Huo ndiyo ukweli. Samia anachukiwa kwa Uzanzibari wake, Uislamu wake na kwamba ni mwanamke.Leta hoja acha uzushi. Hizi simu tunazotumia kujibishana hazijaundwa na waislamu Wala wakristo. Zimeundwa na wachina wafuasi wa Buddha waabudu sanamu.
Yaani akikosolewa Samia mnarukia kuwa anakosolewa kwa kuwa ni Muislamu. Wakati Tundu Lissu anamwita Magufuli "Dikteta uchwara" ilikuwa ni nini?
Nakupinga kwa kumbukumbu sahihi. Magufuli alikosolewa na wakatoliki wenzake waziwazi kuhusu COVID-19.nadhani kubwa tumeona wakati wa magufuli watu walikuwa kimya ikiwemo baadhi viongozi wa kanisa ila sasa ukosoaji umekuwa mkubwa hata kwa yale yaliyofumbiwa macho na wakosoaji kwa nyakati za jiwe.
Ni wakati gani nchi ilikuwa haijatulia? Hii nchi kinachokosekana ni HAKI, haya mambo ya kutulia tumetulizwa kitambo sana.Huo ndiyo ukweli. Samia anachukiwa kwa Uzanzibari wake, Uislamu wake na kwamba ni mwanamke.
Despite all odds ameweza kuuituliza nchi, kujenga uchumi na miundombinu na kuboresha demokrasia na utawala bora.
Iko siku akishatoka watu wataikubali kazi yake