mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,227
Mkuu, muongeze kiroba kingine bili kwangu.
Tatu Nyerere Hakuwa Muhuni Na Hajawahi Kutumia Njia Za Kihuni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, muongeze kiroba kingine bili kwangu.
Mkuu kama huna cha kuchangia kaa kimya, wapishe wenzio wamwage nondoI hate thread za kipuuzi kama hizi
Safi sana mkuu, angalau umetufungua macho.Kipindi hicho nilikuwa na miaka miwili toka nitoke Vitani Uganda na nilikuwa Lugalo,ni kweli kulitokea sintofahamu kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya hivyo kufikia Serikali yetu kupeleka Majeshi yetu mpakani lakini hiyo ilikuwa ni Show of force tu ilikuwa tu kumuonyesha adui kuwa tuko vizuri kijeshi na tuko tayari kwa lolote pindi tukichokozwa.
Bahati nzuri sana Kenya walielea somo hawakuweza kuongeza msuguano uliokuwepo wakati huo na kufanya hali ya Tahadhali(Alert)kuondolewa,ki ukweli hata kama kungekuwa na Ulazima kupigana naamini serikali yetu ingeweza kutumia Diplomasia kumaliza fukuto hilo, sababu kubwa ni hali ya Uchumi wa nchi yetu kwa wakati huo pili jeshi letu wakati huo lilikuwa likijijenga upya(Re-Organisation)baada ya vita vya Kagera,maana Jeshini tulikua na watu engi toka sehemu mbali-mbali wengine walitoka Polisi wengine Magereza na pia tulikuwa na Wanamgambo ambao pia walichukuliwa katika JWTZ lakini wakati huo kulionekana si vizuri kuwa-ingiza Jeshini kama waajiriwa maana tungekuwa na Jeshi kubwa sana kiasi ambacho lingekuwa Mzigo kwa Taifa,Lakini kwa kudhamini mchango wao huko vitani Uganda wengine walihamishiwa kwenye majeshi yetu mengine ya Polisi na Magereza.
Mimi siamini kama Kenya ilitaka kuvamia nchi yetu 1984 ila najua kulikuwa na msuguano wa kisiasa kati ya nchi hizi mbili hivyo kupelekea mtafaruku mkubwa wa kijeshi kwenye mipaka.
Kweli kabisa mkuu nakuunga mkono.mkuu i partly agree with you, ila kuna nyingi hua zinaachiwa kama tetesi tu kumbe ndio zenyewe, siri zikiwa yingi sana nayo inakua tatizo, si vibaya watu kujifunza historia na kujenga uzalendo kupitia simulizi, Mfano mzuri ni yale aliyoyasema mkuu kule bondeni kwenye mziko ya madiba, kwa kiasi kikubwa imani ilejengeka kwenye mioyo ya wakazi wa jamhuri
Amin usiamini hiyo ilikuwa SHOW OF FORCE tu Jeshi kuwekwa kwenye hali ya Tahadhali wakati wa fukuto ni kawaida katika majeshi yote duniani hiyo isikutishe,kipindi hicho ilikuwa vigumu sana kupigana kwa sababu nilizozitaja,Jeshi letu lisingeweza kuingia vitani kabisa hata kama tungeingia vitani Dunia ingetushangaa kabisa,isitoshe tuna wataalamu wazuri wa kijeshi wasingeruhusu Jeshi letu liingie vitani maana kufanya hivyo ni sawa na kujitoa MHANGA.Safi sana mkuu, angalau umetufungua macho.
Kwa hiyo kimsingi ule urundikaji wa wanajeshi mpakani kule Namanga na sirari na maeneo mengine na silaha nzito nzito kule kilimanjaro ulikua kwa ajili ya show off tu ?
Maana kwa jinsi vijana walivyokua wanakula tizi mitaani ilikua ni vita kabisa ile, lakini pia mbona kama Rais alitangaza state of emergency wakati huo??
Sasa mkuu kwa nini Kenya waliamua kuufyata mkia huku wakijua kabisa ile ilikua ni show off tu?Amin usiamini hiyo ilikuwa SHOW OF FORCE tu kipindi hicho ilikuwa vigumu sana kupigana kwa sababu nilizozitaja,Jeshi letu lisingeweza kuingia vitani kabisa hata kama tungeingia vitani Dunia ingetushangaa kabisa,isitoshe tuna wataalamu wazuri wa kijeshi wasingeruhusu Jeshi letu liingie vitani maana kufanya hivyo ni sawa na kujitoa MHANGA.
Mimi sisemi kuwa Kenya ilifyata mkia bali pia aliona ugumu wa wao kuingia vitani kwa haraka haraka bila maandalizi na kwa kitu ambacho si cha mhimu kwa taifa,Ni vigumu sana kugundua hii ni SHOW OF FORCE au ni Real action maana vitendo vyake ni sawasawa kabisa isipokuwa umaliziaji ndiyo huwa tofauti,SHOW OF FORCE mnakuwa na kila kitu ni sawa na wewe unamwendea adui yako unafika mlangoni kwake ukiwa na Panga,Rungu,Nondo na zana zingine harafu unaongea maneno ya kumtisha na wewe kujisifia baadaye ukaondoka polepole bila kumdhuru wala kufanya chochote hiyo inaitwa SHOW OF FORCE kwa lugha rahisi ni kujionyesha mwenye nguvu dhidi ya adui yako,Na hii ni kawaida kwenye Majeshi mengi kukiwa na Fukuto fulani tu Majeshi yanatoka na kuanza Mazoezi ya kijeshi mpakani mwa nchi tuhumiwa au wengine wanafanya Maonyesho ya zana zao za Kivita na wanaita waandishi wa habari wote kuja kushuhudia wakijua habari hizo zitamfikia mlengwa wao hiyo ndiyo inaitwa SHOW OF FORCE aka MKWARASasa mkuu kwa nini Kenya waliamua kuufyata mkia huku wakijua kabisa ile ilikua ni show off tu?
Au intelligence yao ilikua weak kutokuweza kujua kuwa tulikua tunawachimba mkwara tu na hatukua na ubavu wa kupambana vita nyingine???
Mkuu nimeipenda sana hiyo kuna mzee niko nayehapa jirani nimemuuliza kanipa kiundani zaid.