Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwakweli hivi ni moja ya visababishi vikubwa vya kansa maeneo ya kanda ya ziwa.Kanda hii imezungukwa na migodi mingi na bahati mbaya wachimbaji wadogowadogo wanatumia Chemikali hatarishi kama zebaki ambapo katika uoshaji wa dhahabu hutiririsha maji yenye mchanganyiko wa kemikali/Contaminants kwenye mikondo ya maji pia tahadhari ni ndogo kwa watumiaji wa hizo kumikali
Pia hii kanda kuna matumizi makubwa sana ya viuatilifu kwenye mashamba ya pamba na mazao ya bustani na tahadhali ni ndogo kwa watumiaji
Ninamfano mmoja wakulima wa bustani huwa wana tabia moja isiyofaa ya kupiga dawa nyanya na kupeleka sokoni kesho ya yake ili isioze
Wito kwa Sereilikali tunaomba ifanye jitihada za kiutafiti wa kubaini tatizo
Sio kwa kiwango sawa na kanda ya ziwa..kwamfano kigoma wanakula sana samaki wanao patikana ziwa Tanganyika..tukija pwani wanakula sana samaki wanao vuliwa baharini kuliko hao wa kanda ya ziwa.Naona wengi wanataja samaki. Lakini samaki hao hao wanaoliwa Kanda ya ziwa, wanaliwa pia nchi nzima
Nakubaliana na wewe mkuu, wakati watafiti wanafanya utafiti ni vizuri pia na hospitali zijengwe kusaidia wagonjwaHospitali itapunguzaje tatizo wakati mfumo wetu wa afya upo kusubiri kutibu wagonjwa?
Suala hapa ni wataalamu wa afya watoke mahospitalini wakatafute chanzo hasa kisababishi cha hizo kansa sio kusubiri wagonjwa.
#MaendeleoHayanaChama
Wakuu hili swali nauliza kwa wema kabisa. Kuna kiwango kukubwa cha wagonjwa wa Cancer kwa upande wa kando kando ya Ziwa Victoria kuliko maeneo mengine nchini. Mtakumbuka hata Mama Samia alieleza nia ya Serikali kujenga kituo kikubwa Mwanza chenye kutoa matibabu ya Cancer
Sasa najiuliza:
1. Kwa nini kanda hii inaandamwa sana na Cancer?
2. Kitu gani wananchi wafanye kujiepusha na cancer
3. Je Serikali ifanye nini kupunguza tatizo la cancer nchini na hasa kwa kanda ya Ziwa?
Nawakaribisha wenye mawazo na nia njema na wenye kuguswa na hili tatizo tupeane mawazo wakuu ili kupunguza hili tatizo
Nchi zima ipi mkuu,huku nilipo ni ugali maharage tuNaona wengi wanataja samaki. Lakini samaki hao hao wanaoliwa Kanda ya ziwa, wanaliwa pia nchi nzima
Shida mfumo wa afya upo kusubiri watu waugue ili iwatibu na wala sio kupambana kuilinda jamii dhidi ya haya matatizo ya kiafya.Kulingana na matatizo ya kansa, mara nyingi kila kansa ina visababishi vyake. Na ukiangalia hili linatokana na muunhaniko wa kansa aina tofauti nfani ya jamii husika.
Kwa mfano:
1: Kansa ya kibofu cha mkojo vs ini: kuna aina ya konokono walioko kwenye ziwa Victoria, ambao ni sehemu ya mzunguko wa minyoo isababishayo kichocho. Hii baadaye inakuja kusababisha kansa ya kibofu cha mkojo.
Matumizi ya maji ya ziwa bila kuchemsha: kunywa vs kuogelea.
2: Kansa ya kizazi
A: Human papilloma virus
B: Wake wengi/patners
C: Ndoa za mapema/umri mdogo
D: Kuzaa watoto wengi etc.
3: Kansa ya njia ya chakula
A: Namba moja hapo juu
B: Viwanda na mazao yake
C: Viwanda na taka zake
D: Matumizi ya mbolea ya chumvichumvi/mbolea za viwandani kwenye kilimo, ambayo baadaye huenda kwenye vyanzo vya maji
4: Kansa ya koo
A: Migodi na vumbi lake lililo na chemikali.
B: Matumizi ya dawa za kuua wadudu kwenye pamba
Ili kupata suluhisho, inabidi kuvunja chain/mzunguko kulingana na kila kisababishi.
Si kuna mbunge alishawahi kusema bungeni wazazi wake wote wamekufa na cancer wakati ile ripoti ya samaki kukutwa wamekufa kwa hyo chanzo kikubwa akasema ni ziwa Victoria ile migodi ina discharge maji yenye heavy metal halafu ile report ikaingiliwa na wanasiasa mpaka Leo ukweli haujulikani ila migodi ndo chanzo.Sioni mtu akitoa wazo kuwe na tume ya muda maalumu ya watafiti watakao kwenda kutafiti sababu na visababishi vya hiyo cancer wakazi wa huko pahala.
Tukikaa kimya ndugu zetu watakufa na kudhurika kwa wingi. Uchunguzi ufanyie na report ziwe published. Mfano lile tukio la juzi la samaki kufa sijasikia ripoti yake ya ukweli zaidi ya wale matapeli kusema ni mafuta sijui tope sijui mikojo ya ng'ombe.
Hawa wahusika wa ile kamati wanatakiwa kutafutwa na kuwekwa ndani kama wauwaji.
Na ule mgodi ufungwe mara moja na kulipa fidia kwa serikali , na raia wa eneo lile.
Na waziri husika naona wizara inamshinda.
KANSAWakuu hili swali nauliza kwa wema kabisa.
Kuna kiwango kukubwa cha wagonjwa wa Cancer kwa upande wa kando kando ya Ziwa Victoria kuliko maeneo mengine nchini.
Mtakumbuka hata Mama Samia alieleza nia ya Serikali kujenga kituo kikubwa Mwanza chenye kutoa matibabu ya Cancer
Sasa najiuliza:
1. Kwa nini kanda hii inaandamwa sana na Cancer?
2. Kitu gani wananchi wafanye kujiepusha na cancer.
3. Je Serikali ifanye nini kupunguza tatizo la cancer nchini na hasa kwa kanda ya Ziwa?
Nawakaribisha wenye mawazo na nia njema na wenye kuguswa na hili tatizo tupeane mawazo wakuu ili kupunguza hili tatizo
Kwa kweli ni experience binafsi tu nimekutana na hizi case mara nyingi ni watu wa kutokea kanda hiyo. Pia kwa takwimu zilizopo inaonesha kuna ukubwa wa hili tatizo kwa wenzetu wa maeneo hayochanzo cha utafiti n nini mkuu? Au ni experience yako binafsi