Kipindi hicho nilikuwa na miaka miwili toka nitoke Vitani Uganda na nilikuwa Lugalo,ni kweli kulitokea sintofahamu kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya hivyo kufikia Serikali yetu kupeleka Majeshi yetu mpakani lakini hiyo ilikuwa ni Show of force tu ilikuwa tu kumuonyesha adui kuwa tuko vizuri kijeshi na tuko tayari kwa lolote pindi tukichokozwa.
Bahati nzuri sana Kenya walielea somo hawakuweza kuongeza msuguano uliokuwepo wakati huo na kufanya hali ya Tahadhali(Alert)kuondolewa,ki ukweli hata kama kungekuwa na Ulazima kupigana naamini serikali yetu ingeweza kutumia Diplomasia kumaliza fukuto hilo, sababu kubwa ni hali ya Uchumi wa nchi yetu kwa wakati huo pili jeshi letu wakati huo lilikuwa likijijenga upya(Re-Organisation)baada ya vita vya Kagera,maana Jeshini tulikua na watu engi toka sehemu mbali-mbali wengine walitoka Polisi wengine Magereza na pia tulikuwa na Wanamgambo ambao pia walichukuliwa katika JWTZ lakini wakati huo kulionekana si vizuri kuwa-ingiza Jeshini kama waajiriwa maana tungekuwa na Jeshi kubwa sana kiasi ambacho lingekuwa Mzigo kwa Taifa,Lakini kwa kudhamini mchango wao huko vitani Uganda wengine walihamishiwa kwenye majeshi yetu mengine ya Polisi na Magereza.
Mimi siamini kama Kenya ilitaka kuvamia nchi yetu 1984 ila najua kulikuwa na msuguano wa kisiasa kati ya nchi hizi mbili hivyo kupelekea mtafaruku mkubwa wa kijeshi kwenye mipaka.