Kwa nini Kanda ya Ziwa ina Kiwango kikubwa cha Ugonjwa wa Cancer kuliko Maeneo mengine?

Kwa nini Kanda ya Ziwa ina Kiwango kikubwa cha Ugonjwa wa Cancer kuliko Maeneo mengine?

Kinyungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
19,484
Reaction score
38,416
Wakuu hili swali nauliza kwa wema kabisa.

Kuna kiwango kukubwa cha wagonjwa wa Cancer kwa upande wa kando kando ya Ziwa Victoria kuliko maeneo mengine nchini.

Mtakumbuka hata Mama Samia alieleza nia ya Serikali kujenga kituo kikubwa Mwanza chenye kutoa matibabu ya Cancer
Sasa najiuliza:

1. Kwa nini kanda hii inaandamwa sana na Cancer?

2. Kitu gani wananchi wafanye kujiepusha na cancer.

3. Je Serikali ifanye nini kupunguza tatizo la cancer nchini na hasa kwa kanda ya Ziwa?

Nawakaribisha wenye mawazo na nia njema na wenye kuguswa na hili tatizo tupeane mawazo wakuu ili kupunguza hili tatizo
 
Hiyo hospitali kubwa ikijengwa itasaidia kwa kiasi fulani kupunguza

Nafikiri mazingira muda mwingine yanachangia hiyo hali
 
Kanda ya ziwa kitoweo kikuu ni samaki kutoka ziwa Victoria, samaki wanavuliwa kwa sumu baada ya serkali kukataza nyavu zile zinazovua had I viluilui, pia uvuvi wa baruti unaharibu samaki kwa kuwachanachaba, so sumu NFO hupekekea cancer
 
Sioni mtu akitoa wazo kuwe na tume ya muda maalumu ya watafiti watakao kwenda kutafiti sababu na visababishi vya hiyo cancer wakazi wa huko pahala.

Tukikaa kimya ndugu zetu watakufa na kudhurika kwa wingi. Uchunguzi ufanyie na report ziwe published. Mfano lile tukio la juzi la samaki kufa sijasikia ripoti yake ya ukweli zaidi ya wale matapeli kusema ni mafuta sijui tope sijui mikojo ya ng'ombe.

Hawa wahusika wa ile kamati wanatakiwa kutafutwa na kuwekwa ndani kama wauwaji.

Na ule mgodi ufungwe mara moja na kulipa fidia kwa serikali , na raia wa eneo lile.

Na waziri husika naona wizara inamshinda.
 
Nipo kwenye utafiti usio rasmi pia kuhusu uhusiano wa mikoa inayokula ndizi na ugonjwa wa kisukari.

Kagera na Kilimanjaro kuna wagonjwa wengi wa kisukari

Japo utafititi wa awali unaonyesha niyo mikoa wanakula vizuri na hawafanyi kazi ngumu za kuwatoa jasho.

Kisukari ni mojawapo ya lifestyle diseases

Migomba ni permanent crops ukipanda umepanda ,hakuna surba za shamba kivile.
 
Samaki na maji yanayotumika majumbani.

Wachafuzi wa maji ya ziwa Victoria wanaangamiza wenzao
 
Kanda hii imezungukwa na migodi mingi na bahati mbaya wachimbaji wadogowadogo wanatumia Chemikali hatarishi kama zebaki ambapo katika uoshaji wa dhahabu hutiririsha maji yenye mchanganyiko wa kemikali/Contaminants kwenye mikondo ya maji pia tahadhari ni ndogo kwa watumiaji wa hizo kumikali.

Pia hii kanda kuna matumizi makubwa sana ya viuatilifu kwenye mashamba ya pamba na mazao ya bustani na tahadhali ni ndogo kwa watumiaji.

Ninamfano mmoja wakulima wa bustani huwa wana tabia moja isiyofaa ya kupiga dawa nyanya na kupeleka sokoni kesho ya yake ili isioze.

Wito kwa Sereilikali tunaomba ifanye jitihada za kiutafiti wa kubaini tatizo
 
Hiyo hospitali kubwa ikijengwa itasaidia kwa kiasi fulani kupunguza

Nafikiri mazingira muda mwingine yanachangia hiyo hali
Hospitali itapunguzaje tatizo wakati mfumo wetu wa afya upo kusubiri kutibu wagonjwa?

Suala hapa ni wataalamu wa afya watoke mahospitalini wakatafute chanzo hasa kisababishi cha hizo kansa sio kusubiri wagonjwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom