Isenye
JF-Expert Member
- Dec 22, 2024
- 1,985
- 5,167
Maswali ya "kivipi","ilikuaje",iliwezekanaje" na "je,tutafika?" yatajibika kwa taabu na mahangaiko sana.Dah!kuna mmoja alianza kufuga kuku kwa kuokota manyoya
Hahahaaaa inabidi kuwafatilia.kuna mmoja alianza kufuga kuku kwa kuokota manyoya
Wakati umeilazimisha akili yako iitazame punje moja ilivyoleta tija na fanaka kwake mtoa hoja,yeye anapepea mbele na kukuletea kiroja kingine kilicho kichangamfu zaidi.Mwingine eti alianzisha kiwanda cha Mchele kwa kuanza na punje moja ya mchele
Kumchanganya,kumvuta,kumpa njia nyepesi kwa yasiyowezekana,kumlaghai na kumfanya mpokea taarifa akabidhi ubongo wake kwa muongeaji na kumuendesha kimwanasesere/voodoo styles ili hatimaye apigwe PESA kiulaini bila maswali.Sasa lengo lao huwa ni nini haswa?