Elections 2010 Kwa nini Michuzi aling'aka ailipoambiwa anapigia kampeni CCM?

Elections 2010 Kwa nini Michuzi aling'aka ailipoambiwa anapigia kampeni CCM?

nimetembelea michuzi blogsport ya ankali michuzi nakuta picha zote ccm, pamoja na CUF na chadema kuzindua kampeni zao hakuna picha za vyama hivyo kwenye "globu ya jamii".najua ankali ndo walewale ila kama blog yake kaamua kuipa jina la globu ya jamii angekuwa fair la sivyo aamue moja na muwazi kuipa jina la globu ya ccm kwani ni haki yake kutumia blog yake kupiga kampeni kwa chama anachokitaka badala ya kutuchanganya sisi wanajamii
 
Michuzi ni mjasiriamali, anamtumikia highest bidder, 'blogu ya jamii', hiyo ni lugha ya biashara tuuuuuu ili ujisikie 'uko nyumbani'.
 
Unasema kwamba Michuzi ni bias on the news; sasa na wewe mwenyewe pia ni bias. Angalia kichwa cha habari chako "habari za CHADEMA" kwani Chadema kipo peke yake? Don't judge others; before you look at yourself.

Acha kukurupuka wewe.Soma mstari wa kwanza wa post yangu....nimetoa intro kwa kuonesha kuwa haposti habari za vyama vya upinzani.Nimeweka kichwa cha habari namna hiyo kwa kuwa siku kama ya leo ungetemea habari za CHADEMA zitapewa nafasi kubwa kwenye vyombo vingi vya habari.Jifunze kusoma na kuelewa kabla hujaamua kujibu tu ukidhani una uhakika na unachokifanya!
 
Well, Waandishi Wengi Wa Tanzania sio 100% Independent... Michuzi ni Mfanyakazi was Serikali ya Tanzania kwa Miaka Mingi na nadhani Mfanyakazi wa Serikali haruhusiwi kujuhusisha na Masuala ya Upendeleo wa Siasa za kipinzani. Well Ningependa kusikia Mengi ya Upinzani wa CCM toka kwa Michuzi lakini lazima tufikirie his life survival. Niko Nje ya nchi kwa Muda Mrefu na nafuatilia blog ya Michuzi lakini ninamuamini.
Ningenda sana Masuala ya kusikia upinzani was CCM lakini nani atadhubutu? Waandishi wetu hawan mtaji wa kujiendeleza bila Msaada. Labda kweli tunahitaji katiba Mpya... Kuondoa Madaraka ya nguvu ya Rais kama kuteua hata Region Development Directors i guess (RDD's).

Mbona Hamlalamikii IPP Media -- It is a Joke Nowadays...

Asanteni... MICHUZI OYEE...
 
duh.. hivi hata mmepitia au mnaandika kwa kukisia tu? Jamaa kawaweka mapicha kote kwenye Blog na kwenye site yake ya news ya Michuzipost.com Vingine inabidi nyinyi wenyewe muanzishe na blogs jamani..mbona zipo nyingine.
 
CHADEMA sasa watakua kimyaaaaaaaaaa...kazi kukurupuka tu..oooh Michuzi haweki picha zenu..haya hizo hapo sasa!!! Mnataka kuongoza nchi hata hamna mpiga picha!!!

Kaka hapa utakuwa unawakosea CHADEMA kudai kuwa wanakurupuka na kulilia Michuzi kuweka habari zao. Kwa uelewa wangu, naamini kuna memba mmoja hapa ndiye aliuliza kwa nini Michuzi haweki habari za CHADEMA.
Kwa nini tupindishe ukweli hapa kwa kushabikia chama fulani? Let us be real. Blogs ziko nyingi tu but CHADEMA hawajawahi kulalamikia blog ya Michuzi......come on.
 
Hata akishinda CCM mwaka huu basi atashinda kwa tabu saana.. ila sitashangaa kusikia kikwete kashinda kwa asilimia zaidi ya 90.. haha demokrasia yetu ya afrika .. hiii inasikitisha kweli
 
Kaka hapa utakuwa unawakosea CHADEMA kudai kuwa wanakurupuka na kulilia Michuzi kuweka habari zao. Kwa uelewa wangu, naamini kuna memba mmoja hapa ndiye aliuliza kwa nini Michuzi haweki habari za CHADEMA.
Kwa nini tupindishe ukweli hapa kwa kushabikia chama fulani? Let us be real. Blogs ziko nyingi tu but CHADEMA hawajawahi kulalamikia blog ya Michuzi......come on.


Watu mnakurupuka tu humu ndani mna ushabiki bila kutafakari namna hii hatuwezi kufika kwa mawazo mfu. Mbona mimi nimezipata habari za kuanza kwa kampeni za Chadema kupitia Michuzi Blog? Na picha za Mbowe na Sla zimewekwa pamoja na mgombea mwenza pengine wengine hamna habari kuwa Chadema ndio wameanza Kampeni watu usingizi sana humu ndani!!!!!!!!!
 
Michuzi namfahamu fika, kwa maoni yangu binafsi, hana ubaguzi ila nadhani kuna uwezekano hakuna yoyote anayempelekea habari za Chadema, hivyo kama hapelekewi, afanyaje?.

Hebu nyie wapenzi wa Chadema, mrushieni habari za Chadema muone kama hata zitoa.

Ila pia Michuzi nae nibinadamu tuu kama wengine, na kazi za uandishi wa kibongo nazijua fika na msoto wake pia naujua.
Wale waandishi wote ambao sio makini, waliobahatisha kwenye fani, ama wababaishaji, the only means za survival ni kujikomba komba kwa wenye nazo, inawezekana kujaa sana kwa CCM kwenye Michuzi blog, has something to do na survival ya ankal!.

Guys, it is very simple, kama hutaki kujua habari za CCM usiingie kwenye blog ya michuzi, manake kwanza anamuita JK Dr na amesheheni picha kibao za JK huko kwenye kampeni. Za vyama vingine anadonoa tu, kama leo kaweka picha mbili tatu za chadema, wakati mdogo wake-Michuzi Junior Jiachie blog katundika mipicha kibao ya kampeni za chadema

So ukitaka kujua habari za Chadema tembelea Jiachie na JF, ukizitaka za CCM hata ukitaka kuona JK akibeba watoto wadogo au akiahdi baskeli ya matairi matatu kwa mlemavu basi usihangaike ingia michuzi Lol
 
Mimi naona imepoteza dira. Sasa ni Blog ya makulati, birthdays, CCM na imeacha yale mambo ya msingi.

naona ipo kibiashara zaidi. Inaangalia pesa na mambo ya kijamii imeyasahau.
 
Angeeka picha na habari ya bob makani kupiga mwereka ingekuwa imekamilika kuwa ya jamii na si hivi ilivyo ambapo haielezei dr.silaha alikuwa anafanya mchezo gani bafuni mpaka akapiga mwereka.....!
 
Hata akiwa kwenye msafara wa Kikwete. Mbona huwa akisafiri nje ya nchi bado blog inakuwa updated na habari za nyumbani?
Ana vijana anaofanya nao kazi.

Anaudhi sana Michuzi. Halafu kama mfanyakazi wa serikali anavaa na kupiga picha na vitambulishi vya CCM -picha aliyoweka akisema ni birthday yake, yuko Kigoma, amevaa cap ya CCM.

Ajitokeze tu wazi na kusema kuwa yeye ni kada na mwanachama wa CCM, kwani dhambi?

unashangaza kama sio kusikitisha kwani akiwa CCM ni dhambi au anakuudhi kwa lipi?! au unataka afate matakwa yako wewe? labda wamekuudhi wengine sio huyo Michuzi.:confused2:
 
sitaki kumtetea michuzi wala ccm. Kama sikosei yeye alisema hao vyama vingine mfano chadema na wengineo hawana njia ya kufanya publicity ya vyama vyao na shughuli zao. Wao wanahisi kila mtu atawafuata. Asilimia karibu 98 za habari za ccm kwa michuzi zinatumwa kwake, na hao wa chadema mpaka aende mwenyewe (mfano siku mbowe kamtangaza dr slaa kuwania urais) yaani hata video aliweka.

Halafu wewe mutu inaonesha umetumwa ama una chuki binafsi na michuzi ambaye wala halipwi na wewe wala nini. Wewe umemkazania kuwa ni kada wa ccm kwani tatizo liko wapi? Hivi kuwa mjanja ama mtu sawa lazima mtu uwe chadema.

Mnamfagilia dr slaam mnamkumbuka mrema na nccr yake alivyokuwa anasomba watu na siku ya siku ikawaje? Mnamkumbuka nyerere aliwaambia watu jangwani pale kama mtu anapenda kubebwa kama maiti mwacheni sio kosa, dr slaa kwa lipi hasa?? Hayo madesa ya epa na richmod ambayo tumeshachoka kusikia (hamna mengine) mbona yeye hatuzungumzii alivyotemwa na kanisa? Mnataka tumwage mtama hapa??

Nyie chadema wachache wenye njaa msio ne kuwa ccm ni dhambi. Dhambi iko katika kuongozwa na ngo ya ukoo inayoitwa chama cha siasa. Upumavu tu umewajaa. Mumkome michuzi wa watu.
mtu kama huyu, mwenye fikra duni na uwezo mdogo wa kupambanua mambo, hasa pale watu( wapinzani) wanapoleta mawazo mbadala juu ya mustakabali wa nchi hii, anahitaji msaada wa wana- wana jf
amekuja kwenye jamvi sahihi ambapo ataelimishwa na kueleweshwa, wala asiijibiwe kwa matusi kama yeye alivyoona ni njia bora ya kufikisha ujumbe, bali ajibiwe kwa hoja, na hata kama hatakiri atakuwa ameondoka na kitu cha manufaa ya kwake binafsi na familia yake, if at all he/she has one.
 
Bendera si kapigwa chini ubunge unaweza michuzi anataka take charge
 
Sitaki kumtetea Michuzi wala CCM. Kama sikosei yeye alisema hao vyama vingine mfano CHADEMA na wengineo hawana njia ya kufanya publicity ya vyama vyao na shughuli zao. Wao wanahisi kila mtu atawafuata. Asilimia karibu 98 za habari za CCM kwa Michuzi zinatumwa kwake, na hao wa CHADEMA mpaka aende mwenyewe (mfano siku Mbowe kamtangaza Dr Slaa kuwania Urais) yaani hata video aliweka.

Halafu wewe Mutu inaonesha umetumwa ama una chuki binafsi na Michuzi ambaye wala halipwi na wewe wala nini. Wewe umemkazania kuwa ni kada wa CCM kwani tatizo liko wapi? Hivi kuwa mjanja ama mtu sawa lazima mtu uwe CHADEMA.

Mnamfagilia Dr Slaam mnamkumbuka Mrema na NCCR yake alivyokuwa anasomba watu na siku ya siku ikawaje? Mnamkumbuka Nyerere aliwaambia watu Jangwani pale kama mtu anapenda kubebwa kama maiti mwacheni sio kosa, Dr Slaa kwa lipi hasa?? Hayo madesa ya EPA na RICHMOD ambayo tumeshachoka kusikia (hamna mengine) mbona yeye hatuzungumzii alivyotemwa na kanisa? Mnataka tumwage mtama hapa??

Nyie CHADEMA wachache wenye njaa msio ne kuwa CCM ni dhambi. Dhambi iko katika kuongozwa na NGO ya ukoo inayoitwa chama cha siasa. Upumavu tu umewajaa. Mumkome Michuzi wa watu.

...changanya na za kwako...
 
..Michuzi na Raisi Kikwete ni marafiki.
Hapo ndio ninapomkumbuka Nyerere, enzi zake mja kama huyu thubutu kumsogelea Rais au misafara yake. Siku hizi kina Michuzi wa dunia wanampigia Kikwete anapokea mwenyewe.

STA70161-1.jpg
 
Back
Top Bottom