Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
- Thread starter
-
- #21
Mkuu funguka kwa niaba yetu sote mkuu, historia ya nchi hii kuminywa inafanya wtu wapoteze uzalendo kwa taifa laoNihabari za kweli, mkiwapata wapiganaji wetu wa zamani watawasimulia haya.
Usiste kutumwagia hapa mkuu, tuna mengi sana ya kujifunza juu ya nchi hii japo yanafichwaMkuu nimeipenda sana hiyo kuna mzee niko nayehapa jirani nimemuuliza kanipa kiundani zaid.
Mkuu hebu jazilishia nyama mkuu, ilikuaje??nakumbuka nilikuwa darasa la 4 Arusha. baba lituaga akiwa kikosi 977 kj chekereni Arusha kuwa wanakwenda kulinda mipaka Namanga majeshi ya kenya yanavamia tz. Mama alikuwa akilia na hakula wiki nzima. Mh that year.
Wakuu kama mnakumbuka vizuri mwaka 1984 kulikua na vuguvugu kubwa sana la Kenya kuivamia kijeshi Tanzania.
Sababu kubwa ilikua ni mnyukano wa kugombea mali za JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI iliyovunjika mwaka 1978. Za kiintelijensia zinadai Kenya ilitaka kucheza rafu kubwa mno kwa kuchukua assets zote muhimu kitu ambacho mwalimu alipambana nacho mno.
Inadaiwa kuwa kuna baadhi ya mali kama meli na ndege kubwa kubwa ziliibwa na kufichwa Kenya, ikabidi Mwalimu atume vijana maalumu wa TISS ya wakati huo wakafanya yao, na baadhi ya mali zikatoroshwa kurudi Tanzania ikiwamo meli maarufu ya MV Victoria kitu ambacho wakenya kiliwaach midomo wazi.
Wakenya kwa kuwa na uchu wa mali hawakuwa na option zaidi ya kutaka kuivamia kijeshi Tanzania, na kama mnakumbuka mwaka 1984 Tanzania ilikua iko tayari tayari kwa vita nyingine na vuguvugu lilikua hot sana.
Ni nini kilipelekea Kenya wakaahirisha mkakati wao wa kuivamia Tanzania??
Walimwogopa Mwalimu ambaye alikua tayari kwa lolote pindi maslahi ya nchi yake yanapoguswa ikibidi hata kuingia vitani?
Kipindi hicho nilikuwa na miaka miwili toka nitoke Vitani Uganda na nilikuwa Lugalo,ni kweli kulitokea sintofahamu kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya hivyo kufikia Serikali yetu kupeleka Majeshi yetu mpakani lakini hiyo ilikuwa ni Show of force tu ilikuwa tu kumuonyesha adui kuwa tuko vizuri kijeshi na tuko tayari kwa lolote pindi tukichokozwa.
kipindihicho si ndicho cha uhujumu uchumi? hata ukikamatwa na chumvi unawekwa ndani. uchumiwetu ulikuwa vibaya tulinyimwa misaada kwa sababu ya kuivamia UGANDA. Nyelele akatumia njia ya kihuni kupata pesa. tungepigwa mbaya.huu ni ukweli japo mchungu
Mapolomoko
kwanza hakujawah kua na mtu anaeitwa NYELELE hapa tanzania..
pili sababu ya kunyimwa misaada ni baada ya nyerere kupinga masharti ya mkopo ya IMF na WB na sio kwasababu ya vita..
hadithi yako siyo sahihi sana. Kulikuwa na tension mpakani lakiniyo kwa sababu Kenya ilitaka kuvamia Tanzania ila ni kwa sababu Tanzania ilikuwa imefunga mpaka ule kusudi watalii wanaoingilia Kenya wasije kupumzikia Tanzania halafu malipo yaende Kenya. Wakati huo bado Tanzania ilikuwa na jeshi kali sana ambalo lingeweza kuismbaratisha nchi yoyote jirani, na Kenya walikuwa wanalijua hilo; kwa vile viongozi wa kKenya ni strategists sana, sidfhani kama kweli wengijiingiza kupigana na Tanzania ilihali wakijua wangevurugwa sana. Matatizo ya kijesi Tanzania nadhani kuharibika kuanzia muda huo huo lakini siyo kwa kasi kubwa vile ingawa sijui leo yakoje tena. Majuzi nilishangaa kusikia kuwa tunabadilishana ndege za zamani na China, yaani siyo kuwa tunanunua ndege za kisasa.
Ntuzu chukua like hiyo....Wakenya si watu wema kwetu kabisa. Wamejaa dharau, majigambo na kujitweza
Mkuu tatizo vitu vingi sana hii nchi vinabaki kuwa siri za serikali wakati sheria ya classified information inadai miaka 30 ndio mwisho, inabidi mambo yamwagwe hadharani..
Mambo kama haya watawala wanabidi wayaweke kweupe yanasaidia sana kuongeza uzalendo hasa kwa kizazi hiki cha .com
Sijakuelewa! Yaani China Ndo Wanatupa Mpya C Tunawapa Za Zamani au? if xo ni vzur kwani CHINA Taifa Kubwa Sasa.
Kipindi hicho nilikuwa na miaka miwili toka nitoke Vitani Uganda na nilikuwa Lugalo,ni kweli kulitokea sintofahamu kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya hivyo kufikia Serikali yetu kupeleka Majeshi yetu mpakani lakini hiyo ilikuwa ni Show of force tu ilikuwa tu kumuonyesha adui kuwa tuko vizuri kijeshi na tuko tayari kwa lolote pindi tukichokozwa.
Bahati nzuri sana Kenya walielea somo hawakuweza kuongeza msuguano uliokuwepo wakati huo na kufanya hali ya Tahadhali(Alert)kuondolewa,ki ukweli hata kama kungekuwa na Ulazima kupigana naamini serikali yetu ingeweza kutumia Diplomasia kumaliza fukuto hilo, sababu kubwa ni hali ya Uchumi wa nchi yetu kwa wakati huo pili jeshi letu wakati huo lilikuwa likijijenga upya(Re-Organisation)baada ya vita vya Kagera,maana Jeshini tulikua na watu engi toka sehemu mbali-mbali wengine walitoka Polisi wengine Magereza na pia tulikuwa na Wanamgambo ambao pia walichukuliwa katika JWTZ lakini wakati huo kulionekana si vizuri kuwa-ingiza Jeshini kama waajiriwa maana tungekuwa na Jeshi kubwa sana kiasi ambacho lingekuwa Mzigo kwa Taifa,Lakini kwa kudhamini mchango wao huko vitani Uganda wengine walihamishiwa kwenye majeshi yetu mengine ya Polisi na Magereza.
Mimi siamini kama Kenya ilitaka kuvamia nchi yetu 1984 ila najua kulikuwa na msuguano wa kisiasa kati ya nchi hizi mbili hivyo kupelekea mtafaruku mkubwa wa kijeshi kwenye mipaka.