Kwa nini Kenya ilihairisha kuivamia Tz kijeshi mwaka 1984??

Safi sana mkuu, angalau umetufungua macho.

Kwa hiyo kimsingi ule urundikaji wa wanajeshi mpakani kule Namanga na sirari na maeneo mengine na silaha nzito nzito kule kilimanjaro ulikua kwa ajili ya show off tu ?

Maana kwa jinsi vijana walivyokua wanakula tizi mitaani ilikua ni vita kabisa ile, lakini pia mbona kama Rais alitangaza state of emergency wakati huo??
 
Kweli kabisa mkuu nakuunga mkono.

Vizazi vibakuja vizazi vinapita, leo kijana aliyezaliwa miaka ya 90 ukimwambia kulikua na mtu anaitwa Nyerere na alipigana na Id Amin anaona kama story za kutunga hivi

Ila kama haya mambo yangekuwa yanafundishwa tangu shule za msingi , sekondari na mpaka vyuo na kukawa na documents zake ziko public tungekuwa na taifa la watu wazalendo sana aisee
 
Amin usiamini hiyo ilikuwa SHOW OF FORCE tu Jeshi kuwekwa kwenye hali ya Tahadhali wakati wa fukuto ni kawaida katika majeshi yote duniani hiyo isikutishe,kipindi hicho ilikuwa vigumu sana kupigana kwa sababu nilizozitaja,Jeshi letu lisingeweza kuingia vitani kabisa hata kama tungeingia vitani Dunia ingetushangaa kabisa,isitoshe tuna wataalamu wazuri wa kijeshi wasingeruhusu Jeshi letu liingie vitani maana kufanya hivyo ni sawa na kujitoa MHANGA.
 
Sasa mkuu kwa nini Kenya waliamua kuufyata mkia huku wakijua kabisa ile ilikua ni show off tu?

Au intelligence yao ilikua weak kutokuweza kujua kuwa tulikua tunawachimba mkwara tu na hatukua na ubavu wa kupambana vita nyingine???
 
Hili kwangu ni jipya maana kwenye historia ya EAC, niliishia kukariri sababu za kuvunjika tu na hivi nilikuwa nachukia historia ndiyo kabisa hata sijui lolote.
 
Hahaa,
asigwa hii habari umekuwa interested nayo sana mkuu,
Ni vizuri.
 
Sasa mkuu kwa nini Kenya waliamua kuufyata mkia huku wakijua kabisa ile ilikua ni show off tu?

Au intelligence yao ilikua weak kutokuweza kujua kuwa tulikua tunawachimba mkwara tu na hatukua na ubavu wa kupambana vita nyingine???
Mimi sisemi kuwa Kenya ilifyata mkia bali pia aliona ugumu wa wao kuingia vitani kwa haraka haraka bila maandalizi na kwa kitu ambacho si cha mhimu kwa taifa,Ni vigumu sana kugundua hii ni SHOW OF FORCE au ni Real action maana vitendo vyake ni sawasawa kabisa isipokuwa umaliziaji ndiyo huwa tofauti,SHOW OF FORCE mnakuwa na kila kitu ni sawa na wewe unamwendea adui yako unafika mlangoni kwake ukiwa na Panga,Rungu,Nondo na zana zingine harafu unaongea maneno ya kumtisha na wewe kujisifia baadaye ukaondoka polepole bila kumdhuru wala kufanya chochote hiyo inaitwa SHOW OF FORCE kwa lugha rahisi ni kujionyesha mwenye nguvu dhidi ya adui yako,Na hii ni kawaida kwenye Majeshi mengi kukiwa na Fukuto fulani tu Majeshi yanatoka na kuanza Mazoezi ya kijeshi mpakani mwa nchi tuhumiwa au wengine wanafanya Maonyesho ya zana zao za Kivita na wanaita waandishi wa habari wote kuja kushuhudia wakijua habari hizo zitamfikia mlengwa wao hiyo ndiyo inaitwa SHOW OF FORCE aka MKWARA
Kwa wanaojua vita walikuwa wanajua kuwa Tanzania isinge ingia vitani na Kenya kipindi hicho maana uwezo huo ki-ukweli hatukuwa nao sababu ya UCHUMI wetu ulikuwa umedorola,Jeshi letu lilikuwa linajiunga upya(Re-organization)baada ya Vita vya Kagera na Wanajeshi wetu wengi wao walikuwa wamekumbwa na tatizo la Post Traumatic Stress Disorder (PTSD) tatizo hili liliwapata Wanajeshi wengi sana ndiyo maana Wanajeshi wetu waliporudi toka vitani kulikuwa na matatizo mengi sana ya uvunjifu wa amani na Wanajeshi wengi waliweza kuua raia na wakati mwingine wao kwa wao,waliokuwepo kipindi hicho wanaweza kushuhudia vizuri Tatizo hili hutokea baada tu ya vita inapoendelea au vita kumalizika,Ili kulimaliza tatizo hili inapaswa kuwapa ushauri Nasaha Wanajeshi husika.
Kwa hali kama hiyo ingekuwa vigumu sana Jeshi letu kuingia vitani na kupigana na kupata ushindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…