Kwa nini Kenya imeshindwa ku take- off hata baada ya miaka 50 ya Capitalism?



Ndiyo siyo tuu kwamba Singapore wanaizidi Uchina bali Singapore wanazizidi nchi zote za Ulaya ukiondoa labda Uswisi na Luxembourg, wako sawa na nchi ya Sweden kwa utajiri!

Per capital income ya USA ni kubwa kuliko ya Urusi, tena kwa USA imeiacha Urusi kwa kipato cha mwananchi mmoja mmoja kwa mbali sana, na ndiyo maana kuna Warusi wengi wanahamia USA kutafuta maisha bora na ni ishu kupata viza lkn sidhani kama kuna raia wa USA anayetaka kuhamia USA kwa ajili ya kutafuta maisha bora!
 
Ukitaka kujua kwa nini Kenya haijasaidiwa na ubepari soma kitabu cha Prof. Hernando De Soto,
The Mystery of Capital: Why Capitalism Triumphs In The West and Fails Everywhere Else.
 


Sikubaliani na wewe katika hilo, Japani ndiyo nchi ya kwanza kabisa kuendelea Asia na ilikuwa eneo lenye masikini watupu lkn walikuwa wanatrade moja kwa moja na Ulaya na USA isitoshe sehemu kubwa ya trade ya Kenya inakwenda EU, Kenya haiuzi maua na chai au hata Watalii wake hawatoki Afrika, hivyo kusema kwamba kuzungukwa na nchi masikini ndiyo sababu siyo kweli, kama ni hivyo basi Mexiko ingekuwa tajiri kama USA kwa maana ni majirani!
 
Kenya ukabila unawatafuna na hamtaweza kuendelea uchumi wenu unadidimia, maisha ya wachache ndio yenye unafuu 65% ni masikini huwezi kuwa una kundi kubwa la walipa kodi masikini ukategemea uchumi kuimarika Kenya mjitafakari anguko lenu linazidi.
Mi sio mkenya mkuu[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] naona unani adress kama mkenya
 
The way you are adressing the Kenyan economic situation is as if the economy in our country (Tanzania) is in a good state as compared to the 50+ years of independence.
 
The way you are adressing the Kenyan economic situation is as if the economy in our country (Tanzania) is in a good state as compared to the 50+ years of independence.
Usome makala kwanza uelewe kinachozungumziwa umeambiwa Kenya chose capitalism that won Communism. Kenya didn't take place in Southern Africa liberation struggles n hence no sanctions did Kenya face. KENYA had flawless 50 years of independence on a right path. And yet struggling like us.
 
Isitoshe wana-control trade to the so poor neighbors. In short hawana excuse na swali limewashusha mbembwe zao. Wamegundua si kitu.
 
Hivi Kenya ni kanchi kadogo kuliko Singapore, Uswiz au hata Japan eeh,,au unaongelea udogo kiuchumi ?,anyway naona mmeanza kutafuta tundu la kutokea.!
 
Kenya,Kenya,Kenya! Haka kanchi kweli ni mwiba kwa wengi! Mada nzima na utafiti ambatanishi kufuatilia michango humu yaonyesha Watanzania mmemakinika na chochote cha Kenya na maslahi yake! Endeleeni vivyo hivo huku Wakenya wakijenga nchi yao.

Na hebu mleta mada,Take-off kwako wewe ni nini? Kama Mkenya,mimi najua Kenya ili take-off kitambo na inaelekea upeo wa juu hata zaidi!
Nijuavyo pia, mioyoni mwenu mngependa Kenya
isambaratike na kuLand-crash!

Wacheni unafiki!
 
Kenya mnajenga ufisadi na ukabila
 
Uongo mtupu. Russia imekuwa pale pale tangu enzi zile lakini Western Media inaonyesha kuko kubaya...
 
hilo swali halitakiwi kuulizwa na sisi watanzania, especially kama ulishawahi kufika kenya.


Labda kama haujaelewa nilichomaanisha, labda ungeniuliza nikueleweshe, Kenya nakwenda mara kwa mara tena siyo Nairobi tu bali hata Mikoani huko na sehemu nyingi tu ziko underdeveloped, kwanza kuna sehemu nyingi hkn tofauti na TZ yetu au hata kwetu ni bora kidogo isitoshe Mada yangu siyo TZ vs Kenya!
 

Mada za kihivi huwa unazianzisha, ukijibiwa unatoweka halafu baada ya miezi michache unaibuka tena na swali lile lile, na ndio unaona Wakenya hawahangaiki kukujibu maana ushajibiwa mara nyingi tu.

Inafaa ikuingie kwamba mfumo wa nchi sio sababu pekee ambayo inawezesha nchi kuboreka kiuchumi, cha msingi na muhimu ni uwezo wa wananchi wa nchi husika kujituma. Afrika hii, hata majirani zenu wote akina Zambia, Malawi n.k. wote walikumbatia ubepari, lakini bado mnaorodheshwa pamoja kama mataifa maskini wa kutupwa dunia hii.

Ukiangalia hata Uganda ambayo haina eneo kame kama ilivyo Kenya, pia mpo kwenye kundi moja. Nchi yetu ni mfano wa kuigwa, maana nusu yake ni kame tupu, jangwa lakini hatupo nanyi kwenye kundi la maskini. Nyie kilichowaponza, ni kwamba hamkuuelewa mfumo wa communism, ilikua ni kazi ya mtu mmoja tu Nyerere ambaye hakutaka kushauriwa, mkaishia kuwa wavivu na wazembe hadi liinchi likubwa, yaani muungano wa nchi mbili zenye kila aina ya raslimali lakini maskini hadi noma.

Siri ya Kenya ni kujituma, huwa tunajituma kwa kwenda mbele, ni kweli hatuwezi kujilinganisha na Japan, wapo mbele yetu, ila inafaa uelewe wale walianza mapinduzi ya viwanda (industrial revolution) mwaka wa 1870 wakati huku tukiwa gizani. Na mataifa yote yaliyowazunguka walipata huo mwanga, lakini sisi huku tumezungukwa na mivivu.
 
Mimi kila siku huwa nasema haya, nilipokuwa mdogo miaka ya 90's mama yangu alikuwa akienda kununua mahitaji ya nyumbani, yaani Chumvi, sabuni, sukari, vipodozi, Mafuta ya kula n.k karibu vyote vilikuwa 'Made In Kenya'
And my question is what was that export value meant to Kenya? Kwa ile nafasi mliyokuwa nayo nadhani Leo 2018 mlitakiwa muwe kama South Korea,
What happened to you guys? Leo 2018 maelfu kwa Maelfu wanakufa kwa njaa, juzi hapa tumeshuhudia kwa Mara ya kwanza baadhi ya counties zenu zinaona Lami for the first time, ufukara wa kufa mtu,
What happened to you?
 


Ndo hoja yangu ilipo, ni kwa nini Kenya na nchi nyingine za Kiafrika ambazo zime-practice capitalism kwa zaidi ya miaka 50 zimeshindwa ku-takeoff ukilinganisha na nchi za Mabara mengine? Kwanza nafikiri ukiondoa AK sidhani kama kuna nchi nyingine ya Kiafrika ambayo imekuwa na pure capitalism na stability kama Kenya, nchi kama Uganda wamekuwa na coup detat nyingi nafikiri Uganda wamekuwa na Maraisi zaidi ya 6, lkn Kenya haijakuwa na shida yoyote, no civil war, no sanctions, Kenya imekuwa ikitrade freely kila mahali hata Ethiopia walikuwa na socialism enzi za akina Mengistu Haile Mariam, lkn leo hii wako vizuri kidogo, sasa kwa nini ndiyo swali langu!
 

vipi kuhusu Swaziland mbona wamezungukwa na South Africa nchi iliyoendelea zaidi Africa na wao ni maskini wa kutupwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…