Asalaam Aleykum wana JF,
Ama baada ya salamu hizo, niingie kwenye hoja.
Mara nyingi na kwenye jamii nyingi, matajiri na watawala huogopa mabadiliko kwa sababu yanatishia maslahi yao tofauti na wanyonge ambao wengi wao hawana cha kupoteza zaidi ya kupoteza umaskini na unyonge wao.
Haya yaliwahi kusemwa pia na Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, akiwashangaa wana Ujamaa ambao walikuwa wakihofia sera za mabadiliko toka kwenye sera za ubwanyenye na unyonyaji kuingia kwenye ujamaa.
Bahati mbaya sana, hawa watu (matajiri na watawala), huwa wana sauti kubwa sana kuliko wanyonge na watu wa chini. Mara nyingi wakiona maslahi yao yanaguswa, basi huwatumia hao hao wanyonge kupiga kelele kuonesha ubaya wa mabadiliko hayo.
Inahuzunisha sana, tena sana kuona kwenye nchi tajiri kama Tanzania, baadhi ya watu wanaishi maisha ya tabu kiasi kwamba hawana uhakika hata na kula kwao milo miwili kwa siku ilhali wengine wanaishi maisha ya anasa ya kwenda Dubai kila weekend kula bata!
Hii hali haiwezi kuachwa hivi hivi iendelee huku pengo la walio nacho na wasio nacho likizidi kuongezeka.
Naunga mkono kampeni ya CHADEMA ya NO REFORMS, NO ELECTION.
Hii itatusaidia kupata viongozi ambao tutakuwa tumewachagua wenyewe na watakaofanya kazi kwa wivu mkubwa kwa nchi na kwa wale waliowachagua.
Hatutaki tena kuongozwa na waliohongwa vyeo na uongozi au waliopata uongozi kwa kununua n.k.
MABADILIKO KIPINDI HIKI NI LAZIMA, WATAKE AU WASITAKE.
MUNGU IBARIKI NO REFORMS, NO ELECTION.