Kwa nini mashabiki wa Yanga huamini Simba ni mbovu kuliko Timu yao?

Kwa nini mashabiki wa Yanga huamini Simba ni mbovu kuliko Timu yao?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kila wakati Takwimu huwa zinasema tofauti na wana- Yanga wanavyoaminishwa na watu wao wanaowaamini. Juzi Kati hapa almanusra Manara awadanganye Yanga kwamba haijawahi kutokea Timu ya Tanzania kuongoza kundi kwenye mashindano ya CAF ikiwa na Pointi 13.

Alipokumbushwa kwamba simba iliwahi kuongoza kundi Ligi ya Mabingwa ikiwa na Pointi hizo 13, akakaa kimya. Lakini Takwimu zile zilishaanza kushadadiwa na watu wa Yanga kwa kasi ya ajabu sana.

Simba inaongoza kwa kuwa na magoli Mengi kwenye Ligi Kuu Tanzania, lakini mashabiki wa Yanga wameaminishwa kwamba Simba eti ndiyo yenye Fowadi mbovu sana kuliko wao. Inakuwaje Simba inayoipita Yanga magoli ya kufunga kwa tofauti zaidi ya magoli 10 eti yenyewe ndiyo iwe na fowadi mbovu?

Pia kuna hoja hii ya kwamba Simba haijawahi kuifunga Yanga tangu mwaka 2019, hii hoja ni ya kweli lakini imetiwa chumvi mno. Namshukuru sana JanguKamaJangu ambaye ameweka takwimu hizi hapa chini.

29/04/2018: Simba 1-0 Yanga

30/09/2018: Simba 0-0 Yanga

16/02/2019: Yanga 0-1 Simba

04/01/2020: Simba 2-2 Yanga

08/03/2020: Yanga 1-0 Simba

07/11/2020: Yanga 1-1 Simba

03/07/2021: Simba 0-1 Yanga

11/12/2021: Simba 0-0 Yanga

30/04/2022: Yanga 0-0 Simba

23/10/2022: Yanga 1-1 Simba

Kwa takwimu hizi inakuwaje watu wa Yanga wadhanie kwamba kuanzia mwaka 2019 Simba imekuwa dhaifu kwao??
 
Hawana la kusema leo wamefungwa midomo pamoja na mwiko wao huko nyuma
Takwimu zinaongea tofauti na makelele yao kwamba wao ni bora kuliko Simba!! Wote walikuwa Klab Bingwa, wenyewe wameshindwa kusonga mbele simba inaendelea Klab Bingwa Afrika wenyewe wapo Shirikisho. Lakini bado wanadai Simba kuendelea kwao ni kwa sababu huwa anakutana na timu Dhaifu!!
 
Kesho redio zote zitampamba kibu denis wakati walisema mbovu bongo bwana hatuna wachambuzi tuna bendera fuata upepo tu
Yaani kila wakifanya huo uchambuzi wao ni lazima waoneshe kwamba Simba haina ubora na hata kwenye kushinda mechi za kimataifa wao huipa Yanga kipaumbele. Yaani kabla ya Mechi ya leo walivyokuwa wanaizungumzia Yanga utadhani ni ile Barcelona ya Guadiola!!
 
Kila wakati Takwimu huwa zinasema tofauti na wana- Yanga wanavyoaminishwa na watu wao wanaowaamini. Juzi Kati hapa almanusra Manara awadanganye Yanga kwamba haijawahi kutokea Timu ya Tanzania kuongoza kundi kwenye mashindano ya CAF ikiwa na Pointi 13.

Alipokumbushwa kwamba simba iliwahi kuongoza kundi Ligi ya Mabingwa akiwa na Pointi hizo 13, akakaa kimya. Lakini Takwimu zile zilishaanza kushadadiwa na watu wa Yanga kwa kasi ya ajabu sana.

Simba inaongoza kwa kuwa na magoli Mengi kwenye Ligi Kuu Tanzania, lakini mashabiki wa Yanga wameaminishwa kwamba Simba eti ndiyo yenye Fowadi mbovu sana kuliko wao. Inakuwaje Simba inayoipita Yanga magoli ya kufunga kwa tofauti zaidi ya magoli 10 eti yenyewe ndiyo iwe na fowadi mbovu??

Pia kuna hoja hii ya kwamba Simba haijawahi kuifunga Yanga tangu mwaka 2019, hii hoja ni ya kweli lakini imetiwa chumvi mno. Namshukuru sana JanguKamaJangu ambaye ameweka takwimu hizi hapa chini.

29/04/2018: Simba 1-0 Yanga

30/09/2018: Simba 0-0 Yanga

16/02/2019: Yanga 0-1 Simba

04/01/2020: Simba 2-2 Yanga

08/03/2020: Yanga 1-0 Simba

07/11/2020: Yanga 1-1 Simba

03/07/2021: Simba 0-1 Yanga

11/12/2021: Simba 0-0 Yanga

30/04/2022: Yanga 0-0 Simba

23/10/2022: Yanga 1-1 Simba

Kwa takwimu hizi inakuwaje watu wa Yanga wadhanie kwamba kuanzia mwaka 2019 Simba imekuwa dhaifu kwao??
Kwa sababu wao ni hamnazo.
 
Inashangaza sana sijui hizo takwimu wamezitoa wapi
Screenshot_20230416-222647_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom