Kwa nini fangasi ukubwani?

Kwa nini fangasi ukubwani?

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
59,415
Reaction score
119,473
Hi doctors....
Hili swali huwa najiuliza nakosa jibu. Nilipokuwa mdogo (shule ya msingi na sekondari) fangasi nilikuwa nazisikia tu na kuzisoma kwenye vipeperushi....nimekuja kukutana na fangas nilipoingia chuo huku Dar. Nashidwa kuelewa kwa sababu kama ni suala la kushea vyoo na mabafu mbona tulikuwa tunashea tangu zamani? Tena life style ya sekondari ndo hatari zaidi(kwa wenzangu na mimi wa st. Kayumba) maana kama ni kushea vifaa vya kuogea mf.ndoo na sabuni hilo wala sio la kuuliza. Inaweza ikatokea kila siku unaogea ndoo tofauti na huna sababu ya kujiuliza ni ya nani......mlundikano wa maliwatoni ndio balaa kabisa......
Sasa iweje huku ambako kuna ustaarabu umeongezeka magonjwa ndo yanaibuka? Yan najikuta nalazimika kuwa extra careful wakati siku za nyuma nilikuwa naishi kawaida tu na hayakuwepo mambo kama haya.
Ni hali ya hewa?
Ni aina ya maji?
Ni mabadiliko ya kimwili?
Ni nini hasa? Maana hili jambo sio kwangu tu....wengi wanadai hivyo. Mwenye scientific explanation naomba anisaidie tafadhali...
Natanguliza shukrani....
 
Yaani Khantwe doctor unamsalimia 'hi'??????
 
Last edited by a moderator:
Watoto wa kike wapo vulnerable sana na fungus kuliko watoto wa kiume cha msingi kuwa makini sana na vitu vya kushare maliwatoni,ukienda maliwatoni kabla ya kutumia mwaga kwanza maji ya kutosha,na ukimaliza jiswafi na maji mengi then jikaushe kwa taulo lililo safi na kavu,ukishamaliza lianike taulo juani likauke.
 
Asante mkuu kwa ushauri
 
Umenikumbusha enzi zangu za kuoga ziwani unakuta robo tatu ya wanafunzi tupo ziwani tunaoga hadi raha
 
Hi doctors....
Hili swali huwa najiuliza nakosa jibu. Nilipokuwa mdogo (shule ya msingi na sekondari) fangasi nilikuwa nazisikia tu na kuzisoma kwenye vipeperushi....nimekuja kukutana na fangas nilipoingia chuo huku Dar. Nashidwa kuelewa kwa sababu kama ni suala la kushea vyoo na mabafu mbona tulikuwa tunashea tangu zamani? Tena life style ya sekondari ndo hatari zaidi(kwa wenzangu na mimi wa st. Kayumba) maana kama ni kushea vifaa vya kuogea mf.ndoo na sabuni hilo wala sio la kuuliza. Inaweza ikatokea kila siku unaogea ndoo tofauti na huna sababu ya kujiuliza ni ya nani......mlundikano wa maliwatoni ndio balaa kabisa......
Sasa iweje huku ambako kuna ustaarabu umeongezeka magonjwa ndo yanaibuka? Yan najikuta nalazimika kuwa extra careful wakati siku za nyuma nilikuwa naishi kawaida tu na hayakuwepo mambo kama haya.
Ni hali ya hewa?
Ni aina ya maji?
Ni mabadiliko ya kimwili?
Ni nini hasa? Maana hili jambo sio kwangu tu....wengi wanadai hivyo. Mwenye scientific explanation naomba anisaidie tafadhali...
Natanguliza shukrani....

Fangasi na madhara yake kwenye ngozi

· Tunapozungumzia maradhi ya fangasi, wengi wetu hatujisikii vizuri kabisa, yaani kwa kifupi hili somo si kipenzi cha wengi wetu.
·
Fangasi ni nini

· Fangasi imetokea kuwa na madhara makubwa kwenye ngozi zetu hasa wakazi wa maeneo yenye joto kwa sababu za kijiografia zaidi na namna ambavyo hali ya hewa inasaidia vimelea hivi kushamiri.

· Tunapozungumzia maradhi ya fangasi, wengi wetu hatujisikii vizuri kabisa, yaani kwa kifupi hili somo si kipenzi cha wengi wetu.
· Hii inatokana na jinsi maradhi haya yanavyojionyesha. Mara nyingi maradhi haya hutokea kwenye sehemu ambazo ni aibu kuzizungumzia au kuzionyesha hadharani.

· Bahati nzuri ni kuwa wala hatutakiwi tuone aibu kuzungumzia magonjwa haya kwani wengi wetu wanapata maradhi haya. Inasemekana kuwa katika Tanzania mtu mmoja kati ya watano hupata maradhi ya fangasi zaidi ya mara moja katika kipindi cha maisha yake.

· Ingawa wengi wetu tunaona vibaya kuzungumzia maradhi ya fangasi, viumbe hawa wanafurahisha ukivisoma na kuvifahamu vizuri.
· Zamani, kabla sayansi haijaendelea, wanasayansi walidhani fangasi ni mimea, lakini baada ya maendeleo ya kisayansi na maendeleo ya vifaa vya uchunguzi, fangasi ilikuja kutolewa kwenye kundi la mimea baada ya kugundulika kuwa fangasi wanakosa vigezo vya kuwekwa kwenye kundi moja na mimea mingine.

· Fangasi wapo wa aina nyingi, lakini kwenye makala zetu za kuangalia wale fangasi wanaoleta madhara ya kwenye ngozi na tutaangalia fangasi ambao maisha yao yote wanaishi kwenye ngozi wakiitegemea hiyo tu ili waweze kuishi.

· Vimelea hivi vya fangasi vinavyokaa kwenye ngozi viko vya aina mbili tofauti ambavyo ni dematofaiti (dermatophytes) na hamira (yeast).

· Kama ulikuwa hufahamu, basi leo ufahamu kuwa hamira ni fangasi. Fangasi huishi kwenye ngozi kwani hutegemea protini inayopatikana kwenye ngozi ambayo huitwa keratini (keratin).

· Keratini ni protini muhimua kwenye ngozi na inatengeneza asilimia kubwa ya ngozi pamoja na kucha na nywele ambako kama umeshagundua mpaka sasa ni sehemu ambazo fangasi huwa wanashambulia pia.

· Ukiunganisha hivi viwili, yaani protini ya keratini na hali ya hewa ya joto kama maeneo mengi ya Tanzania ukachukua na sababu ya tatu ya uwepo wa hali ya unyevu unyevu, basi utagundua ni kwa nini WaTanzania wengi wanapata mashambulizi ya vimelea hivi aina ya fangasi.

· Kwa hali ya kawaida, fangasi wa aina hii huwa hawana madhara sana zaidi huweka makazi yao tu kwenye ngozi bila kusababisha hali yoyote ya madhara kwenye ngozi. Madhara ya vimelea hivi huonekana baada idadi ya vimelea hivi kuongezeka kwenye eneo dogo la ngozi.
· Maradhi ya fangasi huambukizwa, hivyo ni rahisi kwa maradhi haya kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama wanashirikiana mavazi na vifaa vingine vya usafi wa mwili.

· Fangasi huathiri vipi ngozi
· Vimelea vya fangasi huathiri ngozi moja kwa moja kwa kuvamia na kutafuna keratini ambayo ni protini muhimu ya ngozi ikiwa inatengeneza sehemu kubwa ya ngozi, kucha na nywele.

· Aina za maradhi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi

· Kuna aina tofauti za maradhi ya ngozi yanayosababishwa na fangasi na hayo yote yameganwanywa kwenye makundi mawili.

· 1. Maradhi yaletwayo na dematofaiti (dermatophyte)

· 2. Maradhi yaletwayo na hamira (yeast)
 
Back
Top Bottom