Hii ni kampeni maalumu ya kundi maalumu lililotumika kumhujumu Dkt Magufuli kwa kuaminisha anatuma watu watekwe na kuuawa. Dkt Samia alipoapa na kuw Rais, na yeye akashadadia kusema Dkt Magufuli alikuwa anateka na kuua watu kwa kauli yake ya viroba. Bila kujua kuwa ule ulikua mpango maalumu wa kuharibu taswira ya rais Dkt Magufuli basi Dkt Samia nayeye akawa kwenye kundi la wazushi na watu wakaamini kweli Dkt Magufuli kama rais alituma watu wauawe. Kama mamlaka ya Rais ilituhumiwa na Makamu wa Rais ambaye alikuja kuwa Rais, ni ngumu sana kuuaminisha umma wa Watanzania kwa sasa kuwa Dkt Samia ni msafi. Umma wa watanzania wanaamini ni hiyo hiyo mamlaka ya Rais ambayo Dkt Samia ndiye rais inaagizia watu wakamatwe na kuuawa na hivyo Dkt Samia ni Muuaji ana ratibh utekaji wa watu na kufa na sababu kubwa ni yeye kukiri kumsagia kunguni bosi wake Dkt Magufuli kuhusu watu kuuawa kwenye awamu ya 5. Ila ukweli ni kwamba haya matukio yamekuwapo enzi na enzi ila vyombo vya habari vinayakuza na kuandika mwelekeo wa kusema polisi, serikali etc, ila ukweli hata kwa Dkt Magufuli alisingiziwa mengi ndiyo maana mpaka sasa hata Dkt Samia anaumbuka na anazidi kuumbumbuka na kudhalilika kwa kauli zake za kumsagia kunguni Dkt Magufuli. Muda anao anaweza omba msahama.