kutegemea njia ya Atlantiki ambayo ina changamoto za miundombinu ya ndani.
Na isitoshe, Tanzania inaendelea kuwekeza katika miundombinu inayoweza kuimarisha zaidi uhusiano huu wa kibiashara.
Kwa mfano, Serikali inawekeza $ 2.9B ya ujenzi wa SGR sehemu ya Tabora–Kigoma yenye urefu wa takribani kilomita 506. Kigoma ni mji muhimu wa bandari katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, unaoweza kuwa kiungo cha usafirishaji kuelekea nchi za eneo la Maziwa Makuu.
Reli hii ikikamilika na kuunganishwa ipasavyo na miundombinu ya usafirishaji kuelekea DRC, itapunguza muda wa kusafirisha mizigo kutoka Dar hadi mpaka mwa DRC kutoka masaa 20 hadi 8 na kupunguza kwa maelfu ya dola gharama za usafirishaji..
Wakati huohuo, DRC inajenga Bandari ya maji marefu ya Banana katika pwani yake ya Atlantiki. Mradi huo unaweza kuipa nchi hiyo uwezo wa kupokea meli kubwa na kuimarisha biashara yake ya moja kwa moja na masoko ya kimataifa.
Lakini hata bandari hiyo ikikamilika, bado kutakuwa na swali muhimu, mizigo itatoka vipi katika maeneo ya migodi ya mashariki na kusini mashariki mwa DRC hadi Banana kwa gharama nafuu na muda wa kueleweka ?
Bandari inaweza kutatua changamoto ya kupokea na kupakia mizigo baharini, lakini haiwezi peke yake kutatua changamoto ya kuunganisha maeneo ya uzalishaji na soko. Hilo linahitaji pia barabara, reli, vituo vya mizigo na mifumo bora ya usafirishaji wa ndani.
Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu, Tanzania ina nafasi muhimu ya kuendelea kuwa lango la biashara kwa sehemu ya DRC, hasa katika maeneo yanayoweza kuhudumiwa kwa ufanisi zaidi kupitia ukanda wa mashariki. Hata hivyo, nafasi hiyo itategemea pia Tanzania kuendelea kuboresha bandari, reli, barabara, huduma za forodha na ushindani wa gharama za usafirishaji.
Haya nimeyaandika kwa ufupi na kwa uelewa wangu mdogo. Huenda wenye utaalamu zaidi wakaongezea au kusahihisha baadhi ya hoja