Kwa nini Kenya imeshindwa ku take- off hata baada ya miaka 50 ya Capitalism?

Ila wao na sisi wa TZ kupi kuna afadhari..
Hujaelewa swali au tuite mada kuu.
Rudia kusoma utaliewa swali la msingi.

Tanzania haikufuata njia ya ubepari kwa miaka yote.

Na mleta mada hajasema Tanzania ipo juu kimaendeleo/kiuchumi kuliko Kenya. In fact amesema Kenya bado inahangaika na matitizo yale yale yanayowakabili nchi wajamaa kama Tanzania wakati wao walifuata ubepari njia inayo aminika ni sahihi ktk kuimarisha uchumi na maisha bora ya wananchi ktk nchi husika.
 
Hujajibu swali...

Zaidi umeanza kulinganisha tuu uganda na tz pamoja na kujisifia...

Mjibuni mleta mada, kenya hamkupata vikwazo vyovyote vya uchumi nje na ndani ya bara la afrika, hamkupata vita kama Uganda na Tz, ndani ya miaka 50 mlikuwa mnateleza tuu kwa kufanya shughuli za kiuchumi wakati majirani zenu Rwanda wakichichanjana, Uganda na Tz wakipigana pamoja na vikwazo vingi..

Kwanini sasa hali yenu haipishani sana na hawa wengine ambao walikumbwa na matatizo kibao?
 
Hivi Kenya ni kanchi kadogo kuliko Singapore, Uswiz au hata Japan eeh,,au unaongelea udogo kiuchumi ?,anyway naona mmeanza kutafuta tundu la kutokea.!
Kenya si inchi ndogo
 
vipi kuhusu Swaziland mbona wamezungukwa na South Africa nchi iliyoendelea zaidi Africa na wao ni maskini wa kutupwa

Nani kakudanganya Swaziland ni maskini wa Kutupwa? Hivi unaelewa GDP per capita ya Swaziland ni mara tatu ya Tanzania?
 
Kenya imesimama tofauti yetu na nyie ni kuwa sisi hatuna njaa ila hatupo huru nyie mna njaa ila mpo huru
 
Kenya ina masikini wengi wa kutupwa tatizo ni watu (matajiri) wa chache wanaoshikilia uchumi wa inchi ila sisi Tanzania tunaimarika kwa mtu mmoja mmoja tukiwa na Sera ya kuthamini na kuendeleza wafanya biashara wazawa miaka 3 tutawaacha mbali.
 
Wanaendelea kuwa masikini wakutupwa tatizo uchumi wao umeshikiriwa na matajiri wachache wanaoamua kwa maslahi yao lakini wanainchi wa Kenya ni masikini wa kutupwa naamini miaka 5 ijayo tutawaacha mbali Kenya.
 
Tatizo ni uchumi kuwa chini ya matajiri wachache wanao amua kwa maslahi yao huku wanazaliana masikini wanaozidisha mzigo na ghalama kwa serikali
 
vipi kuhusu Swaziland mbona wamezungukwa na South Africa nchi iliyoendelea zaidi Africa na wao ni maskini wa kutupwa
Africa kuna shida ya uzalendo aliyepata hataki wengine wapate anataka wote wamutumikie umasikini hautokwisha mpaka pale kitakapozaliwa kizazi cha kizalendo
 

Kitu kingine unafaa kukielewa, Kenya ilikua chini ya utawala wa chama kimoja dhalimu kama CCM ilivyo kwa Tanzania, ni baada ya kukiondoa madarakani ndio Kenya ika-take off at turbo speed, leo hii ukanda wote huu mataifa yote yapo nyuma yetu.
 
Nani kakudanganya Swaziland ni maskini wa Kutupwa? Hivi unaelewa GDP per capita ya Swaziland ni mara tatu ya Tanzania?


Lkn ni
Kitu kingine unafaa kukielewa, Kenya ilikua chini ya utawala wa chama kimoja dhalimu kama CCM ilivyo kwa Tanzania, ni baada ya kukiondoa madarakani ndio Kenya ika-take off at turbo speed, leo hii ukanda wote huu mataifa yote yapo nyuma yetu.


Hiyo sidhani kama ni sababu kwani hata AK imeongozwa na Chama kimoja miaka yote mpaka mwisho wa apartheid na ndiyo kilichojenga Uchumi wa AK, Taiwani, Korea Kusini na hata Japani hawajawahi kubadilisha Chama, kwanza Japani inaongozwa na Chama kimoja tangu mwaka 1945, mpaka leo hii, Korea ilijengwa na military dictatorship chini ya Park, hivyo hiyo haiwezi kuwa ni sababu!
 

Nimesema chama dhalimu kama ilivyo CCM huko kwenu, mkiwa na chama kimoja tangu uhuru halafu chenye kudhalimu watu wake na kuendekeza ufisadi, mtakwama sana. Nakumbuka kipindi cha Moi ilifikia hadi tukapigwa economic sanction na Ulaya.
Sisi tumeweza ku-take off baada ya kukiondoa hicho chama na uongozi wake. Labda na nyie mtaokoka siku mtathubutu, lakini kwa jinsi CCM imekita mizizi, hamtoweza, muendelee kubaki nyuma yetu.
 


OK , kama hiyo ndiyo sababu ya Kenya kushindwa, lkn Mada yangu haihusu TZ vs Kenya!
 
OK , kama hiyo ndiyo sababu ya Kenya kushindwa, lkn Mada yangu haihusu TZ vs Kenya!

Hamna sehemu nimesema Kenya imeshindwa, nimesema tulicheleweshwa na CCM ya Kikenya kama mnavyocheleweshwa na CCM yenu.
Tulipoitoa madarakani, Kenya ilipaa sana tangu enzi za rais Kibaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…