Kwa nini Kila Samia akikosolewa inasemwa ni udini?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Sijaelewa ni kwa nini Kila akikosolewa Samia Suluhu Hassan ndani ya chama chake ama kama Rais hoja kuwa ukosoaji huo unatokana na dini yake huibuka.

Hivi ni Rais gani wa nchi hii ambaye hajawahi kukosolewa. Jee walipokosolewa Nyerere,Mwinyi, Mkapa, Kikwete au Magufuli hao Marais walikuwa hawana dini?

Mwalimu Julius Nyerere alitaka kupinduliwa mara mbili wakati wa utawala wake (1964,1982). Jee waliotaka kumpindua walifanya hivyo kwa kuwa alikuwa ni Mkristo?

Mzee Ali Hassan Mwinyi aliitwa Kila aina ya majina ya kejeli na wapinzani wake. Jee hao waliomwita hayo majina walikuwa wanamwita hivyo kwa kuwa yeye ni Muislamu?

Alipoingia Benjamini Mkapa alifanya mambo mazuri na mabaya, lakini wakosoaji wake walimkosoa kwa kuwa ni Mkristo?

Alipokuja Jakaya Kikwete alifanya mambo mema na mabaya, lakini alikosolewa Kila Kona kwa mambo kadhaa wa kadhalika. Jee na yeye alikosolewa kwa kuwa ni Muislamu?

John Magufuli nadhani hakuna rais aliyekosolewa vikali na watanzania kama yeye. Jee alikosolewa kwa kuwa ni Mkristo?

Kwa nini Samia Suluhu Hassan akikosolewa inaibuka hoja kuwa Samia anakosolewa kwa kuwa ni muislam? Lengo la hoja hii ni nini?
 
Wewe unaongoza kwa mada za udini na ubaguzi wakati umeajiriwa na muislamu na kila siku unakula bidhaa za Azam na MoDewji
 
Wewe unaongoza kwa mada za udini na ubaguzi wakati umeajiriwa na muislamu na kila siku unakula bidhaa za Azam na MoDewji
Leta hoja acha uzushi. Hizi simu tunazotumia kujibishana hazijaundwa na waislamu Wala wakristo. Zimeundwa na wachina wafuasi wa Buddha waabudu sanamu.

Yaani akikosolewa Samia mnarukia kuwa anakosolewa kwa kuwa ni Muislamu. Wakati Tundu Lissu anamwita Magufuli "Dikteta uchwara" ilikuwa ni nini?
 
CCM wanatumia kila mbinu kubakia madarakani.
Udini ndiyo Gia ya mwisho Kwa kiongozi mpumbavu
 
Hawana kitu udini ndiyo mtaji
 
Hiyo tabia alianzisha Kikwete alipobanwa na Slaa,nakumbuka Lipumba ilibidi aanze kumpigia kampeni kwa mlengo wa dini,kwa hiyo anafuata nyayo za boss wake
 
Maana ndio njia mbadala ya kumuwezesha kufika kileleni
 
nadhani kubwa tumeona wakati wa magufuli watu walikuwa kimya ikiwemo baadhi viongozi wa kanisa ila sasa ukosoaji umekuwa mkubwa hata kwa yale yaliyofumbiwa macho na wakosoaji kwa nyakati za jiwe.
 
nadhani kubwa tumeona wakati wa magufuli watu walikuwa kimya ikiwemo baadhi viongozi wa kanisa ila sasa ukosoaji umekuwa mkubwa hata kwa yale yaliyofumbiwa macho na wakosoaji kwa nyakati za jiwe.
Taja kanisa lilo kua kimya kama romani ulichapwa waraka kuna Mpaka Askofu wa alinyanganywa hati ya kusafilia Kipindi cha kovid 19 Father Kitima alimkosoa wazi wazi Magu tena Roma alimkosoa sana Magu kuzidi mama Kuna Askofu mkuu wa Jimbo la Dar wa Roma Ruachi Wewe Magu alipigwa spana
 
Acheni kumsumbua jamani hata afurahi na familia yake usiku huu
 
Ndio ngao, wametoka kusema ni mwanamke tokea aanze utekaji ameacha kusema jinsia yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…