Kwa nini Kenya ilihairisha kuivamia Tz kijeshi mwaka 1984??

Kwa nini Kenya ilihairisha kuivamia Tz kijeshi mwaka 1984??

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Wakuu kama mnakumbuka vizuri mwaka 1984 kulikua na vuguvugu kubwa sana la Kenya kuivamia kijeshi Tanzania.

Sababu kubwa ilikua ni mnyukano wa kugombea mali za JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI iliyovunjika mwaka 1978. Za kiintelijensia zinadai Kenya ilitaka kucheza rafu kubwa mno kwa kuchukua assets zote muhimu kitu ambacho mwalimu alipambana nacho mno.

Inadaiwa kuwa kuna baadhi ya mali kama meli na ndege kubwa kubwa ziliibwa na kufichwa Kenya, ikabidi Mwalimu atume vijana maalumu wa TISS ya wakati huo wakafanya yao, na baadhi ya mali zikatoroshwa kurudi Tanzania ikiwamo meli maarufu ya MV Victoria kitu ambacho wakenya kiliwaach midomo wazi.

Wakenya kwa kuwa na uchu wa mali hawakuwa na option zaidi ya kutaka kuivamia kijeshi Tanzania, na kama mnakumbuka mwaka 1984 Tanzania ilikua iko tayari tayari kwa vita nyingine na vuguvugu lilikua hot sana.

Ni nini kilipelekea Kenya wakaahirisha mkakati wao wa kuivamia Tanzania??

Walimwogopa Mwalimu ambaye alikua tayari kwa lolote pindi maslahi ya nchi yake yanapoguswa ikibidi hata kuingia vitani?
 
Duuh, mkuu hebu funguka zaidi, any source please?:A S 114:
 
wengi wao mkuu ndiyo kipindi hicho walichozaliwa sasa ngumu kuamini , ila kwa sisi wengine tulisikia hayo at that time
Mkuu tatizo vitu vingi sana hii nchi vinabaki kuwa siri za serikali wakati sheria ya classified information inadai miaka 30 ndio mwisho, inabidi mambo yamwagwe hadharani..

Mambo kama haya watawala wanabidi wayaweke kweupe yanasaidia sana kuongeza uzalendo hasa kwa kizazi hiki cha .com
 
Nilikua bado sijazaliwa lakini you can provide more sources tukajifunze zaidi
 
ndo kwanza nasikia kutoka kwako
ilikuwaje?
kuna baadhi ya mali tulibaki nazo zingine zikatoroshwa kama ndege nk
ndivo nlisikia.
Nlikuwa mdogo sana kuelewa kama kuna vita wala jumuia
 
Stori nzuri ukimpata anaeijua.!!
 
Wakuu kama mnakumbuka vizuri mwaka 1984 kulikua na vuguvugu kubwa sana la Kenya kuivamia kijeshi Tanzania.

Sababu kubwa ilikua ni mnyukano wa kugombea mali za JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI iliyovunjika mwaka 1978. Za kiintelijensia zinadai Kenya ilitaka kucheza rafu kubwa mno kwa kuchukua assets zote muhimu kitu ambacho mwalimu alipambana nacho mno.

Inadaiwa kuwa kuna baadhi ya mali kama meli na ndege kubwa kubwa ziliibwa na kufichwa Kenya, ikabidi Mwalimu atume vijana maalumu wa TISS ya wakati huo wakafanya yao, na baadhi ya mali zikatoroshwa kurudi Tanzania ikiwamo meli maarufu ya MV Victoria kitu ambacho wakenya kiliwaach midomo wazi.

Wakenya kwa kuwa na uchu wa mali hawakuwa na option zaidi ya kutaka kuivamia kijeshi Tanzania, na kama mnakumbuka mwaka 1984 Tanzania ilikua iko tayari tayari kwa vita nyingine na vuguvugu lilikua hot sana.

Ni nini kilipelekea Kenya wakaahirisha mkakati wao wa kuivamia Tanzania??

Walimwogopa Mwalimu ambaye alikua tayari kwa lolote pindi maslahi ya nchi yake yanapoguswa ikibidi hata kuingia vitani?

Unataarifa nzuri sana lakini umeshindwa kutujuza kwa undani zaidi, tunaomba utuwekee hapa Mkuuuuu
 
Mkuu tatizo vitu vingi sana hii nchi vinabaki kuwa siri za serikali wakati sheria ya classified information inadai miaka 30 ndio mwisho, inabidi mambo yamwagwe hadharani..

Mambo kama haya watawala wanabidi wayaweke kweupe yanasaidia sana kuongeza uzalendo hasa kwa kizazi hiki cha .com
Nionavyo mimi ni kuwa hizo sheria sio lazima ziwe applicable kwa kila nchi, kuna mambo mengine yakuiga lakini kuna mengine lazima uweke na ya kwako kulingana na mazingira yako, hiyo lifespan ya classified info inatumika zaidi na USA na hata hivyo sio kwakila kitu, na wanafanya hivyo kwasababu zao ikiwa ni pamoja kuwahadaa wajinga wengine nao waige. Nahisi hata nchi nyingine kubwa kama Russia, UK, China nk ni tofauti. AKILI ZA KUAMBIWA....CHANGANYA NA ZAKO. So far nadhani system yetu ipo vema sana na imefanya mengi makubwa yakuiepusha nchi na mambo mengi. Japo sisi wa tz tupo sawa na familia ya tajiri wanalala vema ila wakiamka asubuhi wanakazi yakumtukana na kumdhihaki mlinzi aliyekesha kuwalinda.
 
Mkuu nimeipenda sana hiyo kuna mzee niko nayehapa jirani nimemuuliza kanipa kiundani zaid.
 
nakumbuka nilikuwa darasa la 4 Arusha. baba lituaga akiwa kikosi 977 kj chekereni Arusha kuwa wanakwenda kulinda mipaka Namanga majeshi ya kenya yanavamia tz. Mama alikuwa akilia na hakula wiki nzima. Mh that year.
 
Mkuu nimeipenda sana hiyo kuna mzee niko nayehapa jirani nimemuuliza kanipa kiundani zaid.

Kwa kumbukumbu zangu kipindi kile kilikuwa kigumu sana kiuchumi katika nchi hii, tusingeweza kupigana vita vingine.

Hivyo vya Idi Amini tu vilitufungisha mikanda kwa miaka kadhaa badala ya miezi 18 tuliyoambiwa.
 
Nachoweza sema Hawa siku zote wamekua sio jirani zetu wazuri!

Ntuzu chukua like hiyo....Wakenya si watu wema kwetu kabisa. Wamejaa dharau, majigambo na kujitweza
 
Back
Top Bottom